Hizi ni software za computer ambazo hazijapatikana kufuata utaratibu uliowekwa na mtengenezaji wa software hizo.
Njia za kupata software hizi.
- kuwekewa na mtu asiyeaminika bila kununua kwa pesa halali software hiyo.
- Kushusha/download programu hiyo kutoka kwenyesehemu isiyoaminika kwenye Programu internet.
- Programu hiyo inaweza kufanya kazi kwa kiwango kidogo kuliko kilichokusudiwa na mtengenezaji kwa sababu ya kuharibiwa ili iweze kuruhusu watu wengi kutumia bila kununua.
- Programu hiyo mara nyingi huweza kuingia na virus kutoka kwenye internet na kuharibu computer yako.
- wewe unaye download hizi programu za wizi unaweza kugundulika na kukamatwa hata kufungiwa vitu vyako kwenye internet na watu wenye mamlaka husika, mfano kwenye nchi kama Uingereza unaweza kukamatwa pale pale ulipo pindi unaanza kudownload programu hiyo ya wizi. Adhabu ni faini ya pesa nyingi au kifungo.
- Programu hizi kutokana na kuharibiwa kwenye mfumo wake ili isidai uhalali wa mtumiaji huwez kuharibika/ crashing muda wowote na kupotea na data/taarifa zako zote muhimu.
- Unasaidia kuchochea uharibifu wa mali za watu kwa ujumla.
Ushauri.
Ni muhimu sana kununua programu/software kwa usalama wako binafsi na mali zako na pia kwa maadili mema.
ECL Computer Clinic Advice.
0 comments:
Post a Comment