Ulimwengu wa Computer umeanza zamani na unakwenda kwa kasi ya ajabu, maarifa yaliyokuwa yanafanya kazi mwaka juzi, mwaka huu hayafai tena kama unataka kuingia katika ulimwengu huu unahitaji kujitoa kujifunza kwa speed kubwa.
Ulimwengu wa computer unajumuisha maeneo mengi ndio maana zikaanzishwa kozi za Computer science na Information Technology kumsaidia mhusika kuweza kufahamu maeneo yote angalau kwa uchache, Na kulingana na hali hii hizi course zimekuwa zikitengeneza system administrators wazuri sana maana likitokea tatizo kokote wanajua shida iko wapi.
Cha kushangaza Takwimu zinasema ya kwamba, wanaongoza kukosa ajira ni waliosoma Computer Science.
Hizi ni mojawapo ya sababu zinazowafanya wahitimu wa computer science wengi kuhangaika kukosa ajira...na kuifanya hii kozi kuwa imepitwa na wakati kwa sasa.
Kozi haiandai wahitimu wake kwa soko la ajira.
Hii kozi imetengenezwa kukupa maarifa mengi sana juu ya vitu katika ulimwengu wa computer, yaani hutoa msingi tuu wa vitu mbali mbali ambavyo havihitajiki katika kazi za kila siku za Computer Expert, soko linataka Skills mbali mbali na sio maarifa mengi.
Mifumo ya kizamani ya ufundishaji.
Tulivyokuwa kuwa chuo kuna wakati nusura watu wagome, kwa sababu ya elimu iliyokuwa inafundishwa ilikuwa nyingi imepitwa na wakati, na mavyuo yana changamoto hiyo kubwa kupambana na kubadilika kwa mifumo, na wakufunzi wengi sio wazuri katika kufundisha, kwa wanafunzi wanajikuta wanalazimika kusoma maarifa ambayo yamepitwa na wakati ili wafaulu.
Kutokusoma vitu kwa undani.
Uliwengu wa sasa unahitaji watu wa kuingia moja kwa moja katika maeneo mbali mbali, mfano network engineering, cyber security, software engineering na sio mtu anayejua network kidogo, cyber kdgo na software eng. kdgo...hii ni hatari, na hatakama ikimtaka mtu wa design hii itamtaka katika level ya masters na sio graduate aweze kusimamia IT department. Na hali hii inamlazimu mtu aliyesoma computer science asome vyeti vya ziada ili apate ajira.
Gharama kubwa
Hii kozi ya Computer Science mavyuoni ni hela nyingi na zaidi inabidi mtu asome vyeti vya ziada, kwa ajili ya skills za ajira, na pesa zinazidi kuongezeka. Bachelor of Computer science ni miaka 4 inapoteza muda sana wa mtu, ili usome miaka 3 inabidi iwe Bachelor of science in computer science...so unavyochagua kusoma hii kozi ufahamu hayo.
Imepoteza umuhimu wake.
Focus kubwa sasa hivi katika uliwengu wa sasa, haipo tena katika kufahamu vitu vingi tuna AI kwa ajili hiyo, ipo katika kufahamu ujuzi fulani vizuri sana mfano coding, ujuzi ambao watu wako teyari kulipa pesa kupata huduma yako. Na kozi hii inaenda kinyume na huo mwelekeo, wengi wanamaliza bila kuwa na ujuzi wowote wa maana...na zaidi watu walikuwa wakiamini unahitaji kujua computer science ili ujifunze coding ila siku hizi tuna watu kutoka professions mbali mbali na wanajifunza coding hadi wanasheria..wapo..
Tunasonga mbele vipi...
Kuna kipindi tulikuwa tunahitaji watu wa kusimamamia mifumo ya computer, watu ambao watakuwa na maarifa mengi na ndio maana kozi ya computer science ikazaliwa, ila tunavyozidi kwenda tunahitaji watu waliojikita zaidi katika eneno fulani mfano software development sasa hivi tunahitaji vijana wengi sana katika eneo hilo na ndio kazi pekee ambayo unaweza fanya ukiwa kokote duniani...ukiwa kokote kule.
Kwa ushauri wangu kama unataka degree soma IT, ila fanya uwezalo ndani ya hiyo miaka mitatu uwe una ujuzi specific kabisa ikiwezeka soma online courses ukiwa chuoni...ili pale kwenye eneo lako la CV kwenye skills liwe kama ifutavyo:
SKILLS:
User Experience (UX) Design, Digital Marketing, Artificial Intelligence (AI) & Machine Learning (ML), App Development , Cybersecurity...E.T.C
CODING SKILLS:
JavaScript, Kotlin, Python, Rust and C/C++
Na zaidi na zaidi na hizo lugha usiseme tuu unajua ziwe backed na project ambazo umefanya kutumia hizo lugha na macertficates ya network ukisoma UDSM utayapata ya CISCO...au kama nimekutisha sana...kuna Unesi pia pale Muhimbili 😂😂😂
ila katika kozi zote ni IT ndio unaweza kujiajili kwa uaharaka na uwepesi zaidi hata kama huna mtaji wowotw zaidi ya computer mie chuoni nilikuwa natengeneza website navuta hela..nimemaliza hadi leo navuta hela huku na kule so komaa..
Nakubali bro shukurani sana kwa ushauri na maarifa tele Allen creator hapa
ReplyDelete