Tovuti(website) ni kurasa za kielectroniki(webpages) zinazohifadhiwa katika kompyuta server ili ziweze kupatikana kwa urahisi pindi zinapohitajika na watumiaji wengine waliopo kokote kule duniani kwa njia ya mtandao wa intaneti.
Mfano wa kurasa maarufu zaidi ni google.com na facebook.com.

Mambo yanayohitajika kuwepo kwenye tovuti.
  • ·         Utangulizi  mfupi wa biashara yako.
  • ·         Bidhaa zinazopatikana na njia ya kuzipata.
  • ·         Ubora wa bidhaa zako.
  • ·         Upekee wako kwenye soko.
  • ·         Mawasiliano ya kufika kwenye biashara yako.
  • ·         Maono ya biashara yako.

Mambo muhimu ya kuzingatia katika tovuti yako.
  1. · Usiweke taarifa nyeti za biashara yako kwenye tovuti maana kila mtu ataona hata adui wataona na watazitumia kukushinda kwenye biashara.

  1. · Usiweke taarifa nyingi kwenye tovuti, Maelezo mengi hayastahili kuwepo kwenye tovuti maana hakuna atakayesoma Maelezo hayo Zaidi yako, weka Maelezo mafupi na yenye kutosheleza.

  1. · Usiweke picha halisi ya eneo lako la biashara kama halina mvuto au ubora mkubwa.

  1. · Usitumie picha ambazo hazina uhalisia kabisa katika biashara yako au eneo ulipo, mfano kuweka wazungu wakati Wateja wako wengi ni weusi.

  1. · Weka taarifa fupi zile tuu zinazomchochea mtu kutaka kujua zaidi ili apige simu na kufika ofisini.

  1. · Fahamu Wateja wako ni watu wa aina gani ili uweze kuongea nao vizuri mfano kama ni Watu wa daraja la kati na chini kwa kipato na ni watanzania Zaidi hapo tumia lugha ya Kiswahili lakini kama watu wako ni watu wenye pesa na wamataifa mengine mengi tumia kiingereza.

  1. · Tumia wataalamu wazuri wa lugha ili kusiwe na makosa ya sarufi katika tovuti maana hufanya biashara yako  ionekana ya uchwara. 
Fuata hayo na mengine mengi kwa ushauri ntumie barua pepe na mimi nitakusaidia.

  



Karibu upate tovuti  na blogu safi kabisa, za kisasa na kwa bei nafuu sana. Kwa mawasiliano zaidi...

Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   
Sanaa ya Matangazo ni mojawapo ya vitu vinachangia mvuto mkubwa wa bidhaa inayotangazwa, Nini cha kufanya unapohitaji tangazo bora.

Kwanza kabisa onyesha uhalisia kwa kiasi juu ya biashara yako, unapotengeneza tangazo ambalo ni perfect sana, yaani halina uhalisia wa uwezo wako kiasi au uhalisia wa Nchi husika, husababisha watu wakuone wewe ni feki. lakini zaidi la muhimu zingatia ushauri wa mafundi wa sanaa hii.
Mfano mzuri angalia matangazo ya mitandao ya simu, huvutia wengi.

Kwa ushauri na utengenezaji wa matangazo haya karibu uongee nasi.
Tovuti ama kwa jina la kiingereza(website) imekuwa ni kama mavazi ya biashara katika mtandao wa Internet.

Nimeona Clients wengi wakibadili mawazo kwa kutembelea tovuti ya biashara ya wahusika mara moja, pale wanapokuta tovuti haina ufanisi wa hali ya juu au inachelewa kufunguka au ina muonekano mbaya.
 Siku zote hakikisha tovuti yako ina uwezo mkubwa, inapendeza na kuvutia watu haswa pale inapofunguka kwenye simu za mkononi na imekuwa hosted katika server bora na zenye ufanisi wa hali ya juu kabisa.

ECL Computer Clinic huwa tunachukua hatua za ziada kutafuta server bora duniani na kuhost tovuti za wateja wetu huku tukihakikisha zinapata usajili wa Tanzania na zinakubalika na watu wote na rika lote mfano Apollo Heavy Equipment Limited , Bright Future Academy  and so on.... karibu ufanye kazi nasi.

Ni vyema kupata ushauri wa kitaalamu kabla ya kufanya mabadiliko yeyote yale yanahusiana na teknolojia...

Ni kwa sababu zifuatazo
Usalama
Katika ulimwengu wa leo, kuna wizi mwingi sana katika mitandao haswa katika teknolojia inayohusiana na kompyuta, na hata tuna taarifa ya kwamza hapa Tanzania tupo katika nchi chache duniani ambapo wizi mwingi hutokea.

Mabadiliko ya Teknolojia
Teknolojia hubadilika mara kwa mara, unayotaka kutumia au kununua leo inaweza ikawa ishatoka katika usasa na ni ya zamani na inatakiwa kubadilishwa kutokana na sababu za kiusalama. Kwa hiyo ukajikuta umepoteza pesa zako nyingi.

Sheria na Matakwa ya Nchi Husika
Sio kila teknolojia unaweza kuitumia Tanzania au nchi nyingine na hata kuna njia ya kutengeneza system yeyote ili ikidhi viwango vya nchi husika mfano katika maswala ya usajili wa tovuti kwa Tanzania kuna sheria mahususi ambazo ni za kipekee kabisa hazipo duniani kote.

Kupata Wataalamu Husika
Sio kila aliye kwenye fani hii ni bora na anafaa kutumiwa, wengine wana uwezo tofauti na utawapata kulingana na mfuko wako.



Mangi Alinifundisha Siri 6 za Biashara

Mambo niliyojifunza baada ya kuona duka lake likikua, wakati langu likibaki nyuma.

Nilikuwa kijana mdogo, sina uzoefu mkubwa wala mtu wa kuniongoza kwenye biashara. Nilikuwa nikiangalia duka la Mangi likikua kwa kasi, wakati langu lilikuwa linakwenda taratibu sana.

Nilijiuliza maswali mengi. Alikuwa anafanya nini ambacho mimi sifanyi?

Kwa bahati nzuri Mangi alikuwa mfanyabiashara mwenzangu na pia rafiki yangu. Sikusita kumuomba ushauri.

Nilichokuja kuambiwa siku hiyo kilibadilisha biashara yangu na namna nilivyokuwa nikiutazama ulimwengu wa biashara.

💰 1. MTAJI: Usile Biashara Yako

Unapoanzisha biashara na una mtaji fulani, halafu ukaanza kupata faida, kosa kubwa ni kuanza kuitumia faida hiyo kama mshahara wako.

Kama lengo lako ni kukuza biashara, kwa kipindi cha mwanzo lazima uwe tayari kuacha mtaji na faida nyingi zibaki ndani ya biashara.

Mtaji unanunua bidhaa zaidi, bidhaa zaidi zinaleta mauzo zaidi, mauzo yanaongeza faida, na faida inaongeza uwezo wa biashara kukua.

Usitumie biashara ndogo kama ATM yako. Ukiitoa kila hela inayozalishwa, usishangae biashara ibaki palepale.

Swali kubwa ni: “Utakula nini?” Hapo ndipo unatakiwa kupanga maisha yako vizuri. Biashara haiwezi kukua kama kila wiki unaitoa hela yote.

🏪 2. UENDESHAJI: Biashara Inahitaji Mwenyewe

Kuna tabia tuliyoizoea: tunafungua duka, tunamweka ndugu au mfanyakazi, halafu sisi tunaendelea na shughuli nyingine.

Kwa biashara ndogo, hii inaweza kuwa hatari sana. Mmiliki anapaswa kujua kinachoendelea ndani ya biashara yake.

Kwa mtazamo wangu, kama wewe mwenyewe au mwenza wako hamuwezi kuisimamia biashara kwa karibu, fikiria kwanza kama aina hiyo ya biashara inakufaa.

Kadiri biashara inavyokua ndipo unaweza kujenga systems, managers na controls zinazokuwezesha kuondoka bila biashara kufa.

🙏 3. MUNGU: Usipuuze Imani Yako

Kuna mambo kwenye biashara ambayo siwezi kuyaeleza kwa numbers pekee. Mimi naamini biashara na maisha kwa ujumla vinahitaji pia msingi wa kiroho.

Unaweza kupanga vizuri, kuwa na mtaji na kufanya kazi kwa bidii, lakini bado ukahitaji kumtegemea Mungu kulingana na imani yako.

Fanya sehemu yako kwa bidii, lakini usisahau kumtafuta Mungu.

⏱️ 4. NIDHAMU: Biashara Haipendi Mazoea Mabaya

Watu wengi hawapendi mabosi wanaosisitiza muda na nidhamu. Lakini ukweli ni kwamba biashara bila nidhamu inaweza kufa polepole bila mwenyewe kugundua.

Kuchelewa, uvivu, kauli zisizofaa, uzembe, kutokujali wateja na kutokamilisha majukumu vinaweza kuharibu biashara haraka.

Nidhamu si kumtesa mfanyakazi. Ni kujenga utamaduni ambao kila mtu anajua kazi yake na anawajibika kuifanya vizuri.

🤝 5. UTU: Heshimu Watu Wanaokusaidia

Kama una biashara na una wafanyakazi, usiwachukulie kama mashine. Wao ni binadamu.

Waheshimu, wasikilize na jali mahitaji yao inapowezekana. Mshahara pekee haujengi loyalty.

Wafanyakazi wenye kuheshimiwa wana uwezekano mkubwa wa kujiona sehemu ya biashara badala ya kuona ni sehemu ya kupita tu.

⚠️ Usidharau mahusiano kazini. Migogoro, kutokuaminiana na mazingira mabaya ya kazi vinaweza kuleta hasara kubwa kwa biashara.

🔥 6. BIASHARA NI FULL-TIME

Hili ndilo somo nililolielewa kwa maumivu.

Biashara ndogo haiwezi kutegemea uwepo wako mara moja moja halafu utegemee ikue yenyewe.

Kama hauko tayari kuweka muda, nguvu na attention yako kwenye biashara, fikiria investment ambayo haihitaji uwepo wako kila siku.

Kuna tofauti kati ya kuwa mfanyabiashara anayesimamia biashara na kuwa investor anayemiliki sehemu ya biashara.

Ujumbe mkubwa niliojifunza:

Biashara haikui kwa sababu tu una mtaji. Inakua kwa nidhamu, reinvestment, usimamizi, muda, watu sahihi na maamuzi sahihi.

Mangi alinionyesha kwamba wakati mwingine tatizo si biashara yako. Tatizo ni namna unavyoendesha biashara.

Leo Mangi ni mfanyabiashara mkubwa wa maduka ya jumla ya vyakula. Mimi nilichukua somo moja kubwa kwake: panua fikra zako.

Kama umejipanga kufanya biashara, usiingie kwa hisia tu. Jifunze. Uliza waliokutangulia. Kosea kidogo. Rekebisha mapema.

Na zaidi ya yote, usitumie hela yako yote kujaribu kuonekana umefanikiwa kabla biashara haijafanikiwa.



Tehama inaleta mabadiliko makubwa sana katika ulimwengu wetu tena kwa kasi kubwa mno, kasi hii ina pande mbili  yaani nzuri na upande mwingine ni hatari. Katika uzuri wake ni kweli mtumiaji wa mwisho hupata urahishwaji zaidi wa kazi na ubora zaidi ila kasi hii kwa upande wa biashara na wataalamu waliopo ndani inaweza kukuza na hata kuua biashara kwa kuchelewa kidogo.

Yafuatayo ni mambo 5 muhimu kujua kama unataka kuingia katika ulimwengu huu wa tehama kwa njia ya kusoma au kufanya biashara.


  1. Kubali mabadiliko haraka na zaidi jifunze kuendana nayo kwa uharaka huo huo kama yalivyoingia, kwa sababu unavyoyagomea au kuchelewa kubadilika ni kama kuivisha biashara yako kitanzi.
  2. Mfano :
    kampuni ya zamani ya kutengeneza programu za kusafu(browse) mtandao yaani browser inayoitwa Netscape ilikuwa inauza programu zake na kufaidika sana lakini ghafla kampuni ya Microsoft iliamua kutengeneza na kugawa bure browsers hali iliyopelekea kampuni ya Netscape kwenda mahakamani kuizuia kampuni ya Microsoft ila haikufanikiwa ilikufa baadaye kwa kukataa mabadiliko.
     2. Uwe mtu wa kupenda kujifunza sana kupitia mtandao wa internet na mara kwa mara kuangalia            teknolojia mpya ili usije ukashtuliwa na kuingia kwa teknolojia mpya.
    
    3. Weka maono makubwa na ya mbali yanayoendana na eneo husika na ukuaji wake wa teknolojia          na pia ukilinganisha na ukuaji wa teknolojia hiyo duniani.
       Mfano: unapofungua Internet cafe sehemu nyingine hazihitaji kabisa hiyo huduma kwa sababu             ya jamii husika ina kipato kikubwa na sehemu nyingine inahitaji huduma za printing tuu na              copy, na sehemu nyingine inahitaji zote yaani internet,printing na copy(ila hiyo sio investment               pekee).
        
     4.Kwa Wanafunzi
   Wanafunzi wa ulimwengu huu wa tehama wana kazi mbili ya kwanza ni upokea kinachotoka               chuoni na ya pili ni kuupdate kile kinachotoka chuoni kwa sababu teknolojia hukua kwa kasi na        hata ikibadilishwa mitaara kwa kasi kiasi gani vyuo havitaweza kuendana na kasi hiyo na hata           kuwafanya wanafunzi kupoteza kufahamu misingi ya teknolojia kwa uzuri zaidi.

    5.Kutokana na kubadilika badilika kwa sekta hii inakupasa kuweza kujua kiwango cha mabadiliko ndani ya sekta hii . Mfano biashara ya kuuza simu ina kiwango kikubwa sana cha mabadiliko(simu hupitwa na wakati kwa haraka zaidi ya laptop) ukilinganisha na biashara ya kuuza kompyuta pakato(Laptop) ila zote zinabadilika.

    6.Onana na wafanyabiashara husika na pia IT Professionals au IT Consultants maana wao hujua soko lipoje na faida ipoje katika maeneo mengi ya ICT na kitu cha kuwekeza kwa sasa na kwa njia gani utaanza kuwekeza.

  Kwa ushauri zaidi wasiliana nasi!



Kwa miaka tumekua tukiona watu wanaanzisha mablogu kama michuzi, milardayo na wengineo wengi, na tunafurahi maana wanatuletea taarifa nyingi kwa kweli, lakini unajua hawa wanapata hela nyingi ambazo hata wewe unaweza pata!!!

Blogu ni tovuti ambazo zinaruhusu mtumiaji aweze kuhusishwa na kile ambacho kimewekwa kwenye tovuti, kama habari kwa mfano, mtu anaweza iona na kuandika yeye ameiopokeaje na hata kuwasiliana papo na hapo kwa watu wengine kuhusu habari hiyo.

Je kuanzisha biashara hii inagharimu kiasi gani?
Kuanzisha biashara hii inahitaji uwelewa wa utumiaji wa mtandao, inahitaji uwe na internet zaidi ya hapo hakuna gharama nyingine zaidi...Kumbuka: uelewa huu wa mtandao sio wa kwenda chuo ni uelewa mdogo tuu  ambao unaweza kujua ndani ya wiki 2 au moja tuu.

Nini kinahitajika ili kuanzisha biashara hii?
unahitaji kitu cha kuandika, mfano michuzi yeye kaamua kujikita kwenye habari na kwa hilo amewapata wengi ambao wanatembelea kwenye blogu yake...kama hauna fikiri kwanza ni kitu gani  watu gani wanataka.

Unapataje pesa sasa?
Jinsi blogu yako itakavyo vuta watu wengi na kuingia, basi utapata hela kwa njia zifuatazo;

  • Matangazo
Ukitembelea blogu hizi utakuta matangazo kama ya vodacom na makampuni mengine ambayo hulipa mtu anapoclick tuu na hata mtu anapoliona hilo tangazo. Mfano mkikubaliana mtu anapoclick upate Tsh 100 na kuendelea na kwa mwezi labda ulipwe laki 4 ni wewe utachagua na kukubaliana na mwenye tangazo.

  • Pia unaweza uza vitu kama vitabu vya mtandao vyenye mafunzo mbali mbali kwa njia ya sauti au video kwa watu.

  • Unaweza pia ukauza post zako kwa njia ya kuwaweka kampuni kama ndio wamechangia kuileta...mfano: unawe za kwenye TV kipindi cha Tamthilia unasikia tamthilia hii imeletwa kwenu na Wizara ya afya.
Ukweli ni kwamba huku ubunifu wako utakuletea pesa, na kujitoa kwako na ukitaka kujifunza hivi endelea kutembelea hapa na karibuni tutaleta mafunzo haya bure.

Tehama(ICT) na Teknolojia kwa ujumla imeweza kuajiri zaidi ya milioni 6.7 na inawalipa mara 2 zaidi ya sekta nyingine katika Nchi ya Marekani(compIT), lakini kwa hapa Tanzania bado fani hii ina watu wachache sana na ukizingatia vijana wengi wanalalamika ukosefu wa ajira.

Kwa nini ni jawabu mojawapo la Ajira?

  • Mtaji wake ni mdogo sana na ukilinganisha na maeneo mengine ya kuwekeza kama kilimo na sekta nyingine na pia unalenga vijana zaidi ambao ndio wanakumbwa na tatizo hilo la ukosefu wa ajira.
  • Tehama haihitaji mtu aajiriwe ili aweze kujipatia kipato kwenye sekta hii kwa maana hutegemea zaidi ubunifu wa mtu na juhudi zake binafsi na mahali mtu alipo ndio panaweza geuka ofisi.
  • Unaweza ukajifunza tehama bila hata kuingia darasani au kwenda chuoni na ndani ya mwezi ukawa vizuri kabisa.

Ukitaka kujifunza tehema wasiliana nasi tutakupa mwanga katika tasnia hii.



 Programu bora Afrika
   Afrika hatuna haja ya kushindana kugundua teknolojia kama Mataifa mengine kwa maana huko huhitaji pesa nyingi sana, ila tunaloweza kufanya ni kuitumia teknolojia iliyekuwepo na kuiweka katika mazingira ambayo itatusaidia katika maisha, Pongezi ziwaendee hawa wataalamu hawa wa tehama walivyo weza kufanya haya. Angalizo zipo nyingine sokoni pia ila muda unavyozidi kwenda tutazigundua na kuzitangaza ili zifahamike. Tazama hapa