Huwa inafika muda katika kila biashara, ambapo inatakiwa ikue na itanue mipaka yake au ibaki kama ilivyo na isubiri kuanguka.


Muda umebadilika, jinsi biashara ilivyokuwa ikifanyika miaka 10 hadi 15 iliyopita sivyo inavyotakiwa ifanyike sasa, wateja ulikokuwa ukiwategemea miaka 10 au 15 iliyopita hawatakuwapo tena.

Hapo ndio inabidi ubadilishe mbinu za biashara, utafute mbinu za kuwafikia wateja wapya na huku ukiongeza ubora wa huduma zako kwa wateja wako waliopo.

Ndio maana tunakushauri upanue mipaka na utengeneze tovuti ambayo itakusaidia kukutangaza Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, na pia itakuwapa imani wateja wako ya kwamba wapo wenye mikono sahihi na kampuni au biashara inayokwenda na wakati.

Furahia Offer hii, 50% Discount ili usije ukawa mojawapo ya biashara nyingi zinazoendelea kufungwa hapa mjini.

Tehama(Information technology) Katika nchi za chini ya jangwa la Sahara, Afrika Mashariki bado ni changa sana. Na kama inavyofahamika teknolojia hurahisisha sana maisha na hupunguza mzigo mkubwa wa kazi kwa watu.

GUNIA ZITO.

Nimeifananisha na gunia zito kwa sababu kutengeneza teknolojia mbadala ili kuweza kutatua changamoto katika jamii inahitaji mafunzo, moyo wa kujitoa binafsi na jitihada zaidi.

Lakini pia inahitaji macho ya kuona hizo fursa katika jamii ili uweze kuzifanyia kazi. Watu wengi hukimbilia kazi ambazo hazihitaji sana ubunifu lakini huku ubunifu ndio mahali pake, pindi unapokosa akili za  ubunifu basi utashindwa kufanya lolote katika tehama.

LENYE PESA

Kama nilivyoeleza hapo mwanzo, pindi teknolojia hizi zinapotengenezwa na wataalamu, huingia sokoni na kurahisisha maisha ya wengi.
watu wengi, makampuni mengi na watu wengi yametajirika sana duniani kwa tehama, mfano 

kampuni kubwa zaidi ya Tax duniani haimiliki tax hata moja bali imeunganisha wamiliki wa Tax,
lakini tatizo waliloliona ni shida ya kupata Tax pale ambapo unaihitaji na haupo barabarani. 

UBER  kwa sasa inaingiza mabilioni ya Pesa duniani kote, hata hapa Tanzania zipo programu kama za mpesa, tigopesa zinaingiza pesa nyingi mno, 

zipo programu za vituo vya mafuta kama Petronite

zipo programu za maduka kama duka pro,

na programu za masomo kama thL na kadhalika na kadhalika...

JINSI YA KUWA MMOJAWAPO WA WABEBAJI.

1. Uwe na uwezo kujifunza kwa bidii sana, na kukuballi kutatua changamoto mbali mbali hata zisizolipa kwa muda huo.

2. Chukua masomo ya Tehama kuanzia ngazi mbali mbali kama cheti, diploma au degree.

3. Ikiwa huna vigezo, basi ujue kusoma na kuandika kiingereza vizuri na uwe na moyo wa kishujaa wa kusoma zaidi ya wale wanaosoma darasani ila ni lazima utafanikiwa.

Janga la ukosefu wa ajira haliwezi kuisha kama tutaendelea kusaka watu kutoka njee wafungue makampuni ndio tuajiriwe ila tuu kama sisi wenyewe tutakapoamua kutoka na kugeuza changamoto kuwa mtaji wetu.

Kwa maswali wasiliana nami katika, 
elisanteshibanda@yahoo.comTehama(Information Technology), imejaa fursa nyingi, na katika nchi zetu changa, fursa ni nyingi mno.

Katika Tehama juhudi za mtu binafsi na Mungu wake, ndio zitamfanya afinikiwe au asifanikiwe.

Mtaji wa Tehama ni computer tuu, ambayo ni gharama ndogo sana kuipata.

Ni vitu gani mtu anaweza soma/jifunza ili afanikiwe katika Tehama.

Graphics Design(Sanaa ya Matangazo)
Hii ni sanaa ya matangazo ya biashara. Hakuna biashara duniani isiyotaka matangazo

na ukiangalia dunia ya leo, tumezungukwa na matangazo, yanazidi kuwepo na jinsi biashara zinavyozidi kuongezeka kasi ya uhitaji wa matangazo inazidi kuongezeka.

Jinsi ya Kujifunza
@ Chukua kozi fupi ya wiki 6, na wewe utaweza kuwa vizuri kwenye sanaa hii. 
Vigezo: Kuanzia Form Four Leaver
Price: 300,000Tsh
Training: MAXPO training
Mahali: Rains Technologies, Ilala Bungoni, Chunya str.

@Tumia njia ya Video ya kujifunza, kwa kutumia mitandao kama Youtube.

Web Development
Huu ni utaalamu wa kutengeneza tovuti mfano wa tovuti ni kama cnn.com, bbc.co.uk n.k 
Kila biashara inavyokua na kutaka kupita mipaka ya kiwilaya, kimkoa au kitaifa inahitaji tovuti kwa ulazima. Maana tovuti ni ofisi pekee ya kampuni ambayo inaweza fikiwa na mteja ,
Akiwa kokote kule duniani.

Kwa kuangalia uchumi wetu unavyokua na ongezeko la makampuni soko la tovuti litaongezeka maradufu.

Jinsi ya kujifunza
@Chukua kozi fupi ya wiki 8, ujifunze kutengeneza tovuti.
Training: MAXPO Training
Bei: 400,000/-Tsh
Mahali: Rains Technologies, Ilala Bungoni, Chunya str.

@Chukua certificate in InformationTechnology/Diploma/Degree kwa mwaka 1, 2, 3 N.k
Mahali: University of Dar es salaam Computing Centre
Vigezo: Tembelea chuoni.

@Tumia mafunzo ya vitabu na video za kwenye mtandao ili kujifunza kutoka kwa watu mbali mbali.


Computer Application
Kozi hii inakuweza kuifahamu computer ndani na njee, kuendesha stationery, na hata kutumia computer ya windows 10 na Apple computer(MAC OS) kama mtaalam.


Lakini pia inakupa uwezo wa kujifunza microsoft office yote.
Pamoja computer networks.

Jinsi ya kujifunza
@Chukua kozi fupi  ya wiki 4 ya Computer application.
Vigezo: Yeyote
Training: MAXPO Training
Bei: 250,000/-Tsh
Mahali: Rains Technologies, Ilala Bungoni, Chunya str.


@Chukua certificate /diploma/ degree katika Information Technology, computer science, ICT.
Mahali: University of Dar es salaam Computing Centre
Vigezo: Fika Chuoni.

@Tumia mtandao wa youtube kujifunza na google kupata vitabu.

Mafunzo ya Tehama, yanaanza taratibu na ni marahisi kwa mtu mwenye jitihada ya kusoma na nidhamu ya kujifunza bila kukata tamaa.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nami katika 

elisanteshibanda@yahoo.com
                  


Interview za mchujo ni interview za awali, ambazo hutumika kupunguza watu wengi walioomba kazi husika,

ili wabaki wachache kwa ajili ya hatua ya pili ya interview(usaili).
Interview hizi zina sifa kubwa sana ya kuvunja mioyo ya watu walioomba kazi, kwa watu wengi hujikuta wamejiandaa visivyo na kufanya vibaya.


Hebu kwanza tufahamu mambo ya kuzingatia unavyojiandaa na interview.


Muombe Mungu akusaidie kujibu kwa ufasaha, maana ni rahisi sana kujibu visivyo, pamoja ya kuwa unajua kila kitu.Fahamu kwa undani kazi iliyotangazwa. Ni rahisi kusema, mimi nimesoma chuo kama IT, Computer science N.K na ndio maana kozi yangu imeorodhoshwa na nikaitwa, 
ila kufikiri huko sio sahihi na wengi hufeli maswali yanayohusiana na kazi hiyo. 
Fanya utafiti wa hali ya juu kwenye mtandao au kwa waliokwisha fanya teyari na uelewe.Fahamu majukumu yaliyotangazwa na kazi husika na uhakikishe unayafahamu jinsi ya kuyatekeleza yote
au kama ukishidwa yote angalau ujue nini kinaendelea,     kwa maana maswali mengine hulenga humo.


Fahamu ni masomo/kozi gani yanayoendana na kazi husika,uliyoyasoma chuoni, halafu uyapitie kwa umakini.


MIUNDO YA MASWALI YA INTERVIEW(USAILI)

Muundo wa 1

Muundo huu utakutana na maswali 40 hadi 50, yanayokuwa ya kuchagua, na huwa yanagusa sehemu mbali mbali, ila zaidi sehemu zinazohusiana na kazi husika na sub course husika mojawapo huonekana kwa wingi.

Mfano:
Kazi ya Business analyst, maswali mengi asilimia 60-70 yatakuwa ya software engineering.

Jinsi ya kujiandaa:
Tafuta subcourse husika na uisome sana gusia maeneo mengine pia.

Muundo wa 2

Muundo huwa na maswali 4 hadi 5, ila maswali huwa yanalenga maeneo husika na yale ya kuzunguka.

Mfano:
System Administrator, maswali 2 yatahusiana na Networking lakini 2 mengine yawaweza kugusa database na hardware.

Jinsi ya kujiandaa:
Soma yote yanayoendana na kozi husika na course zinazoendana na hiyo course.

Muundo wa 3

Muundo huu una maswali 4 hadi 5, na maswali hugusa course husika tuu na huulizwa kwa mfumo wa maswali ya scenario.
Mfano:
System Administrator, maswali yote ni ya networking, na yanaulizwa yakitakiwa kujibiwa kitaalamu na sio kitaaluma
Namaanisha kitaalumu ujibu kama mtu mwenye ujuzi na scenario hiyo  na sio kama mtu aliyakariri kutoka kwenye kitabu. 

Jinsi ya kujiandaa:
kama una uzoefu kumbuka uzoefu wako, kama una mafunzo ya certifications yatumie ipasavyo, lakni kama huna hivyo vyote usijali jiandae vyema na sub course husika nawe utafanikiwa.

Muundo wa 4

Muundo huu huwa na maswali 4 hadi 5, ambayo hujikita zaidi kitaalamu na katika majukumu yaliyorodheshwa na tangazo la kazi.

Jinsi ya Kujiandaa:
Soma kwa umakini yale majukumu ujue jinsi ya kuyatimiliza kivitendo kila moja na kama kuna vigezo vipitie hata ujue tuu kwa mbali nini kinaendelea.

Angalizo:
Ni kawaida kabisa kumaliza mtihani huu usijue kama umefaulu au umefeli, na hali hii huifanya ionekane ngumu sana, ila kabla ya kujibu swali tafakari linahitaji nini na ujibu vizuri ukujibu juu juu uamini kuna watu watajibu kwa umakini kuliko wewe.


Hiyo ni muundo ambayo imekuwapo ila inaweza badilika muda wowote hata kesho ikaja mengine zaidi, na sijakugusia interview za awamu ya pili na za mahojiano,ila kwa hayo chukua hatua, na nikutakie interview njema.
Kwa ushauri zaidi wasiliana nami 
elisanteshibanda@yahoo.com


Imekuwa ni jambo la kawaida huku mavyuoni kutenganisha ajira na masomo, 
haswa katika vyuo vyetu hapa Tanzania, 
kiasi ambacho tumekuwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira,
 ambalo ukilatazama kwa umakini kuna uwezo fulani wahitimu wanakosa ndio maana, tatizo linakuwa kubwa mno. 
Lakini pia kuna sababu za msingi tuu ambazo ni za kiuchumi ambazo hata wahitimu hawahusiki ambazo zinakuza tatizo hili.

Kwa upande wa Information Technology na kozi zote zinazoendana na hiyo kozi, 

kuna vitu vifuatavyo ambavyo mwanafunzi akivifanya vinaweza fungua njia au 
kupanua wigo wako wa ajira kwa kiasi kikubwa sana. 


GPA/ UFAULU CHUONI

Huu ni ufaulu wako chuoni, najua ninavyozungumza hivi kwa wingine ni kama kuwaambia wanywe maji ya sumu, ila ndugu zangu hakuna jinsi, 
 GPA ina faida kwanza GPA kubwa inachangia kwa kiasi kukuitisha katika interview ya kazi,

kwa maana inaonesha una uelewa mkubwa na inaonesha kwa kiasi unaweza chapa kazi,
kama ulisoma kwa bidii kwa kiasi hicho basi unaweza ukawa na bidii hata kazini.

Lakini pia mavyuoni tunahitaji wahadhiri na kigezo kikubwa ni GPA ndio utaitwa kwenye interview za huko na hata watu wanaoomba ni wachache sana.
GPA nzuri huanzia 3.5 na kuendelea ila vyuoni ajira zake inategemea huwa inaweza anzia 3.5 wakati mwingine 3.8.


PROFESSIONAL CERTIFICATIONS/ VYETI VYA UTAALAMU.

Hivi ni vyeti vya kitaalamu yaani kubobea katika sehemu fulani, 
hivi havikupi degree au diploma, ila inapewa hadhi ya kuwa mtaalamu katika eneo moja tuu la IT mablo linaweza likawa sio kubwa. 


Mfano 
ukitaka kubobea kwenye networking lazima upitie CCNA Certifications, MCSA na kadhalika. 
Katika kazi kama za System Administrator bila vyeti kama hivi kuapply ni kazi bure na hata kama ukiitwa mitihani inaweza kukushinda kwa ugumu wake. SKILLS/UJUZI BINAFSI

 Katika maswala ya IT, swali halipo sana unamefundishwa nini
 ila lipo katika unaweza kufanya nini 
na unajua nini?


Hakuna muda mzuri wa kujifunza lugha mbali mbali za computer 
na kujua jinsi ya kuzitumia kama muda huo, 
maana kuna kujiajiri kwingi sana huko na hata serikali na mashirika,
yanatafuta watu wa kutengeneza software  mbali mbali.
Mfano wa lugha za kujifunza ni Android, Java, HTML, PHP,Javascript, CSS, Ruby, Python N.K.
Na pia uwezo binafsi wa kutengeneza programs peke yako, websites, blogs N.K

PUBLIC WORKING PROJECTS/Project ambazo umefanya na bado zinafanya kazi.

Tofauti ya elimu ya vyuo vyetu na vyuo vya njee,
ni kwamba mkazo uliokuwepo upo kwenye projects au practical,
ni mkubwa sana ukilinganisha na hapa ambao upo kwenye nadharia zaidi. 

Kwa hiyo hakikisha projects unayofanya inatatua matatizo ya jamii.
Hiyo hata kwenye interview sehemu ya projects inaweza mvutia HR kukuita.


IMPORTANT INTERNSHIP EXPERIENCE/MAFUNZO YA VITENDO YENYE TIJA.

Unapofika muda wa kutafuta field usifanye mzaha, tafuta makampuni ya kiteknolojia, ili ijifunze jinsi yanavyofanya kazi na hata kupata kazi kwenye makampuni mengine itakuwa rahisi kwa maana mzigo wa kuku train utakuwa umepungua.


Hayo ni maeneo muhimu ambayo ukiyashughulikia vizuri hautapoteza muda mwingi kutafuta ajira, kama hali itakuwa shwari ya uchumi.
Kwa ushauri zaidi wasiliana nami,
elisanteshibanda@yahoo.com