Imekuwa ni jambo la kawaida huku mavyuoni kutenganisha ajira na masomo,
haswa katika vyuo vyetu hapa Tanzania,
kiasi ambacho tumekuwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira,
ambalo ukilatazama kwa umakini kuna uwezo fulani wahitimu wanakosa ndio maana, tatizo linakuwa kubwa mno.
Lakini pia kuna sababu za msingi tuu ambazo ni za kiuchumi ambazo hata wahitimu hawahusiki ambazo zinakuza tatizo hili.
Kwa upande wa Information Technology na kozi zote zinazoendana na hiyo kozi,
kuna vitu vifuatavyo ambavyo mwanafunzi akivifanya vinaweza fungua njia au
kupanua wigo wako wa ajira kwa kiasi kikubwa sana.
GPA/ UFAULU CHUONI
Huu ni ufaulu wako chuoni, najua ninavyozungumza hivi kwa wingine ni kama kuwaambia wanywe maji ya sumu, ila ndugu zangu hakuna jinsi,
GPA ina faida kwanza GPA kubwa inachangia kwa kiasi kukuitisha katika interview ya kazi,
kwa maana inaonesha una uelewa mkubwa na inaonesha kwa kiasi unaweza chapa kazi,
kama ulisoma kwa bidii kwa kiasi hicho basi unaweza ukawa na bidii hata kazini.
Lakini pia mavyuoni tunahitaji wahadhiri na kigezo kikubwa ni GPA ndio utaitwa kwenye interview za huko na hata watu wanaoomba ni wachache sana.
GPA nzuri huanzia 3.5 na kuendelea ila vyuoni ajira zake inategemea huwa inaweza anzia 3.5 wakati mwingine 3.8.
PROFESSIONAL CERTIFICATIONS/ VYETI VYA UTAALAMU.
Hivi ni vyeti vya kitaalamu yaani kubobea katika sehemu fulani,
hivi havikupi degree au diploma, ila inapewa hadhi ya kuwa mtaalamu katika eneo moja tuu la IT mablo linaweza likawa sio kubwa.
Mfano
ukitaka kubobea kwenye networking lazima upitie CCNA Certifications, MCSA na kadhalika.
Katika kazi kama za System Administrator bila vyeti kama hivi kuapply ni kazi bure na hata kama ukiitwa mitihani inaweza kukushinda kwa ugumu wake.
SKILLS/UJUZI BINAFSI
Katika maswala ya IT, swali halipo sana unamefundishwa nini
ila lipo katika unaweza kufanya nini
na unajua nini?
Hakuna muda mzuri wa kujifunza lugha mbali mbali za computer
na kujua jinsi ya kuzitumia kama muda huo,
maana kuna kujiajiri kwingi sana huko na hata serikali na mashirika,
yanatafuta watu wa kutengeneza software mbali mbali.
Mfano wa lugha za kujifunza ni Android, Java, HTML, PHP,Javascript, CSS, Ruby, Python N.K.
Na pia uwezo binafsi wa kutengeneza programs peke yako, websites, blogs N.K
PUBLIC WORKING PROJECTS/Project ambazo umefanya na bado zinafanya kazi.
Tofauti ya elimu ya vyuo vyetu na vyuo vya njee,
ni kwamba mkazo uliokuwepo upo kwenye projects au practical,
ni mkubwa sana ukilinganisha na hapa ambao upo kwenye nadharia zaidi.
Kwa hiyo hakikisha projects unayofanya inatatua matatizo ya jamii.
Hiyo hata kwenye interview sehemu ya projects inaweza mvutia HR kukuita.
IMPORTANT INTERNSHIP EXPERIENCE/MAFUNZO YA VITENDO YENYE TIJA.
Unapofika muda wa kutafuta field usifanye mzaha, tafuta makampuni ya kiteknolojia, ili ijifunze jinsi yanavyofanya kazi na hata kupata kazi kwenye makampuni mengine itakuwa rahisi kwa maana mzigo wa kuku train utakuwa umepungua.
Hayo ni maeneo muhimu ambayo ukiyashughulikia vizuri hautapoteza muda mwingi kutafuta ajira, kama hali itakuwa shwari ya uchumi.
Kwa ushauri zaidi wasiliana nami,
Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa
elisanteshibanda@yahoo.com
Elimu ya IT hapa Tanzania ni changa sana na imejaa ujuzi mwingi na unahitajika sana katika Taifa hili,
ujuzi wa IT wa ngazi ya chini kabisa, unaweza ukampa mtu uwezo mkubwa tuu wa kujiajiri na
kuendeleza maisha yake.
Zifuatazo ni kozi ambazo zinaweza kumsaidia yeyote kuwa na uwezo wa kujiajiri.
Jinsi ya kufanya kazi na kulipwa mtandaoni ukiwa Tanzania
Course in Graphics Design.
Kozi hii itamuwezesha mwanafunzi kufanya yafuatayo;
- Kuchora chochote kwa njia ya kompyuta.
- Kubuni/design magazeti, vitabu,vipeperushi,kalenda n.k
- Kutengeneza matangazo makubwa na madogo kwa ajili ya kuprint au kuweka mtandaoni.
- Kubuni/design business cards, cover letter, cards za mialiko N.K
- Kurekebisha picha zilizopigwa na camera kiustadi zaidi na kuboresha muonekano wake.
Course in Web Design
Kozi hii inajikita katika kuunda tovuti za aina mbali mbali yaani za kibiashara na binafsi, na hii itampa mwanafunzi uwezo kufanya yafuatayo.
- Kuweza kuunda tovuti(website) na kuelewa inayoendana na tovuti.
- Kuipandisha tovuti kwenye mtandao.
- Kuunda tovuti za kisasa kwa njia tofauti.
- kutengeneza mablogu(tovuti ambazo watu wanaweza kuongea humo yaani kuchat mfano hii ni blogu) ya aina zote.
- kusajili tovuti ndani na njee ya nchi.
Course in Computer Administration
- Ujuzi huu utamsaidia mwanafunzi kupata uwezo wa kufanya yafuatayo;
- Kufahamu kompyuta na mifumo inayoendana nayo.
- Kufahamu Computer Hardware, yaani vifaa vyake na jinsi inavyofanya kazi, na hata kujua jinsi ya kuitengeneza pale inapoharibika.
- Kufahamu Computer software, yaani programu za kompyuta na aina zake, jinsi ya kuziweka, kuzitoa na hata kuzishughulikia na kuzitibu pale ambapo zinakuwa hazifanyi kazi vizuri.
- Kufahamu mfumo wa usalama wa kompyuta, jinsi ya kuilinda kompyuta yako na mshambulizi ya kimtandao ya virusi na watu wa njee wanaokuzunguka.
- Kufahamu mifumo ya mawasiliano(Networks) ya kompyuta, jinsi inavyofanya kazi na jinsi ya kuifunga njia ya kuilinda pia.
- Kufahamu jinsi ya kutumia windows 10 na programu nyingine za kuendesha kompyuta mfano windows 8 na Linux.
Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na magroup ya Whatsapp ya MAXPO Tanzania Maximize your potential
Course in Advanced Microsoft Office
Kozi hii inamsaidia mtu kuweza kufanya shughuli zote za kiofisi kwa njia ya kompyuta, kuanzia zile nyepesi mpaka zile ngumu kufanya kwenye kompyuta.
Kozi hutoa uwezo wa kufanya yafuatayo;
Kutumia programu za microsoft office zifuatazo
Microsoft Word
Microsoft Powerpoint
Microsoft Excel
Kwa kiwango cha juu kabisa katika
Kukusanya data
Kuchambua data
Kupresent/wasilisha data mbele za watu
Na pia kutengeneza njia za kuingiza data na kutumia microsoft office katika biashara yako yoyote ile
kwa ajili ya kumbu kumbu na hata kuonyesha muelekeo wa biashara, katika mapato na matumizi.
Kumalizia kozi zote hizi hupatikana kwenye vyuo vya kitaalamu yaani Professional colleges ambazo zimejikita tuu katika kozi hizi,
kuchagua chuo chenye uwezo mdgo utakupelekea kupoteza muda wako na kutoka katika kiwango kibaya.
Nakushauri chukua mafunzo ya MAXPO Tanzania, yanatolewa na Kampuni ya Rains Technologies Co LTD iliyopo Ilala, Bungoni Str/Chunya Str Dar es salaam.
na wanakupangia ratiba kulingana na ratiba yako na wana Professional Lecturers wenye uzoefu na pia ni wafanyabishara katika Tehama, kwa hiyo utapata, elimu na ushauri na kusaidiwa jinsi ya kuanza, ila pia kuna vyuo vingine vipo ila sina uhakika na hivyo ila pia ukumbuke jitihada zako binafsi zitakusaidia kupata ujuzi zaidi
Kwa ushauri zaidi wasiliana nami katika
Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na magroup ya Whatsapp ya MAXPO Tanzania Maximize your potential