Soma mwongozo wa field training kwa wanafunzi wa IT na Computer Science Tanzania. Fahamu makampuni bora ya Software, Networking, Graphics na Plan B ukikosa field.
Field Training (Mafunzo ya Vitendo) ni sehemu muhimu sana katika safari ya masomo ya Degree au Diploma ya kozi za IT, Computer Science, Computer Engineering, na Software Engineering. Field haipo tu kwa ajili ya kujaza logbook ya chuo, bali ina mchango mkubwa sana katika maisha yako ya baadaye ya kitaaluma.
Umuhimu mkubwa wa kufanya field kwenye kampuni au taasisi sahihi nchini Tanzania unajumuisha:
- Kukusaidia kugundua sehemu sahihi ya kubobea (specialization) kwenye sekta ya IT.
- Kujenga uzoefu wa kwanza wa kuweka kwenye CV yako. Kuna tofauti kubwa kati ya kusema umefanya field Vodacom au Selcom na kusema umefanya Serikali ya Mtaa.
- Kufahamu ni ujuzi (skills) gani wenye soko na unaolipwa vizuri kwa sasa katika soko la ajira la Tanzania.
- Kupata Connections na IT Professionals na waajiri wanaoweza kukupa ajira au mchongo pindi utakapomaliza chuo.
1. Mtandao na Miundombinu (Networking & Infrastructure)
Kama unavutiwa na mambo ya Routers, Switches, Data Centers, Fiber Optics, na Network Security, unapaswa kutafuta nafasi kwenye makampuni ya Simu au Internet Service Providers (ISPs).
- Makampuni ya Simu: Vodacom, Tigo (Axiata), Airtel, na Halotel.
- ISPs & Network Providers: Raha Liquid Telecom, SimbaNET, Azam Telecom, na Seacom.
- Mashirika ya Umma: TTCL Corporation na eGA (Mamlaka ya Serikali Mtandao) — hizi ni sehemu rahisi na bora zaidi kupata uzoefu wa mtandao wa taifa.
2. Software & Web Development (Coding)
Kama unalenga kuwa Programmer au Software Engineer, unahitaji kwenda kwenye makampuni yanayojihusisha moja kwa moja na kutengeneza mifumo, Mobile Apps, FinTech, na Websites.
- FinTech & Tech Companies: Selcom Tanzania, ShuleSoft, Smart Codes, Nyumbani Creative, Ramani.io.
- Tech Innovation Hubs: Buni Hub, Sahara Ventures, Kinu Hub.
⚠️ Anagalia Hili (Note): Makampuni haya mara nyingi huwa na timu ndogo ya waandika code na hawana muda mwingi wa kufundisha msingi. Ukipata nafasi, hakikisha una nidhamu, unajituma, na unauliza maswali ya msingi ukiwa tayari una ujuzi wa awali wa programming.
3. Graphics Design, UI/UX na Digital Media
Kwa wale wanaopenda Graphics Design, Video Editing, au User Interface Design, unapaswa kutafuta nafasi kwenye vyombo vya habari au Digital Agencies zenye studio za kisasa za uzalishaji.
- Vyombo vya Habari: TBC, Millard Ayo/Ayo TV, Azam Media, ITV/Radio One, Clouds Media Group.
- Digital & Creative Agencies: Genesis Tanzania, Ogilvy Africa (Tanzania), Dentsu.
4. Computer Configuration & Hardware Maintenance
Hii inahusisha matengenezo ya kompyuta, installation ya mifumo, na troubleshooting.
🚀 PLAN B: Unapokosa Field Sehemu Kubwa (Mbinu Ya Kijanja)
Umetafuta field Vodacom, Selcom, au eGA umekosa kabisa, muda unakwenda na chuo kimeanza kukupa pressure? Usipanic.
Nenda kutafta field kwenye taasisi au ofisi yoyote (hata kama haina kitengo cha IT au ina IT wa mtu mmoja tu), mfano: Halmashauri za Wilaya, Ofisi za Mkurugenzi, au Ofisi za Serikali za Mikoa. Ofisi hizi nyingi kwa sasa zina mtandao mzuri wa intaneti (LAN/Fiber) na zina mazingira tulivu.
Hakikisha ofisi hiyo inakujazia fomu zako za chuo vizuri. Baada ya hapo, tumia muda wako na intaneti yao bure kusoma Online Courses (Udemy, Coursera, YouTube, YouTube FreeCodeCamp) kwenye Programming, Data Science, au Cloud Computing.
Ukitumia miezi miwili au mitatu ya field hivi, utatoka na ujuzi mkubwa sana wa kukuwezesha kufanya kazi za Freelance (Upwork, Fiverr) au kuanzisha Startup yako kuliko hata mtu aliyekuwa anafanya field kwenye kampuni kubwa akiwa anatumwa tu kuprint mafile!
❌ Sehemu Zisizofaa Sana Kwenda Field Ya IT
Ili usipoteze muda wako wa miezi miwili au mitatu, epuka sana kuomba au kukubali kufanya field katika sehemu zifuatazo:
- 1. Benki za Biashara (Commercial Banks): Kutokana na ulinzi mkali wa taarifa na fedha (Cybersecurity & Compliance), benki hazitakuruhusu kabisa kugusa au kuona mifumo yao. Utabakia kukaa Mapokezi (Front Desk) au kusaidia wateja kujaza fomu—jambo ambalo halitaongeza ujuzi wowote wa IT.
- 2. Shule za Sekondari au Primary: Mara nyingi utaishia kutengeneza kompyuta moja ya Mwalimu Mkuu au kusimamia Computer Lab yenye kompyuta za zamani zisizo na mfumo mzuri wa mtandao.
- 3. Serikali za Mtaa na Ofisi Ndogo Zisizotumia Tech: Kama sehemu haina mtandao wa intaneti wa maana, haina LAN, na haina mifumo ya kidijitali, USIENDE. Hautajifunza kitu na wala hutapata fursa ya kutumia Plan B.