MADHARA/MATOKEO YA KUFANYA CODING(APP DEVELOPMENT) UNAYOTAKIWA KUJUA MAPEMA, 2024

 


Bila shaka App Development(Utengenezaji wa programu za kwenye simu na kompyuta) ni mojawapo ya kazi inayojichotea umaarufu mkubwa sana duniani kwa sasa, tunahitaji wataalamu wengi sana katika upande huu wa teknolojia ukizingatia kila siku zinavyosogea tunazalisha mifumo mingi zaidi ya kutatua changamoto nyingi za kila siku.
Na katika kazi zinazopatikana kwa urahisi ukiwa kokote kule duniani na zenye malipo mazuri basi ni kazi ya App development.

Kutokana na ajira kuwa chache, vijana wengi wamekuwa wakitaka kujikita katika kutengeneza Apps na kubobea katika hii fani wengine wakiwa mavyouni na wengine mtaani, kwa yafuatayo naomba uzingatia kama unataka kuingia katika njia hii.

KUJITENGA

Kazi hii inahitaji kupoteza muda mwingi sana ukikaa mbele ya kompyuta kuandika programu, kwa hali hii inamuhitaji mtu ambaye sio mtokaji sana, yaani mtu anayependa kukaa ndani kwa zaidi ya asilimia 70 ya siku 😕 na ambaye atakuwa teyari kuchelewa kulala kila siku majogoo yaani.

KUWEZA KUFIKIRI HARAKA

Kutokana na kazi imekaa kutatuta changamoto fulani utahitaji kuwa na uwezo wa kufikiri na kutatua matatizo haraka, hataka kama hauna kwa sasa, usijali..unapoendelea ubongo wako utajifunza na kuwa sharp sana katika kutatua changamoto mbali mbali, hii ni nzuri sana.

KUVUNJA MAHUSIANO

Kutokana na kupoteza muda mwingi kufanya shughuli hii especially usiku, "Professor mmoja wa IT aliwaambia wanafunzi wake Oa haraka, zaa haraka zaidi kabla mkeo hajakuacha" 😅 Hawa watu huishia kupata tabu kwenye mahusiano kwa sababu wanakuwa busy sana especially mwanamke gani atapendelea tabia yako ya kukesha...

PESA NYINGI

Yes, sijakosea ukiwa developer mzuri utalipwa katika Dollars, na ukiwa na mawazo endelevu utatengeneza Apps ambazo zitakuingizia pesa kila dakika. so katika yote pes utapata maani si unajua hadi leo ma developer ndio matajiri zaidi duniani kuliko hata ma engineers na kadhalika, uwe unajifunza na kuwekeza mapema kabla umri haujakutupa.

MUDA

Kuna watu wanakuwa na vichwa vizuri na kuendelea na coding maisha yao yote, ila umri wa kufanya coding huwa from 13th mpka miaka 28 hivi, baada ya hapo unahitaji kuwa umeshajiendeleza vya kutosha na kuanza either kuajili watu vijana wafanye na uwalipe au ufanye shughuli nyingine maana utaanza kuwa na majukumu mengi.

MATATIZO YA KIAFYA

Ndgu yangu nini marafiki mpka wamefanyiwa operation za mgongo, ni tatizo moja kubwa sana kwa kukaa kwenye kiti kwa muda mrefu, na kibaya unakuwa hata hujua ya kwamba muda unasogea unashtuka tuu teyari yamepita masaa 6 umekaa tuu, pia uzito ulipitiliza kwa kutofanya mizunguko ya kutosha ni muhimu sana kufanya mazoezi kwa ulazima kuanzia mara 4 kwa wiki.


Kwa haya machache kama Developer pia na Trainer ningependa kuwashauri vijana, kama ni wa kike kuwa makini na muda maana wao ndio wana muda wa kuolewa kwa hiyo usijikute umekaa ndani mpka unashindwa kuonekana na Hamisi wa kutokea Uluguru huko akuoe...😆




0 comments:

Post a Comment