Kama kijana mdogo nisiyekuwa na uzoefu  hata kidogo  wala msaada katika biashara, nilijikuta nikiona jinsi gani duka la Mangi lilikuwa likikua kwa kasi, na la kwangu taratibu mno, nilijiuliza maswali mengi lakini kwa sababu Mangi alikuwa mfanyabiashara mwenzangu na rafiki yangu sikusita kumuomba ushauri, na ndipo aliponiambia mambo haya amabyo yalibadilisha biashara yangu na mtazamo wangu katika uwanda huu wa biashara.

MTAJI.
Unapoanzisha biashara na unapokuwa na mtaji wako wa kiasi fulani , unapokuwa ukipata faida . inakupasa ufanye kila liwezekanalo kutogusa FAIDA, sijakosea sio MTAJI pekee bali FAIDA na MTAJI kwa mwaka mzima, hapo ndipo utaona ukuaji wa duka unaostahili..utapata wapi hela ya kula na matumizi mengine we mtu mzima umiza kichwa.

UENDESHAJI
Imezoeleka kuwaweka ndugu na jamaa au hata watu tuu tunaowaajiri kama wauzaji halafu sio tukaendelea na kufanya kazi nyingine.HAYO NI MAKOSA TENA NI MWIKO KUFANYA HIVYO.
Wafanyakazi waajiriwa wengi wameanzisha maduka yamekufa kwa sababu hiyo.
Wanaopaswa kuendesha duka lako ni "WEWE", "MKEO" na "WEWE+MKEO" kama watu hao hawatakuwepo, tafuta shughuli nyingine ya kufanya na hela yako.

MUNGU
Unaweza ukafanya vizuri kote katika hayo niliyoyasema hapo juu, lakini ukweli ni kwamba biashara zimetawaliwa na nguvu za giza sana, ni lazima uchague utakaa upande gani na ukae huko moto  moto na sio robo au nusu, kama ni uchawi ujue ipo siku utakufa na biashara yako itakufa vibaya na utaangamiza watoto na familia yako so nakushauri mtafute Mungu wako.

NIDHAMU
Watu wengi huchukia mabosi, wakiwaona kama wanawanyanyasa wanavyowashurutisha kufanya kazi, yaani wakitunza nidhamu kazini, lakini ukweli ni kwamba biashara inahitaji nidhamu ya hali ya juu mno, isiyosuburi kukumbushwa...mazoea, uchelewaji, kauli chafu,uvivu huua biashara mara moja.

UTU
lazima uwe na utu, ujali wafanyakazi wako, kimahitaji na hata kimahusiano yaani waheshimu, hata kama umewazidi kipato kiasi gani.
"Kumbuka wamiliki wengi wa biashara wameuawa na majambazi kwa mpango uliosukwa na wafanyakazi wao au hata kuporwa mali kutokana na kisasi walichonacho wafanyakazi"

FULLITIME/PARTTIME
Biashara sio part time nik full time job kama hauko teyari kuwekeza muda wako wote nenda kanunue hisa wekeza huko maana huko hauhitajiki sana kama una hisa ndogo na hisa zikizidi bado ushauri wangu utaendelea utakabidhiwa ofisi tuu.

Kwa hayo nimeona nikushirikishe wewe ili kama umejipanga kufanya biashara basi uwe makini usije ukapoteza hela zako bure.
Mangi yeye ni mfanyabishara mkubwa wa maduka ya jumla ya vyakula kwa aina nyingine ya biashara tanua fikra zako.

Tehama inaleta mabadiliko makubwa sana katika ulimwengu wetu tena kwa kasi kubwa mno, kasi hii ina pande mbili  yaani nzuri na upande mwingine ni hatari. Katika uzuri wake ni kweli mtumiaji wa mwisho hupata urahishwaji zaidi wa kazi na ubora zaidi ila kasi hii kwa upande wa biashara na wataalamu waliopo ndani inaweza kukuza na hata kuua biashara kwa kuchelewa kidogo.

Yafuatayo ni mambo 5 muhimu kujua kama unataka kuingia katika ulimwengu huu wa tehama kwa njia ya kusoma au kufanya biashara.


  1. Kubali mabadiliko haraka na zaidi jifunze kuendana nayo kwa uharaka huo huo kama yalivyoingia, kwa sababu unavyoyagomea au kuchelewa kubadilika ni kama kuivisha biashara yako kitanzi.
  2. Mfano :
    kampuni ya zamani ya kutengeneza programu za kusafu(browse) mtandao yaani browser inayoitwa Netscape ilikuwa inauza programu zake na kufaidika sana lakini ghafla kampuni ya Microsoft iliamua kutengeneza na kugawa bure browsers hali iliyopelekea kampuni ya Netscape kwenda mahakamani kuizuia kampuni ya Microsoft ila haikufanikiwa ilikufa baadaye kwa kukataa mabadiliko.
     2. Uwe mtu wa kupenda kujifunza sana kupitia mtandao wa internet na mara kwa mara kuangalia            teknolojia mpya ili usije ukashtuliwa na kuingia kwa teknolojia mpya.
    
    3. Weka maono makubwa na ya mbali yanayoendana na eneo husika na ukuaji wake wa teknolojia          na pia ukilinganisha na ukuaji wa teknolojia hiyo duniani.
       Mfano: unapofungua Internet cafe sehemu nyingine hazihitaji kabisa hiyo huduma kwa sababu             ya jamii husika ina kipato kikubwa na sehemu nyingine inahitaji huduma za printing tuu na              copy, na sehemu nyingine inahitaji zote yaani internet,printing na copy(ila hiyo sio investment               pekee).
        
     4.Kwa Wanafunzi
   Wanafunzi wa ulimwengu huu wa tehama wana kazi mbili ya kwanza ni upokea kinachotoka               chuoni na ya pili ni kuupdate kile kinachotoka chuoni kwa sababu teknolojia hukua kwa kasi na        hata ikibadilishwa mitaara kwa kasi kiasi gani vyuo havitaweza kuendana na kasi hiyo na hata           kuwafanya wanafunzi kupoteza kufahamu misingi ya teknolojia kwa uzuri zaidi.

    5.Kutokana na kubadilika badilika kwa sekta hii inakupasa kuweza kujua kiwango cha mabadiliko ndani ya sekta hii . Mfano biashara ya kuuza simu ina kiwango kikubwa sana cha mabadiliko(simu hupitwa na wakati kwa haraka zaidi ya laptop) ukilinganisha na biashara ya kuuza kompyuta pakato(Laptop) ila zote zinabadilika.

    6.Onana na wafanyabiashara husika na pia IT Professionals au IT Consultants maana wao hujua soko lipoje na faida ipoje katika maeneo mengi ya ICT na kitu cha kuwekeza kwa sasa na kwa njia gani utaanza kuwekeza.

  Kwa ushauri zaidi wasiliana nasi!