Fahamu njia na vigezo vya kusoma IT Tanzania ya leo, 2023



IT(Information Technology) ni kozi nzuri sana kwa vijana na pia ni mojawapo ya sekta ambayo makampuni yaliyowekeza humo yanatengeneza pesa nyingi sana.

Na tunapokwenda IT Imekuwa ikifuta nafasi za kazi nyingi sana kwa kompyuta kuzifanya hizo kazi, mfano;

Assembly line & factory workers

Phone Operators and receptionists

Cashiers

Bank tellers and clerks

Pilots

Journalists and reporters

Stock traders

Postal workers

Travel agents

Accountants

Na kadhalika ni kazi nyingi zinapotea,hatuwezi maliza ila pia IT inatengeneza ajira zake nyingi sana, nyingine hazihitaji hata uajiriwe na mtu.

NJIA  YA SHULE KUPITIA ADVANCE HIGH SCHOOL

Kuanza kama ni mwanafunzi wa sekondari hakikisha unasoma masomo ya science na biashara na uendelee advance na masomo hayo hlafu ukifika chuo  chagua kozi za IT.


NJIA YA SHULE KUPITIA CHUO

Soma mpaka form four masomo ya science na biashara, halafu chukua certificate ya IT, halafu diploma halafu degree. Vyuo bora ni University of Dodoma, St.Joseph University in Tanzania, Dar es salaam Institute of Technology,College of Information and Communication Technologies (CoICT) - University of Dar es salaam na University of Dar es salaam Computing centre.


NJIA YA  KUTOKEA CHUO NA KUENDELEA.

Soma kozi yeyote halafu ukimaliza unaweza nenda kwenye vyuo vya IT, kama unaweza soma degree nyingine ya IT au nenda kwenye vyuo vinavyotoa ujuzi wa IT na ujifunze unaotaka.

Mfano Degree ya Uchumi ila unapenda IT. basi nenda kwenye chuo kinachotoa IT, tafuta Ujuzi unaoutaka mfano:

Application Development

Networking(Inategemea vigezo)

Cyber security(Inategemea vigezo)

Computer TIA

Web development

Graphics Design.

Accounting package Training.

Halafu tafuta college inayotoa ujuzi husika katika vyuo nilivyoviorodhosha hapo juu.

Mara nyingi kozi nyingine hapo huwa hazifundiswi mavyuoni mfano cyber security au App development kwa hizi kozi inabidi ufanye paid online training katika mitandao kama Udemy, Tutsplus etc.


NJIA YA BURE

Kama unapenda IT na hauna hela zaidi ya hela ya bundle, basi chagua kozi unayotaka kusoma, halafu nenda kwa wanao download movies mtandaoni waambia wakusaidie kukutafutia hizo online courses then wakuwekee kwenye hard drive ili ukajifunze wemyewe privately, na watu wengi wamejifunza kwa njia hii, ila hautapata cheti chochote zaidi ya ujuzi.




4 comments:

  1. Naomba kuuliza mfano Kwa aliye faulu form four Kwa masomo ya hisabati b, biology c,English c,Kiswahili c na geography d,je amekidhi vigezo?

    ReplyDelete
  2. Nataka nafasi kusoma it imawezkana na napenda sana kusomea it kam ndoto yangu

    ReplyDelete
  3. Nataka past papers za ict za veta

    ReplyDelete