Katika kozi ambazo zinaongoza kwa watu wake kutokuwa na ajira ni Computer science, Information Technology and nyinginezo za Technology. Ni ajabu lkni ukilinganisha na nature ya ulimwengu wa sasa, ila ndio uhalisia.

Jambo kubwa linalofanya watu hawa kukosa ajira ni kosa ambalo linafanya mavyuoni bila kutambua, vyuo vinajikita katika kuwa expose(funulia) katika ulimwengu mzima wa IT nakusahau kwa fanya wachague mapema sehemu gani wanatakiwa wajikite kwa isiyopungua miaka 2 ya mwisho ya masomo yao.

Kwa kutambua hilo nimejaribu kuchambua maeneo kadhaa unaposoma chuo unahitaji kujikita kulingana na soko halisi huku njee.


Cyber Technology

Hili eneo linahusika na ulimwengu wa Mtandao wa Internet na Network, jinsi gani connection zinafanyika kati ya watu na vifaa na programu mbali mbali, kwa ufupi ukijikita katika cyber technology utajikita zaidi katika ku maintain security ya mifumo isidukuliwe na kulinda data za watu katika mifumo hiyo, hawa watu ni muhimu sana katika kila organization inayotumia mifumo na yenye data nyeti sana mfano serikali, benki na maeneo yanayofanya tafiti na sasa hata chaguzi...

Njia.

Kwanza uwe katika kozi kama computer science au IT,  halafu unatakiwa usomee vyeti vya ujuzi maalumu mfano CompTIA Security+ na Certified Ethical Hacker (CEH) na pia ujichanganye katika mashindano mbali mbali ya mambo hayo yanayotokea ili kujinoa.

Ila vyovyote ufanyavyo unatakiwa uji-update katika Artificial Intelligence maana inachukua nafasi kubwa sana, marobot ndio yanahack siku hizi, na Ai ndio ina ulinzi mkali kuliko watu, so unaweza soma ukashangaa anaajiriwa robot anaitwa Junior kutoka uswisi 😂

KAZI

Peleka CV yako maeneo kama Benki, Nafasi zikitoka serikalini zaidi TCRA, na makampuni ya mitandao ya simu


Application Development

Bila ubishi tunahitaji Apps siku hzi kwa hali na mali na bei ya App moja sasa, unaweza ukajisikia kizungu zungu...kwa sababu wataalamu ni wachache sana na bado tuna mahitaji mengi sana ya App kwa ajili ya mazingira yetu ya Africa, Tanzania.

Njia

Ngoma iko wazi, tutorial lundo mtandaoni chuoni usimuone Prof wa watu yeye ni mkufunzi wewe ndio mhusika haswa na Tech inabadilika kwa speed kubwa sana, ingia website za matorrent badala ya kudownlaod movies download udemy tutorials katika Lugha za Apps kama Javascript na mifumo mbali mbali...YOutube kuna professional watakueleza 1 mpka 10, pa kuanza hadi pa kumaliza.


Server/Computer troubleshooting, maintenance and installation.

Hapa kuna wataalamu wengi ila wamejikita zaidi katika maeneo ya kawaida sana, yaani kutengeneza computer za kawaida tuu, ila katika upande wa servers ni wachache sana, kila kampuni kubwa inahitaji server kuweza kutumia programu za ERP, na nyinginezo nyingi tuu...Lkni pia kutokana na kuboreka kwa mtandao wa Internet, makampuni mengi yamekuwa yakitumia server za njee ya nchi maana kutunza server computer imekuwa gharama sana kuliko kulipa kwa wenye nazo.


Njia

somea Microsoft Certified Solutions Expert (MCSE), CompTIA Server+, Red Hat Certified Engineer (RHCE) na VMware Certified Professional-Data Center Virtualization (VCP-DCV), masomo haya yanapatikana mtandaoni na utabidi ulipie, ili uwe mzuri katika IT ni lazima uingie gharama no shortcut, vyeti hivyo vitakuitisha kwenye interview haraka sana.


Software Sales, maintenance and installations.

Huku unajikita zaidi katika kuuza Programu za kitaalamu, za mifumo mbali mbali ya kuendesha makampuni au taasisi  mfano hospital management, school management, church management N.K 


Njia

Unahitaji unavyosoma uzitatute hizi programu uelewe zinavyofanya kazi na uanze kuziuza, au wewe utengengeneze za kwako. soko lipo kubwa , sehemu nyinginr unahitaji kutoa elimu kabla ya kuuza ila zinahitajika sana hadi sasa.


Network Installations and Maintenance and security.

Eneo hili linahusika na kufunga mtandao kwa njia ya nyaya na bila wire, pamoja na maendeleo makubwa ya teknolojia, badi tunahitaji waya kwa sababu zina ulinzi mzuri wa kuto kutoa nafasi ya kudukuliwa, na pia nimejumuisha kufunga mifumo ya camera za ulinzi kwenye majengo.


Njia

Nenda kasome vyeti vya cisco na pia kaa na wataalamu wa mifumo ya security camera, kama hakuna vyeti hata ujuzi wenyewe unaweza andika katika CV yako ikawa safi sana, na ukapata ajira au kipato haraka.


Computer Rent and sales

Kama una uwezo wa kupata mtaji, fungua duka la kuuza computers au laptops. siku hizi taasisi nyingi zinapenda kukodi computer kwa muda maalumu na kukulipa, kama ukiwa nazo basi utafaidika, anza na kuuza kwanza baadaye ukipata channel nzuri utakodisha, nunua kutoka China maana laptops zimekuwa bei ndgo sana siku hizi.


Professional Software Training.

Sizingumzi kufundisha computer hapa, nazungumzia kufundisha hizi programu za kuendesha taasisi na makampuni mfano za wahasibu, mahospitali, mashule na kadhalika, kuna zile maarufu ukizifahamu zitakufanya uitwe na makampuni kwenda kuziweka, kuziuza na hata kufundisha wafanyakazi wao.


Njia

Jifunze mtandaoni au kama upo kweye sekta mabayo imekuvutia tengeneza mfumo mzuri na uuze kama kuna uhitaji eneo hilo.


Graphics Design

Sanaa ya matangazo ni muhimu siku hzi kwa ukuaji wa biashara, ila imekuwa nyepesi sana maana programu zimekuwa nyepesi kutumia ya kwamba watu wengi wanafanya wao wenyewe. Ila kuna matangazo yanahitaji skills zaidi kama ya Video so jikite huko, nenda mbali zaidi kwenye 3D na motion graphics.

Njia

Youtube ina mafunzo ya kila aina ya programu, tafute mafunzo muhimu ya programu mama kama Adobe Illustrator, Photoshop na Indesign, then hamia katika After effects, Maya, cinema4D na kuendelea kazi zipo nyingi mitandao ya UPwork.



 


Ukweli Wa Ndani Kuhusu Kazi Ya App Development: Fursa, Pesa Nyingi Na Changamoto Zake

📅 Imeboreshwa: 2026 ⏱️ Muda wa Kusoma: Dakika 5

Bila shaka App Development (Utengenezaji wa Programu za Simu na Kompyuta) ni mojawapo ya kazi zinazojichotea umaarufu mkubwa sana duniani na hapa Tanzania kwa sasa. Kila siku inayopita, jamii na makampuni yanahitaji mifumo mipya ya kidijitali ili kutatua changamoto za kila siku—kuanzia mfumo wa malipo, utoaji wa huduma, mpaka usafirishaji.

Kati ya kazi zinazopatikana kwa urahisi ukiwa mahali popote duniani (Remote Jobs na Freelancing) na zenye malipo ya juu zaidi, kazi ya App Development inashika nafasi za juu. Hata hivyo, kabla hujafanya maamuzi ya kuanza safari hii ukiwa chuo au mtaani, kuna mambo mazito ya ndani unayopaswa kuyajua mapema.

1. Kujitenga (Isolation) Na Kukesha Mbele Ya Kompyuta

Kazi ya kuandika code inahitaji utulivu wa hali ya juu na muda mwingi sana wa kukaa peke yako mbele ya kompyuta. Fani hii inamhitaji mtu ambaye si mtokaji sana—yaani mtu aliyetayari kukaa ndani kwa zaidi ya 70% ya siku na aliye tayari kuchelewa kulala (kukesha majogoo) ili kutatua bug au kumaliza project.

💡 Jinsi ya Kurekebisha: Tumia mbinu ya Pomodoro (fanya kazi min 25, pumzika min 5) badala ya kukaa masaa 6 mfululizo. Hii inasaidia ubongo usichoke haraka na kupunguza msongo wa mawazo.

2. Uwezo Wa Kufikiri Haraka Na Kutatua Matatizo (Problem Solving)

Lengo kuu la App yoyote ni kutatua tatizo la mtu au mfumo. Unapoingia kwenye fani hii, utahitaji kujenga uwezo wa uchanganuzi wa haraka (Logical Thinking). Hata kama huna uwezo huo hivi sasa, usiwe na shaka—unavyozidi kuandika programu na kutatua changamoto, ubongo wako utajifunza na kuwa sharp sana katika kufanya maamuzi ya haraka.

3. Changamoto Za Mahusiano Na Maisha Ya Kijamii

Kutokana na kutumia muda mwingi kufanya kazi usiku na mchana, uwezo wako wa kushiriki maisha ya kijamii unakuwa mdogo. Kama alivyowahi kusema Professor mmoja wa IT kwa wanafunzi wake: "Oa haraka, zaa haraka zaidi kabla mkeo hajakuacha" 😅.

Ma-developer wengi hupitia wakati mgumu kwenye mahusiano kwa sababu wanakuwa busy sana na kompyuta. Ni wanawake au wanaume wachache sana wanaoweza kuvumilia mwenzi anayekesha kila siku mbele ya screen.

✅ Jinsi ya Kurekebisha: Tengeneza ratiba rasmi ya kazi na heshimu muda wa familia/mwenzi wako. Weka mipaka wazi kati ya muda wa kazi na muda wa maisha ya binafsi.

4. Fursa Za Pesa Nyingi (Kipato Cha Dola)

Ukiwa App Developer mzuri na mwenye uzoefu, fursa za kifedha ni kubwa sana. Unaweza kuajiriwa na makampuni ya nje na kulipwa kwa Dola (USD) ukiwa hapa hapa Tanzania, au ukatengeneza App yako mwenyewe inayokuingizia kipato cha kila siku kupitia matangazo au usajili (subscriptions).

Si ajabu kwamba ma-developer ndio wanaotengeneza safu kubwa ya matajiri wa teknolojia duniani leo. Muhimu ni kujifunza vizuri na kuwekeza kwenye ujuzi unaotakiwa sokoni kabla ya umri kwenda.

5. Kipindi Cha Umri Wa Ku-Code (Miaka 13 Hadi 28)

Licha ya kuwa mtu anaweza ku-code maisha yake yote, kipindi chenye tija kubwa na nishati ya kuandika code usiku na mchana ni kuanzia miaka 13 hadi 28. Baada ya hapo, majukumu ya kifamilia na umri huongezeka.

💡 Ushauri Wa Mkakati: Unapofikisha miaka 30+, unapaswa uwe umejiendeleza na kusogea kwenye nafasi za uongozi kama Tech Lead, Software Architect, au Project Manager ambapo unatumia uzoefu wako kuongoza vijana badala ya kuandika kila mstari wa code wewe mwenyewe.

6. Matatizo Makubwa Ya Afya (Mgongo Na Uzito)

Hili ni tatizo kubwa sana linalowakabili ma-developer wengi. Kutokana na kukaa kwenye kiti kwa zaidi ya masaa 6 hadi 8 mfululizo bila kupumzika, wengi huishia kupata matatizo makubwa ya ututi wa mgongo (spine problems) na kupatwa na uzito uliopitiliza (obesity).

  • ✅ Fanya Mazoezi: Hakikisha unafanya mazoezi ya mwili angalau mara 4 kwa wiki ili kuweka viungo vyako vizuri.
  • ✅ Ergonomic Setup: Tumia kiti kinachoshikilia mgongo vizuri (Ergonomic Chair) na urekebishe kioo cha kompyuta kilingane na macho yako.

📌 Ushauri Wangu Kama Developer Na Trainer Kwa Vijana

Kama wewe ni kijana wa kike au wa kiume unayeingia kwenye App Development, hakikisha unapanga muda wako kwa umakini wa hali ya juu. Kwa mabinti zetu wa Kitanzania, fani hii inahitaji nidhamu ili usijikute umekaa ndani masaa 24 na kushindwa kushiriki maisha ya kijamii na kifamilia! 😆

App Development ni fani bora inayoweza kukutoa kimaisha, lakini lazima uwe na mizani sahihi (balance) kati ya kazi, afya yako, na maisha yako ya kibinafsi.