Tehama(Information technology) Katika nchi za chini ya jangwa la Sahara, Afrika Mashariki bado ni changa sana. Na kama inavyofahamika teknolojia hurahisisha sana maisha na hupunguza mzigo mkubwa wa kazi kwa watu.

GUNIA ZITO.

Nimeifananisha na gunia zito kwa sababu kutengeneza teknolojia mbadala ili kuweza kutatua changamoto katika jamii inahitaji mafunzo, moyo wa kujitoa binafsi na jitihada zaidi.

Lakini pia inahitaji macho ya kuona hizo fursa katika jamii ili uweze kuzifanyia kazi. Watu wengi hukimbilia kazi ambazo hazihitaji sana ubunifu lakini huku ubunifu ndio mahali pake, pindi unapokosa akili za  ubunifu basi utashindwa kufanya lolote katika tehama.

LENYE PESA

Kama nilivyoeleza hapo mwanzo, pindi teknolojia hizi zinapotengenezwa na wataalamu, huingia sokoni na kurahisisha maisha ya wengi.
watu wengi, makampuni mengi na watu wengi yametajirika sana duniani kwa tehama, mfano 

kampuni kubwa zaidi ya Tax duniani haimiliki tax hata moja bali imeunganisha wamiliki wa Tax,
lakini tatizo waliloliona ni shida ya kupata Tax pale ambapo unaihitaji na haupo barabarani. 

UBER  kwa sasa inaingiza mabilioni ya Pesa duniani kote, hata hapa Tanzania zipo programu kama za mpesa, tigopesa zinaingiza pesa nyingi mno, 

zipo programu za vituo vya mafuta kama Petronite

zipo programu za maduka kama duka pro,

na programu za masomo kama thL na kadhalika na kadhalika...

JINSI YA KUWA MMOJAWAPO WA WABEBAJI.

1. Uwe na uwezo kujifunza kwa bidii sana, na kukuballi kutatua changamoto mbali mbali hata zisizolipa kwa muda huo.

2. Chukua masomo ya Tehama kuanzia ngazi mbali mbali kama cheti, diploma au degree.

3. Ikiwa huna vigezo, basi ujue kusoma na kuandika kiingereza vizuri na uwe na moyo wa kishujaa wa kusoma zaidi ya wale wanaosoma darasani ila ni lazima utafanikiwa.

Janga la ukosefu wa ajira haliwezi kuisha kama tutaendelea kusaka watu kutoka njee wafungue makampuni ndio tuajiriwe ila tuu kama sisi wenyewe tutakapoamua kutoka na kugeuza changamoto kuwa mtaji wetu.


Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   
au elisanteshibanda@yahoo.com
Tehama(Information Technology), imejaa fursa nyingi, na katika nchi zetu changa, fursa ni nyingi mno.

Katika Tehama juhudi za mtu binafsi na Mungu wake, ndio zitamfanya afinikiwe au asifanikiwe.

Mtaji wa Tehama ni computer tuu, ambayo ni gharama ndogo sana kuipata.

Ni vitu gani mtu anaweza soma/jifunza ili afanikiwe katika Tehama.

Graphics Design(Sanaa ya Matangazo)
Hii ni sanaa ya matangazo ya biashara. Hakuna biashara duniani isiyotaka matangazo

na ukiangalia dunia ya leo, tumezungukwa na matangazo, yanazidi kuwepo na jinsi biashara zinavyozidi kuongezeka kasi ya uhitaji wa matangazo inazidi kuongezeka.

Jinsi ya Kujifunza
@ Chukua kozi fupi ya wiki 6, na wewe utaweza kuwa vizuri kwenye sanaa hii. 
Vigezo: Kuanzia Form Four Leaver
Price: 300,000Tsh
Training: MAXPO training
Mahali: Rains Technologies, Ilala Bungoni, Chunya str.

@Tumia njia ya Video ya kujifunza, kwa kutumia mitandao kama Youtube.

Web Development
Huu ni utaalamu wa kutengeneza tovuti mfano wa tovuti ni kama cnn.com, bbc.co.uk n.k 
Kila biashara inavyokua na kutaka kupita mipaka ya kiwilaya, kimkoa au kitaifa inahitaji tovuti kwa ulazima. Maana tovuti ni ofisi pekee ya kampuni ambayo inaweza fikiwa na mteja ,
Akiwa kokote kule duniani.

Kwa kuangalia uchumi wetu unavyokua na ongezeko la makampuni soko la tovuti litaongezeka maradufu.
Jinsi ya kujifunza
@Chukua kozi fupi ya wiki 8, ujifunze kutengeneza tovuti.
Training: MAXPO Training
Bei: 400,000/-Tsh
Mahali: Rains Technologies, Ilala Bungoni, Chunya str.

@Chukua certificate in InformationTechnology/Diploma/Degree kwa mwaka 1, 2, 3 N.k
Mahali: University of Dar es salaam Computing Centre
Vigezo: Tembelea chuoni.

@Tumia mafunzo ya vitabu na video za kwenye mtandao ili kujifunza kutoka kwa watu mbali mbali.


Computer Application
Kozi hii inakuweza kuifahamu computer ndani na njee, kuendesha stationery, na hata kutumia computer ya windows 10 na Apple computer(MAC OS) kama mtaalam.


Lakini pia inakupa uwezo wa kujifunza microsoft office yote.
Pamoja computer networks.

Jinsi ya kujifunza
@Chukua kozi fupi  ya wiki 4 ya Computer application.
Vigezo: Yeyote
Training: MAXPO Training
Bei: 250,000/-Tsh
Mahali: Rains Technologies, Ilala Bungoni, Chunya str.


@Chukua certificate /diploma/ degree katika Information Technology, computer science, ICT.
Mahali: University of Dar es salaam Computing Centre
Vigezo: Fika Chuoni.

@Tumia mtandao wa youtube kujifunza na google kupata vitabu.

Mafunzo ya Tehama, yanaanza taratibu na ni marahisi kwa mtu mwenye jitihada ya kusoma na nidhamu ya kujifunza bila kukata tamaa.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nami.
Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   

au katika elisanteshibanda@yahoo.com
                  

Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa