Field training/ mafunzo ya vitendo ni muhimu sana, kama mojawapo ya mafunzo ya degree/diploma na umuhimu wake upo katika;

  1. Kukusaidia kujua sehemu ya kubobea katika profession yako ya IT.
  2. Kupata ujuzi wa kwanza wa kuweka katika CV yako, kuna tofauti unaposema umefanya field MIcrosoft Tanzania na serikali ya Mtaa wa kwa Tumbo😜
  3. Kufahamu ujuzi gani una soko  zaidi ndani ya IT.
  4. Kukusaidia kupata connection na waajiri, na kukutanisha na IT Professionals.

Vigezo vya sehemu ya kufanya field bora.

  1. Kuwe na kitengo cha IT imara katika sehemu zifuatazo kama Networking, computers configuration and maintenance, software/web development, graphics design  au Tech Training(Universities/colleges)

Networking:

Nenda kwa makampuni ya Networks au ISP(Internet service Providers) mfano Raha Telecom, Simba Networks ila sehemu nyepesi na nzuri zaidi kupata ni TTCL.


Computer Config. and Maintenance:

Nenda kwa wauzaji na wasambazaji wa computers kwa ukubwa na kwa mafundi wa computer though hii fani haina malipo makubwa sana katika Tech. labda kuwe na tenda za kufanya haya mambo katika makampuni.

Software/Web develop.

Nenda kwenye makampuni yanayotengeneza Apps and websites mfano shule soft, Nyumbani creative, smart codes na mengine mengi.
Note.
Makampuni haya huwa na wafanyakazi wachache sana so huwa hawachukui sana trainees, na wakikuchukua huwa hawana muda wa kumfundisha mtu sana sasa ujitume kweli kujifunze huku ukiwauliza maswali ya hapa na pale.

Graphics Design:

Nenda kwenye makampuni ya habari kama TBC, ITV na TV nyingine zinazotengeneza matangazo kwa wingi hata kama ni za mtandaoni.

PLAN B

Umetafuta field umekosa kabisa, muda unakwenda na chuo kinaweza  kikakuzingua, nenda sehemu ambayo haina hata IT kabisa, 
 ila iwe na Internet ya Maana nzuri , mfano halmashauri nyingi siku hizi zina network na ziko safi,  pale utajaziwa fomu zako,  ila  tumia  muda wako na internet yao kusoma online courses  za programming na vinginevyo yaani utatoka bomba kuliko hata hao waliopata field microsoft....na utaweza kufanya kazi za mtandaoni(Freelancing) kabla hata ya kumaliza chuo...na unaweza anzisha kampuni yako baadaye ni wewe tuu.


USHAURI WANGU KUPITIA MAPITO YANGU BINAFSI

Kwa kipindi tulicho nacho sasa, PLAN B ni bora zaidi, makazini na makampuni makubwa mengi hayakupi nafasi za kujifunza sana, na pia ajira nyingi siku hizi ni za freelancing kuna vijana wanapata mamilioni kwa mwezi kuwashinda hata wale waliojariwa.
chagua kipi bora ila unaweza fanya vyote pia plan A na Plan B ila tuu ujitoe kweli kweli.


SEHEMU ZISIZOFAA KWENDA FIELD

Benki:

Kwa sababu ya usalama hawatakuruhusu katika mifumo yako so utabakia kuwa mapokezi na hiyo inaboa sana.

Mashuleni:
utaishia kutengeneza kompyuta ya mwalimu mkuu na lab ambayo ina  kompyuta hovyo sana.

Serikali za mtaa.

Sehemu ambazo kuna LAN na INTERNET nenda kafanye plan B, ila tuu pakiwa haposomeki usiende.

Sehemu zote zenye matumizi madogo ya Tech usiende.

Tumia  muda vizuri, wahi na kuwa mwepesi wa kujifunza na tengeneza connection ukiwa huko, unaweza ukaitwa tena kama ni private.

Kama una maswali zaidi nitumie katika email yangu ya  elisanteshibanda@yahoo.com