Skills bora za IT, kuweka kwenye CV, 2025



Kama unasoma IT, tambua CV yako haitakiwi kuishia na diploma/degree pekee  inatakiwa kuwe na certifications au skills ili uweze kuwa na tija kwa waajiri.
Certifications zinahitaji pesa, skills hazihitaji pesa ila zinahitaji jitihada binafsi na kujifunza.

App Development.

Siku hizi kuna soko kubwa sana la application za android na iOS maana watu wanatumia sana smart phones ambazo zinafanya vizuri zaidi katika hizo application/programu. Na kwa sasa gharama za kutengeneza App moja ya Android inafika millioni 5, ukisoma mtandaoni kwa njia ya video unaweza tengeneza ila sio vyepesi ni ngumu sana.
Kazi ambazo utapita kirahisi ukiwa na ujuzi huu ni Software Engineer, System Analyst, Business Analyst etc.

Networking

Huu ni ujuzi wa kufunga networks za computer, ujuzi huu huwa na certifications za Cisco ila kuufahamu kutakusaidia kupita kwenye interview nyingi za Kazi za IT.

Cyber security

Kama Networking na hii ni certification, ila unaweza soma online kwa bei nafuu na kuwa na hichi cheti utakua lulu katika kazi za makampuni ya mawasiliano, TCRA, na mabenki huwachukua mara moja watu hawa.

Comp TIA

Huu ni ujuzi wa computer in general maintenance na zaidi, harwdare na software ukiwa nao huuu kazi za ICT Officer utakuwa una nafasi kubwa sana za kuzipata..unaweza ukasoma yote bure mtandaoni ukafahamu ujuzi au ukasoma na kulipia certfication yake ukawa nayo.


Web Development

Huu ni ujuzi wa kutengeneza tovuti/website, kampuni nyingu huingia gharama za kuwaajiri watu kutengeneza website na kuzi maintain na nyignine bado hazina, ukiwa na huu ujuzi unaweza hata uka suggest katika application letter ya kwamba unaweza ukatengeneza na website ya kampuni pia.


Graphics Design

Hakuna kampuni isiyojitangaza na makampuni hulipia gharama kubwa sana kudesign haya matangazo, so ukiwa na ujuzi huu, utaokoa pesa kwenye kampuni inayotaka kukuajiri na hyo ukijtetea hata kwenye application letter wanaweza wakaona una umuhimu zaidi kuliko watu wengine kwenye interview.

Na skills nyingine kama za MS office, database na kadhalika...zote hizi kama upo chuo basi hakikisha unazizoa kwa hali na mali maana chuoni una muda huko njee hakuna muda wa kujifunza kuna muda wa kufanya tuu.




1 comment:

  1. Casino at Harrah's Lake Tahoe - Mapyro
    Property Location 오산 출장마사지 A stay at 삼척 출장안마 Casino at Harrah's 춘천 출장샵 Lake Tahoe places you in a 전주 출장샵 convenient location, within a 5-minute drive of Heavenly Ski National Park and Heavenly 삼척 출장샵

    ReplyDelete