Kuomba kazi ni jambo la kawaida na ni njia mojawapo ya kufikia malengo yako. Kuna vigezo vingi ambavyo hutumika kumuita mtu aliyeomba kazi kwenye usaili(Interview).
1. Uwezo wa kuifanya kazi kwa ubora zaidi kuliko wengine wanayoiomba.
2.Elimu.
3.Ujuzi.
Ukiangalia pointi namba moja itatumika Zaidi au itaonekana tuu ndani ya barua ya maombi ya kazi(cover letter/application letter).
Yafuatayo ni ya kuzingatia unapoandika hiyo barua.
1.Mtangulize Mungu mbele.
2. Kama ni ya kiingereza basi hakiki msamiati wako uwe sahihi na unaotumia lugha nyepesi na isiyo na maneno ya kitaalamu mengi.
3. Aya ya rejea(reference) eleza umetoa wapi taarifa ya kazi husika.
4. Unapohitaji kutaja hiyo kampuni, itaje jina lake na sio kuishia kutaja kampuni. Mfano “Ningependa kufanya kazi Vodacom” hii ni safi wakati “ningependa kufanya kazi kwenye hii kampuni” hii ni mbaya.
5. Onyesha ya kwamba unapendezwa na kazi yao, Zaidi pale kama shirika husika ni NGO ya kijamii au hata serikalini.
6. Onyesha ya kwamba unafahamu malengo yao na ungependa kua mmoja wao katika kuyafanikisha.
7. Eleza kwa nini wewe unafaa zaidi kuliko wengine walioomba nafasi husika. Tumia vigezo vifuatavyo.
· Ujuzi wako
· Ari yako ya kufanya kazi
· Mapenzi binafsi kwa kampuni.
· Ikiwezekana jinsi malengo yako yanashabihiana na ya kampuni husika.
8. Tumia maneno machache na barua iwe fupi, ikiwezekana, upande mmoja tuu wa karatasi.
9. Tambua unayemwandikia ni afisa rasirimali watu, kwa hiyo chunga lugha yako isiwe ya kitaalamu sana la sivyo hatakuelewa na ataweka barua pembeni.
10. Kama unatuma barua kwa njia ya posta inapendeza na inafaa uiandike kwa mkono barua yako ya kazi na sio kutype barua hiyo labda ikiwa pale wametaka wenyewe.
Mfano:
Mpendwa [Jina la Mwajiri],
Ninaandika barua hii kuonyesha nia yangu ya kuomba nafasi ya Afisa wa Teknolojia ya Habari (IT) katika [Jina la Kampuni], kama ilivyotangazwa kwenye mtandao wa ajira portal wa serikali. Kwa uzoefu wangu katika elimu ya IT na uzoefu wa vitendo katika kubuni tovuti, nina furaha juu ya fursa hii ya kuchangia kwa timu yako na kusaidia kufanikisha dhamira yako.
Katika nafasi yangu ya awali, niliweza kusimamia miradi mbalimbali ya IT, ikiwemo kubuni na kuzindua tovuti za NGOs kama vile The Green Foundation Services huko Zanzibar. Utaalamu wangu katika miundombinu ya IT, usimamizi wa mitandao, na usalama wa mtandao imenifanya niweze kutoa msaada kamili kwa mashirika na kuhakikisha uendeshaji mzuri wa mifumo yao ya teknolojia.
Ninavutwa sana na [Jina la Kampuni] kutokana na kujitolea kwake kwa [dhamira maalum au mradi wa kampuni]. Niko tayari kuleta ujuzi wangu katika usimamizi wa IT, utatuzi wa matatizo, na ushirikiano wa timu ili kusaidia kufanikisha malengo yako.
Asante kwa kuzingatia maombi yangu. Natumai kupata nafasi ya kujadili jinsi uzoefu, ujuzi, na vyeti vyangu vinaweza kuwa na thamani kwa timu yako. Tafadhali jisikie huru kuwasiliana nami wakati wowote kwa ajili ya kupanga mahojiano.
Wako kwa dhati,
[Jina Lako]