Vyuo Bora vya kujifunza IT(Information Technology) Tanzania.


Katika Upande wa Elimu ya juu, ni vizuri kupata ushauri bora kabla hujaenda kujiunga na chuo chochote.
Kwa maana uamuzi wako huo utaamua mambo yafuatayo katika maisha yako...

KIPATO CHAKO BINAFSI
Kozi hii ya IT, Kichwa chako ni ofisi yako, kwa hiyo kama utapata elimu mbovu,utapoteza uwezo wako wa kujiajiri na unaweza ishia pabaya.

AJIRA
Interviews za kazi hizi za IT, sio nyepesi, na kwa hali hii itakushinda kushindana na watu waliofundishwa vyema na kuwa wazuri katika maeneo muhimu ya Information Technology.

MCHANGO WAKO KWA TAIFA
Kozi hii au profession hiii au kazi hii ya IT ina mzigo mkubwa katika taifa hili changa kiteknolojia.
Kuna matatizo katika jamii ambayo yanahitaji kutatuliwa kidigitali,kwa sababu hii kama utakuwa na elimu mbovu,

utakuwa mmoja wa walalamikaji badala ya wabunifu na watatuaji matatizo.VIGEZO VYA CHUO BORA KATIKA IT
Vifuatavyo ni mojawapo ya vigezo muhimu,ila vinaweza vikawepo vingine zaidi.

UBUNIFU UNAOFANYA KAZI
katika mavyuo mengi sikatai kama kuna ubunifu ila mwingi unaishia kwenye makaratasi ya chuo na kutupwa stoo(store). 
Ubunifu hujulikana kwa project ambazo zinavuka mipaka ya chuo na kuifikia jamii.

UFUATILIAJI WA CHUO KWA PROJECT ZA WANAFUNZI.
Kuna mavyuo yanaongoza kwa kutupa store project za wanafunzi lakini pia kutokuchukulia kwa umakini project zinazofanywa na wanafunzi, kiasi kwamba wanafunzi wako huru kuforge project zao na chuo kuzipokea tuu kwa kutokujali ya kwamba hii project imefanyika au laa. 

ASILIMIA YA VITENDO KATIKA ELIMU INAYOTOLEWA.
Ni muhimu kwa chuo kuwa na asilimia kubwa sana ya vitendo kuliko nadharia

VIFAA VYA KUJIFUNZIA IT
Ni muhimu kusoma  kwenye chuo chenye vifaa vya kutosha ili ujue haswa nini kinaendelea makazini ila ni kwa  asilimia ndogo hii pointi ina umuhimu maana IT inakuwa kwa kasi na Vyuo vya haviwezi kuwa na vifaa vya kisasa kila wakati.


"Chuo kinaweza kumtengeneza mhitimu wa IT,ila ni jukumu la mwanafunzi binafsi akiwa chuoni, kutoka chuoni kama mtaalamu,na sio mhitimu pekee kwa maana wahitimu hupata shida sana kutafuta ajira wakati wataalamu hutafutwa na ajira na pia hujiajiri."
Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   


VIFUATAVYO NI VYUO BORA KUJIFUNZA IT  TANZANIA.
 1. Dar es salaam Institute of Technology (DIT)

2. St.Joseph University in Tanzania.

3.University of Dar es Salaam.

4. University of DodomaKwa kumalizia, vyuo vipo vingi na wanafunzi wanazidiana uwezo 
kwa hiyo inawezekana ubunifu wa hali ya juu ukatokea kwenye chuo ambacho hakipo hata kwenye list hii, 
na pia vyuo vingine vinaweza vikaboresha ufundishaji wake na kuvipiku vyuo vilivyopo sasa.

Na la muhimu college za IT zipo nyingi na kwenye mikoa mingi, kwa hiyo kukosa nafasi kwenye vyuo hapo juu haimaanishi IT yako umeitupa, ila ina maana wewe ndio wa kukin'garisha chuo ulichokuwepo.
Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   

Kwa ushauri zaidi wasiliana nami katika Elisanteshibanda@yahoo.com

20 comments:

 1. Perfect bro
  for
  perfect
  article

  ReplyDelete
 2. Thanks,, nimependa advices,na
  blog yko keep it up

  ReplyDelete
 3. Kaka samahani Nina mdogo wangu nataka kujua chuo kizur kwa masomo ya it na yeye yupo mbeya aiport ya zamani ameitimu 4 mwaka jana na ameoata Chet Ila nataka sifa zinazo takiwa huko chuon na ghalama zao kulingana na ushauri wako na Kama kipo mbeya nambie kuepkana na ghalama za hapa na pale no 0713472938 or 0742151450 naitwa Jackson

  ReplyDelete
 4. Napenda kuuliza je ni kozi ipi nzuri ya IT itakayo maliza kusoma alafu utume maombi kwenda jkt baada ya hapo jwtz Kama mtu uliesoma IT?

  ReplyDelete
  Replies
  1. Nilikuwa nauliza kuwa ni ajira gani ambazo hupatikana baada ya course hii kwa wahitimu wake

   Delete
 5. Elimu Yako unayoitoa ni nzuri, tafadhari endelea kufanya hivyo!

  ReplyDelete
 6. Sorry Kwa Mimi ambae napenda kusomea IT na IPO kwenye damu unanishauri vp

  ReplyDelete
 7. Mimi nahitaji kusoma IT hasa chuo gani kizuri kwa dar es salaam na sifa za kupokelewa kwenye hicho chuo naomba jibu no.0623518982

  ReplyDelete
 8. Inamaana kilimanjaro Institute kimezidiwa na vyuo ivyoulivyovitaja?? Maana yake mtaani huku naskiaga sana wakikitaja hiko chuo lakini sijakiona kwenye orodha..Samahani kakayangu naomba unijibu kwa sababu mimi meenyewe sijui pia kwahiyo naomba ushauri wako.

  ReplyDelete
 9. Kaka mm Nina D2 na Ç1 et naeza soma IT nko shnyanga ila nataka chuo kilichopo mwanza he unanshauli nkasomee chuo gan na hizo pass zinaeza nluhusu kusoma hyo koz

  ReplyDelete
 10. Mi nauliza ni vigezo gani anavotakiwa kua navyo mtu aliehitimu form4 kujiunga na masomo ya IT

  ReplyDelete
 11. Chuo bora cha it cha serkali being kdogo n nzur n kp

  ReplyDelete
 12. Ningependa kufahamishwa sifa za kujiunga na vyuo hivyo

  ReplyDelete
 13. Ushauri nzuri. Samahani naomba uliza nimesoma chuo cha mipango adi diploma je naweza transfer adi chuo chenu?

  ReplyDelete