Mambo 5 muhimu ya kuzingatia unaponunua kompyuta mpya 2024.


Fuatilia kwa umakini mambo haya ili usije ukapoteza hela yako bure au kupata kompyuta isiyolingana na mahitaji yako.

MATUMIZI

Kwa matumizi ya kiofisi ,kama kuandika (microsoft word)  na kutumia spreadsheet(excel),intaneti na kusoma barua pepe unapaswa kununua kompyuta yenye uwezo mdogo hadi yenye uwezo wa kati:
vipimo:
RAM=2GB-4GB
Processor= 1.8-2.0 Ghz 
Architecture= 32Bit.


Kwa matumizi ya kujiliwaza(Entertainment) mfano kucheza michezo kama mpira(FIFA) magari,au kwa matumizi ya kudesign hii unahitaji kompyuta yenye uwezo mkubwa:
Vipimo:
RAM=4GB-8GB
Processor=2.5Ghz--> Nakuendelea, Dual-->na Kuendelea
Architecture= 64Bit.


VIFAA VINAVYOAMBATANA NA KOMPYUTA.

Ni muhimu sana kuhakikisha vifaa kama adapter vinavyokuja na kompyuta kama vimetengenezwa na mtengenezaji halisi wa kompyuta hiyo na ni original! Unapokuwa unapewa Vifaa hivyo hakiki kama vimeandikwa jina la mtengenezaji wa kompyuta hiyo mfano HP na adapter yake iandikwe HP na hata muonekano wake uwe unaridhisha machoni ya kwamba ni original ukijimuisha uzito wake pia. 


HAKIKI UKUBWA WA HARD DRIVE, RAM NA PROCESSOR .

hakikisha kompyuta inapowashwa inaonesha ukubwa halisi kama ulivyoandikwa kwenye vitabu vyake au kama mlivyokubaliana na muuzaji. Ili usidanganywe, inapowashwa kompyuta pale kwenye desktop right-click computer halafu chagua properties hapo utaweza kuona ukubwa wa vitu hivyo.


NENDA MAHALI PANAPO AMINIKA KWA UUZAJI WA VITU ORIGINAL.

Usijaribu kununua kompyuta maeneo ambayo yamezoeleka kwa wizi kwa maana , kuna mambo mengi ambayo mtu mwingine hawezi kukagua zaidi ya mtaalamu wa Tehama. Na kama utahitajika kununua huko tafadhali nenda na mtaalamu wa tehama.

HAKIKI THIBITISHO(WARRANTY) YA KOMPYUTA HIYO.

Kama kompyuta ni mpya ni lazima na muhimu iwe na thibitisho hata la kuanzia mwaka mmoja(1) na ikipungua sana napo haishauriwi mwisho miezi sita(6).


USIJARIBU KUNUNUA KOMPYUTA MPYA KUTOKA KWA MTU AU KOMPYUTA YENYE UWEZO MKUBWA KWA GHARAMA NDOGO.

Kuwa makini kizuri chajiuza kibaya chajitembeza. Unapoona kompyuta yenye uwezo mkubwa kwa gharama ndogo usinunue mpaka umeipeleka kwa mtaalamu aihakiki kama ni nzima.

Imeandaliwa na 
Elisante Shibanda.
 

2 comments:

  1. Maandiko yako yamenisaidia
    Lakini Mimi bado na shida kwenye ufahamu wa processor intel core maana naona1.8,2.0,2.5Ghz pia kuna dual sihelewi kabisa na architecture inasaidia nini mwisho kabisa Intel core i3 naweza tumia kwa games?

    ReplyDelete
  2. Maandiko yako yamenisaidia
    Lakini Mimi bado na shida kwenye ufahamu wa processor intel core maana naona1.8,2.0,2.5Ghz pia kuna dual sihelewi kabisa na architecture inasaidia nini mwisho kabisa Intel core i3 naweza tumia kwa games?

    ReplyDelete