Computer science, Information Technology n.k ,Tofauti ni nini haswa katika Elimu, kipato na Muendelezo.2023


Ulimwengu wa teknolojia ya mtandao yaani Information technology ni mkubwa sana, na  wengi huwa wanajikuta wanashindwa kufikia malengpo yao, kwa  kushindwa kujua tofauti ya kozi zilizopo, hebu fuatilia uelewe kipi ni kipi?

Information Technology

Hii ni kozi ambayo inadili zaidi na mawasiliano ya njia ya kompyuta na uendeshaji wa mifumo/systems ya kompyuta na hata designing. 

kozi hii hutoa watu/professionals ambao ni system administrators,ICT officers, Graphics Designers etc 


watu ambao wapo kwa ajili ya kuwasaidia watu wengine kuweza kutumia vizuri, mifumo ya kompyuta.

Kazi.

Hawa watu wengi huwa wanaajiriwa, 

zaidi ila pia wanaweza kuajiajili kwa katika kufanya maintenance ya vifaa vya ICT, ICT Equipment supply, 

na hata kufunga mifumo ya network sehemu mbali mbali na akijiendeleza huweza kuwa Webmaster wa tovuti mbali mbali.

Kipato.

Mishahara yao hulipwa kulingana na elimu ya Degree au ya diploma aliyonayo kama fani nyingine na Zaidi ikizingatia kazi anayofanya na unyeti wa kazi hiyo.



Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   

Computer science.

Uwanda huu upo ndani zaidi kuliko IT, maana hawa watu mbali na kujua vitu vyote vya kozi ya IT,


pia huweza kujua kutengeneza program za aina mbali mbali za computer, na pia hufundishwa lugha nyingi za computer na huwa wako vizuri kiasi hata kwenye hardware ya computer.

Kazi.

Hawa watu utawakuta kama pia ma system administrators, business analysts, system analysts, ICT Officers, Application programmers, software developers. 

Pia wengi hujiajiari na kuanzisha makampuni/biashara za kutengeneza kompyuta hardware na software, 
websites na kazi nyinginezo nyingi katika uwanda wa technology.

Kipato

Wanapoajiriwa kipato chao hakitofautiani na IT.

Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   

Computer Engineering

Fani hii, hujikita Zaidi na hardware ya computer, huku tunapata watu ambao wanaunda vifaa ambavyo vinaweza fanya kazi na mifumo ya computer. 

Hawa kwa nchi zenye viwanda vya kutengeneza vifaa hivyo,  huwa ni soko kubwa sana, 

ila kwa nchi ambazo zinaendelea huwa bado wana soko dogo sana, na hata huogopwa kuajiriwa kulingana na Title yao ya Kuwa engineer.

Kazi.

Hawa hufanya kazi ya kutengeneza vifaa ila pia huweza kufanya kazi nyingi ambazo mtu wa computer science anafanya, 
pia ni mafundi waliobobea katika kurekebisha computer mbovu.

Kipato

Hawa huwa na mshahara wa juu kuliko IT na Computer Science, maana hulipwa katika kiwango cha ma engineers,

 lakini pia hufungua biashara kubwa za computer maintenance na hardware Suppliers na zaidi...
  

Software engineering

Katika Fani hii tunakutana na watu ambao wanataka kubobea katika kutengeneza programu za computer, 

hawa watadeal na program tuu na kidgo sana mambo mengine katika fani ya teknolojia.


Kazi.

Hawa hufanya kazi kutengeneza program za kila aina, pia huingia kwenye network na kubobea humo,

na huwa pia kuweza kufanya kazi za Computer Science kwa kiasi na hukinzana kabisa na computer engineers maana wao hufanya kazi na hardware.

Kipato

Hawa wana mshahara mkubwa wa kiwango cha Engineer kama computer engineer anavyolipwa na pia huwa wanajiajiri sana na kuanzisha makampuni ya kutengeneza programu.

 

Jinsi ya Kujiendeleza…

Ulimwengu wa Computer umejaa vyeti vya mafunzo mbali, 

ili mtu abobee katika sehemu maalumu hizo huitwa certifications mfano mafunzo ya Network hutoa vyeti,

kama CCNA, CCNP na kuendelea na mafunzo ya database kama Oracle , na hata auditing(Ukaguzi) kwa maelezo Zaidi fuatilia article yangu ya kuhusu certications za IT.


Lakini pia anaweza jiendeleza katika masters degree za vitu mbali na hata kuwa Tutorial au lecturer au professor maana bado kuna upungufu mkubwa mno katika ngazi hizo.

Kwa muongozo zaidi, Wasiliana nami katika email elisanteshibanda@yahoo.com au

Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa    

1 comment: