Project ni kitu muhimu sana katika kutimiza masomo ya kozi ya IT/Computer Science/Comp Eng./Software Eng etc ila pia inaweza kukusaidia kukutoa kimaisha ukiwa chuoni na hata baada ya kumaliza chuo.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA:

  • Kupata wazo jipya kabisa ambalo halijawahi kufanyika, haiwezekani kwa 78%.
  • Programu au App inayofanya kazi na kupendwa na watu Ulaya, inaweza isifanye kazi vizuri Africa..sababu ni Tamaduni, miundo mbinu..etc.
  • Sio kila wazo la Tech, haijalishi ni zuri kiasi gani, ni muda wake, mengine watu wanaweza wasilipokee au wasilipende kwa sababu tuu ya muda bado.
  • Mawazo mazuri sio lazima yawe "complicated"magumu yaani hata tech yake, coding lundo...Hell No 😀 Issue ya muhimu ni moja tuu, kurahisisha utendaji wa kazi, na tumia technolojia ya bure kwa nafasi kubwa sana...
  • Kuchukua wazo la mtu na kuliboresha ni ubunifu pia, ila vizuri uombe kibali na pia uliboreshe kwa viwango vya hali ya juu isije ikaonekana umecopy tuu.
  • Ukitaka baadaye uwe unafanya software development, hakikisha kwenye project unajifunza ku code, yaani wewe ndio uwe mwandika code, usifanye uhuni wa kurukia rukia na kuwaachia wengine.
  • Usipende shortcuts katika coding, itakufanya ushidwe kudevelop uwezo mzuri wa kuandika programu baadaye.
  • Usiogope kupresent wazo, kwa sababu litatumia lugha nyingi au hujui utatumia lugha ghani ya computer kulitimiza, niamini utapata tuu lugha za kutumia, na utajifunza vizuri na utaweza bila shida yeyote...nimepita hapo naelewa pressure yake unaweza unahisi unataka kuaga dunia..πŸ˜‚
  • Sio lazima uwe programmer kama ni kiongozi mzuri unaweza tengeneza Team na ukasonga mbele😎 ila Programmer akisusa utajuta.πŸ˜₯
  • Mawazo mazuri ya Project ni matatizo ya kila siku, katika maeneo ya kazi, katika jamii..mfano tunaona Uber ni mtu aliona matax yanazingua..etc.

Muhimu kuliko vyote RELAAAAXXXXX...mambo yatakuwa  sawa tuu..


Kama una wazo la project na unatafuta mtu kupata kujua utalifanyaje na lugha ghani utumie wasiliana nami kupitia email yangu ya elisanteshibanda@yahoo.com, kuwa mpole utajibiwa