Vyuo Bora vya kujifunza IT(Information Technology) Tanzania, 2024




Katika Upande wa Elimu ya juu, ni vizuri kupata ushauri bora kabla hujaenda kujiunga na chuo chochote.
Kwa maana uamuzi wako huo utaamua mambo yafuatayo katika maisha yako...




JINSI YA KUSOMA IT: Mwongozo kwa Wanafunzi Waliofeli Form Four, 2024

KIPATO CHAKO BINAFSI
Kozi hii ya IT, Kichwa chako ni ofisi yako, kwa hiyo kama utapata elimu mbovu,utapoteza uwezo wako wa kujiajiri na unaweza ishia pabaya.


AJIRA
Interviews za kazi hizi za IT, sio nyepesi, na kwa hali hii itakushinda kushindana na watu waliofundishwa vyema na kuwa wazuri katika maeneo muhimu ya Information Technology.

MCHANGO WAKO KWA TAIFA
Kozi hii au profession hiii au kazi hii ya IT ina mzigo mkubwa katika taifa hili changa kiteknolojia.
Kuna matatizo katika jamii ambayo yanahitaji kutatuliwa kidigitali,kwa sababu hii kama utakuwa na elimu mbovu,

utakuwa mmoja wa walalamikaji badala ya wabunifu na watatuaji matatizo.



VIGEZO VYA CHUO BORA KATIKA IT
Vifuatavyo ni mojawapo ya vigezo muhimu,ila vinaweza vikawepo vingine zaidi.




UBUNIFU UNAOFANYA KAZI
katika mavyuo mengi sikatai kama kuna ubunifu ila mwingi unaishia kwenye makaratasi ya chuo na kutupwa stoo(store). 
Ubunifu hujulikana kwa project ambazo zinavuka mipaka ya chuo na kuifikia jamii.

UFUATILIAJI WA CHUO KWA PROJECT ZA WANAFUNZI.
Kuna mavyuo yanaongoza kwa kutupa store project za wanafunzi lakini pia kutokuchukulia kwa umakini project zinazofanywa na wanafunzi, kiasi kwamba wanafunzi wako huru kuforge project zao na chuo kuzipokea tuu kwa kutokujali ya kwamba hii project imefanyika au laa. 

ASILIMIA YA VITENDO KATIKA ELIMU INAYOTOLEWA.
Ni muhimu kwa chuo kuwa na asilimia kubwa sana ya vitendo kuliko nadharia

VIFAA VYA KUJIFUNZIA IT
Ni muhimu kusoma  kwenye chuo chenye vifaa vya kutosha ili ujue haswa nini kinaendelea makazini ila ni kwa  asilimia ndogo hii pointi ina umuhimu maana IT inakuwa kwa kasi na Vyuo vya haviwezi kuwa na vifaa vya kisasa kila wakati.


"Chuo kinaweza kumtengeneza mhitimu wa IT,ila ni jukumu la mwanafunzi binafsi akiwa chuoni, kutoka chuoni kama mtaalamu,na sio mhitimu pekee kwa maana wahitimu hupata shida sana kutafuta ajira wakati wataalamu hutafutwa na ajira na pia hujiajiri."




Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na magroup ya Whatsapp ya MAXPO Tanzania  Maximize your potential   


VIFUATAVYO NI VYUO BORA KUJIFUNZA IT  TANZANIA.
 1. Dar es salaam Institute of Technology (DIT)

2. St. Joseph University in Tanzania.

3.University of Dar es Salaam.

4. University of Dodoma



Kwa kumalizia, vyuo vipo vingi na wanafunzi wanazidiana uwezo 
kwa hiyo inawezekana ubunifu wa hali ya juu ukatokea kwenye chuo ambacho hakipo hata kwenye list hii, 
na pia vyuo vingine vinaweza vikaboresha ufundishaji wake na kuvipiku vyuo vilivyopo sasa.

Na la muhimu college za IT zipo nyingi na kwenye mikoa mingi, kwa hiyo kukosa nafasi kwenye vyuo hapo juu haimaanishi IT yako umeitupa, ila ina maana wewe ndio wa kukin'garisha chuo ulichokuwepo.




Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na magroup ya Whatsapp ya MAXPO Tanzania Maximize your potential  


 





28 comments:

  1. Thanks,, nimependa advices,na
    blog yko keep it up

    ReplyDelete
  2. Kaka samahani Nina mdogo wangu nataka kujua chuo kizur kwa masomo ya it na yeye yupo mbeya aiport ya zamani ameitimu 4 mwaka jana na ameoata Chet Ila nataka sifa zinazo takiwa huko chuon na ghalama zao kulingana na ushauri wako na Kama kipo mbeya nambie kuepkana na ghalama za hapa na pale no 0713472938 or 0742151450 naitwa Jackson

    ReplyDelete
  3. Napenda kuuliza je ni kozi ipi nzuri ya IT itakayo maliza kusoma alafu utume maombi kwenda jkt baada ya hapo jwtz Kama mtu uliesoma IT?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nilikuwa nauliza kuwa ni ajira gani ambazo hupatikana baada ya course hii kwa wahitimu wake

      Delete
  4. Elimu Yako unayoitoa ni nzuri, tafadhari endelea kufanya hivyo!

    ReplyDelete
  5. Sorry Kwa Mimi ambae napenda kusomea IT na IPO kwenye damu unanishauri vp

    ReplyDelete
  6. Mimi nahitaji kusoma IT hasa chuo gani kizuri kwa dar es salaam na sifa za kupokelewa kwenye hicho chuo naomba jibu no.0623518982

    ReplyDelete
  7. Inamaana kilimanjaro Institute kimezidiwa na vyuo ivyoulivyovitaja?? Maana yake mtaani huku naskiaga sana wakikitaja hiko chuo lakini sijakiona kwenye orodha..Samahani kakayangu naomba unijibu kwa sababu mimi meenyewe sijui pia kwahiyo naomba ushauri wako.

    ReplyDelete
  8. Kaka mm Nina D2 na Ç1 et naeza soma IT nko shnyanga ila nataka chuo kilichopo mwanza he unanshauli nkasomee chuo gan na hizo pass zinaeza nluhusu kusoma hyo koz

    ReplyDelete
  9. Mi nauliza ni vigezo gani anavotakiwa kua navyo mtu aliehitimu form4 kujiunga na masomo ya IT

    ReplyDelete
  10. Chuo bora cha it cha serkali being kdogo n nzur n kp

    ReplyDelete
  11. Ningependa kufahamishwa sifa za kujiunga na vyuo hivyo

    ReplyDelete
  12. Ushauri nzuri. Samahani naomba uliza nimesoma chuo cha mipango adi diploma je naweza transfer adi chuo chenu?

    ReplyDelete
  13. sant broooo wang mm n mwanafunzi wa kidato cha nne mbeya secondary apenda kusoma sana it na ipo kweny damu naomb ushaur ni jinsi gan ya kuwa it mzur na niweze kujiajili

    ReplyDelete
  14. Bro minaipenda sana IT ndo nimemaliza form4 Nina three ya 23 nimepangiwa chuo cha ustawi was jamii lakini naipenda IT kinoma ushaur wako Niko pwani

    ReplyDelete
  15. Mimi ni mwalimu Nina degree ya masomo ya sanaa yaan geoghaphy na kiswahili,nauliza kwa wataalamu, Kuna ubaya wowote wa kuwa na degree ya IT Au I.C.T? Kma haupo nisaidien vyuo vizuri na Ada zake

    ReplyDelete
  16. Ndugu ningeomba kujua vyuo Bora vya it Na sifa zake pamoja Na ada zake nisaidie bro 0627347511

    ReplyDelete
  17. Habari zenu, nipo hapa kushuhudia, jinsi nilivyo kuwa mwanamitindo tajiri na maarufu duniani mwenye mafanikio makubwa, nimekuwa nikipitia magumu miaka nenda rudi, tangu nilipofiwa na wazazi wangu wote wawili, sikuweza kuendelea zaidi na mshikaji wangu kutokana na Suluhu la kifedha basi, hadi miezi mitano iliyopita, nilimaanisha rafiki ambaye aliniingiza kwenye familia ya freemason, mwanzoni niliogopa kujiunga, kwa sababu nimesoma habari nyingi za uongo kwenye mtandao kuhusu familia ya freemasonry, na ambayo sasa ninaijua. hiyo sio kweli, zote zilikuwa habari za uongo, na napenda kutumia fursa hii kusema asante sana kwa familia ya freemason, ndugu wote wa familia hii, nawashukuru sana kwa support mnayonipa, na kwa waliodhani familia ya freemasonry ni mbaya, haijui sheria na kanuni za huyu jamaa, tafadhali acha kuhukumu ulikuwa hujui, na acha kusambaza habari za uongo, kama una nia ya kuwa mwanachama ufurahie. faida za familia ya freemasonry, contact off anuani icial hapa chini kwa taarifa zaidi.

    WhatsApp; +31 687 329 133
    Barua pepe; info.masonic.oregon@email.cz
    Barua pepe; info.masonic.oregon@gmail.com
    Au soma zaidi kuhusu sisi kwenye kiungo cha ukurasa wa Facebook; https://web.facebook.com/infomasonicoregon

    ReplyDelete