Imekuwa ni kawaida kabisa kwa tovuti nyingi hutengenezwa, ili ziweze kuingiza pesa na mojawapo ya njia rahisi ni kuweka matangazo.

Aina ya Matangazo:

  • Matangazo ya baishara nyingine ya moja kwa moja
  • Matangazo ya Google(Google Ads)
Faida ya kuweka matangazo.
Matangazo haya ya moja kwa moja makampuni huweka pesa nyingi sana ili waweze kuwekewa tangazo lao kwa muda maalumu wakati matangazo ya google ads haya google hulipa kiasi kidogo kwa kila mtu anapobofya tangazo lao.

Hasara ya kuweka matangazo.
  1. Inaondoa umakini wa wageni wanaotembelea tovuti yako kwa kuishia kuangalia zaidi matangazo.
  2. Inafanya wageni waondoke haraka, wakati mwingine bila hata kuangalia kilichowaleta kwenye tovuti yako.
  3. Matangazo ya biashara nyingine yanashusha thamani biashara yako, kwa kushindwa kuheshimu kile unachokiuza wewe.
  4. Kwa matangazo ya google kuna wakati unaweza wekewa matangazo ambayo hayaendani na biashara yako na kuishia kuwakwaza wageni wako na wasirudi tena. Mfano mzuri ni tovuti ya dini inaweza wekewa matangazo ya udaku.
Ushauri.
  • Kwa tovuti za makampuni binafsi makubwa au hata makampuni yanayojiweza vizuri si vyema kabisa kuweka matangazo.

  • Kwa makampuni ya habari na mitandao ya kijamii ambapo watu huenda kuenjoy, unaweza weka matangazo
Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   

Kuomba kazi ni jambo la kawaida na ni njia mojawapo ya kufikia malengo yako. Kuna vigezo vingi ambavyo hutumika kumuita mtu aliyeomba kazi kwenye usaili(Interview).

1. Uwezo wa kuifanya kazi kwa ubora zaidi kuliko wengine wanayoiomba.

2.Elimu.

3.Ujuzi.

Ukiangalia pointi namba moja itatumika Zaidi au itaonekana tuu ndani ya barua ya maombi ya kazi(cover letter/application letter).

Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   

Yafuatayo ni ya kuzingatia unapoandika hiyo barua.

1.Mtangulize Mungu mbele.

2. Kama ni ya kiingereza basi hakiki msamiati wako uwe sahihi na unaotumia lugha nyepesi na isiyo na maneno ya kitaalamu mengi.

3. Aya ya rejea(reference) eleza umetoa wapi taarifa ya kazi husika.

4. Unapohitaji kutaja hiyo kampuni, itaje jina lake na sio kuishia kutaja kampuni. Mfano “Ningependa kufanya kazi Vodacom” hii ni safi wakati “ningependa kufanya kazi kwenye hii kampuni” hii ni mbaya.

5. Onyesha ya kwamba unapendezwa na kazi yao, Zaidi pale kama shirika husika ni NGO ya kijamii au hata serikalini.

6. Onyesha ya kwamba unafahamu malengo yao na ungependa kua mmoja wao katika kuyafanikisha.

7. Eleza kwa nini wewe unafaa zaidi kuliko wengine walioomba nafasi husika. Tumia vigezo vifuatavyo.

· Ujuzi wako

· Ari yako ya kufanya kazi

· Mapenzi binafsi kwa kampuni.

· Ikiwezekana jinsi malengo yako yanashabihiana na ya kampuni husika.

8. Tumia maneno machache na barua iwe fupi, ikiwezekana, upande mmoja tuu wa karatasi.

9. Tambua unayemwandikia ni afisa rasirimali watu, kwa hiyo chunga lugha yako isiwe ya kitaalamu sana la sivyo hatakuelewa na ataweka barua pembeni.

10. Kama unatuma barua kwa njia ya posta inapendeza na inafaa uiandike kwa mkono barua yako ya kazi na sio kutype barua hiyo labda ikiwa pale wametaka wenyewe.
           
Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   
Kwa mfano wa barua nzuri ya kuomba kazi, nitafute katika email yangu elisanteshibanda@yahoo.com

Tovuti(website) ni kurasa za kielectroniki(webpages) zinazohifadhiwa katika kompyuta server ili ziweze kupatikana kwa urahisi pindi zinapohitajika na watumiaji wengine waliopo kokote kule duniani kwa njia ya mtandao wa intaneti.
Mfano wa kurasa maarufu zaidi ni google.com na facebook.com.

Mambo yanayohitajika kuwepo kwenye tovuti.
  • ·         Utangulizi  mfupi wa biashara yako.
  • ·         Bidhaa zinazopatikana na njia ya kuzipata.
  • ·         Ubora wa bidhaa zako.
  • ·         Upekee wako kwenye soko.
  • ·         Mawasiliano ya kufika kwenye biashara yako.
  • ·         Maono ya biashara yako.

Mambo muhimu ya kuzingatia katika tovuti yako.
  1. ·         Usiweke taarifa nyeti za biashara yako kwenye tovuti maana kila mtu ataona hata adui wataona na watazitumia kukushinda kwenye biashara.
  2. ·         Usiweke taarifa nyingi kwenye tovuti, Maelezo mengi hayastahili kuwepo kwenye tovuti maana hakuna atakayesoma Maelezo hayo Zaidi yako, weka Maelezo mafupi na yenye kutosheleza.
  3. ·         Usiweke picha halisi ya eneo lako la biashara kama halina mvuto au ubora mkubwa.
  4. ·         Usitumie picha ambazo hazina uhalisia kabisa katika biashara yako au eneo ulipo, mfano kuweka wazungu wakati Wateja wako wengi ni weusi.
  5. ·         Weka taarifa fupi zile tuu zinazomchochea mtu kutaka kujua zaidi ili apige simu na kufika ofisini.
  6. ·         Fahamu Wateja wako ni watu wa aina gani ili uweze kuongea nao vizuri mfano kama ni Watu wa daraja la kati na chini kwa kipato na ni watanzania Zaidi hapo tumia lugha ya Kiswahili lakini kama watu wako ni watu wenye pesa na wamataifa mengine mengi tumia kiingereza.
  7. ·         Tumia wataalamu wazuri wa lugha ili kusiwe na makosa ya sarufi katika tovuti maana hufanya biashara yako  ionekana ya uchwara. 
Fuata hayo na mengine mengi kwa ushauri ntumie barua pepe na mimi nitakusaidia.

Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   

Karibu upate tovuti  na blogu safi kabisa, za kisasa na kwa bei nafuu sana. Kwa mawasiliano zaidi...