Project ni kitu muhimu sana katika kutimiza masomo ya kozi ya IT/Computer Science/Comp Eng./Software Eng etc ila pia inaweza kukusaidia kukutoa kimaisha ukiwa chuoni na hata baada ya kumaliza chuo.

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA:

  • Kupata wazo jipya kabisa ambalo halijawahi kufanyika, haiwezekani kwa 78%.
  • Programu au App inayofanya kazi na kupendwa na watu Ulaya, inaweza isifanye kazi vizuri Africa..sababu ni Tamaduni, miundo mbinu..etc.
  • Sio kila wazo la Tech, haijalishi ni zuri kiasi gani, ni muda wake, mengine watu wanaweza wasilipokee au wasilipende kwa sababu tuu ya muda bado.
  • Mawazo mazuri sio lazima yawe "complicated"magumu yaani hata tech yake, coding lundo...Hell No ๐Ÿ˜ค Issue ya muhimu ni moja tuu, kurahisisha utendaji wa kazi, na tumia technolojia ya bure kwa nafasi kubwa sana...
  • Kuchukua wazo la mtu na kuliboresha ni ubunifu pia, ila vizuri uombe kibali na pia uliboreshe kwa viwango vya hali ya juu isije ikaonekana umecopy tuu.
  • Ukitaka baadaye uwe unafanya software development, hakikisha kwenye project unajifunza ku code, yaani wewe ndio uwe mwandika code, usifanye uhuni wa kurukia rukia na kuwaachia wengine.
  • Usipende shortcuts katika coding, itakufanya ushidwe kudevelop uwezo mzuri wa kuandika programu baadaye.
  • Usiogope kupresent wazo, kwa sababu litatumia lugha nyingi au hujui utatumia lugha ghani ya computer kulitimiza, niamini utapata tuu lugha za kutumia, na utajifunza vizuri na utaweza bila shida yeyote...nimepita hapo naelewa pressure yake unaweza unahisi unataka kuaga dunia..๐Ÿ˜‚
  • Sio lazima uwe programmer kama ni kiongozi mzuri unaweza tengeneza Team na ukasonga mbele๐Ÿ˜Ž ila Programmer akisusa utajuta.๐Ÿ˜ฅ
  • Mawazo mazuri ya Project ni matatizo ya kila siku, katika maeneo ya kazi, katika jamii..mfano tunaona Uber ni mtu aliona matax yanazingua..etc.

Muhimu kuliko vyote RELAAAAXXXXX...mambo yatakuwa  sawa tuu..


Kama una wazo la project na unatafuta mtu kupata kujua utalifanyaje na lugha ghani utumie wasiliana nami kupitia email yangu ya elisanteshibanda@yahoo.com, kuwa mpole utajibiwa 





 

Field training/ mafunzo ya vitendo ni muhimu sana, kama mojawapo ya mafunzo ya degree/diploma na umuhimu wake upo katika;

  1. Kukusaidia kujua sehemu ya kubobea katika profession yako ya IT.
  2. Kupata ujuzi wa kwanza wa kuweka katika CV yako, kuna tofauti unaposema umefanya field MIcrosoft Tanzania na serikali ya Mtaa wa kwa Tumbo๐Ÿ˜œ
  3. Kufahamu ujuzi gani una soko  zaidi ndani ya IT.
  4. Kukusaidia kupata connection na waajiri, na kukutanisha na IT Professionals.

Vigezo vya sehemu ya kufanya field bora.

  1. Kuwe na kitengo cha IT imara katika sehemu zifuatazo kama Networking, computers configuration and maintenance, software/web development, graphics design  au Tech Training(Universities/colleges)

Networking:

Nenda kwa makampuni ya Networks au ISP(Internet service Providers) mfano Raha Telecom, Simba Networks ila sehemu nyepesi na nzuri zaidi kupata ni TTCL.


Computer Config. and Maintenance:

Nenda kwa wauzaji na wasambazaji wa computers kwa ukubwa na kwa mafundi wa computer though hii fani haina malipo makubwa sana katika Tech. labda kuwe na tenda za kufanya haya mambo katika makampuni.

Software/Web develop.

Nenda kwenye makampuni yanayotengeneza Apps and websites mfano shule soft, Nyumbani creative, smart codes na mengine mengi.
Note.
Makampuni haya huwa na wafanyakazi wachache sana so huwa hawachukui sana trainees, na wakikuchukua huwa hawana muda wa kumfundisha mtu sana sasa ujitume kweli kujifunze huku ukiwauliza maswali ya hapa na pale.

Graphics Design:

Nenda kwenye makampuni ya habari kama TBC, ITV na TV nyingine zinazotengeneza matangazo kwa wingi hata kama ni za mtandaoni.

PLAN B

Umetafuta field umekosa kabisa, muda unakwenda na chuo kinaweza  kikakuzingua, nenda sehemu ambayo haina hata IT kabisa, 
 ila iwe na Internet ya Maana nzuri , mfano halmashauri nyingi siku hizi zina network na ziko safi,  pale utajaziwa fomu zako,  ila  tumia  muda wako na internet yao kusoma online courses  za programming na vinginevyo yaani utatoka bomba kuliko hata hao waliopata field microsoft....na utaweza kufanya kazi za mtandaoni(Freelancing) kabla hata ya kumaliza chuo...na unaweza anzisha kampuni yako baadaye ni wewe tuu.


USHAURI WANGU KUPITIA MAPITO YANGU BINAFSI

Kwa kipindi tulicho nacho sasa, PLAN B ni bora zaidi, makazini na makampuni makubwa mengi hayakupi nafasi za kujifunza sana, na pia ajira nyingi siku hizi ni za freelancing kuna vijana wanapata mamilioni kwa mwezi kuwashinda hata wale waliojariwa.
chagua kipi bora ila unaweza fanya vyote pia plan A na Plan B ila tuu ujitoe kweli kweli.


SEHEMU ZISIZOFAA KWENDA FIELD

Benki:

Kwa sababu ya usalama hawatakuruhusu katika mifumo yako so utabakia kuwa mapokezi na hiyo inaboa sana.

Mashuleni:
utaishia kutengeneza kompyuta ya mwalimu mkuu na lab ambayo ina  kompyuta hovyo sana.

Serikali za mtaa.

Sehemu ambazo kuna LAN na INTERNET nenda kafanye plan B, ila tuu pakiwa haposomeki usiende.

Sehemu zote zenye matumizi madogo ya Tech usiende.

Tumia  muda vizuri, wahi na kuwa mwepesi wa kujifunza na tengeneza connection ukiwa huko, unaweza ukaitwa tena kama ni private.

Kama una maswali zaidi nitumie katika email yangu ya  elisanteshibanda@yahoo.com