Kabla Hujaamua kutengeneza tovuti kwa ajili ya biashara yako...2025




Tovuti(website) ni kurasa za kielectroniki(webpages) zinazohifadhiwa katika kompyuta server ili ziweze kupatikana kwa urahisi pindi zinapohitajika na watumiaji wengine waliopo kokote kule duniani kwa njia ya mtandao wa intaneti.
Mfano wa kurasa maarufu zaidi ni google.com na facebook.com.

Mambo yanayohitajika kuwepo kwenye tovuti.
  • ·         Utangulizi  mfupi wa biashara yako.
  • ·         Bidhaa zinazopatikana na njia ya kuzipata.
  • ·         Ubora wa bidhaa zako.
  • ·         Upekee wako kwenye soko.
  • ·         Mawasiliano ya kufika kwenye biashara yako.
  • ·         Maono ya biashara yako.

Mambo muhimu ya kuzingatia katika tovuti yako.
  1. · Usiweke taarifa nyeti za biashara yako kwenye tovuti maana kila mtu ataona hata adui wataona na watazitumia kukushinda kwenye biashara.

  1. · Usiweke taarifa nyingi kwenye tovuti, Maelezo mengi hayastahili kuwepo kwenye tovuti maana hakuna atakayesoma Maelezo hayo Zaidi yako, weka Maelezo mafupi na yenye kutosheleza.

  1. · Usiweke picha halisi ya eneo lako la biashara kama halina mvuto au ubora mkubwa.

  1. · Usitumie picha ambazo hazina uhalisia kabisa katika biashara yako au eneo ulipo, mfano kuweka wazungu wakati Wateja wako wengi ni weusi.

  1. · Weka taarifa fupi zile tuu zinazomchochea mtu kutaka kujua zaidi ili apige simu na kufika ofisini.

  1. · Fahamu Wateja wako ni watu wa aina gani ili uweze kuongea nao vizuri mfano kama ni Watu wa daraja la kati na chini kwa kipato na ni watanzania Zaidi hapo tumia lugha ya Kiswahili lakini kama watu wako ni watu wenye pesa na wamataifa mengine mengi tumia kiingereza.

  1. · Tumia wataalamu wazuri wa lugha ili kusiwe na makosa ya sarufi katika tovuti maana hufanya biashara yako  ionekana ya uchwara. 
Fuata hayo na mengine mengi kwa ushauri ntumie barua pepe na mimi nitakusaidia.

  


0 comments:

Post a Comment