Kufeli Form Four Sio Mwisho wa Dunia: Njia za Kusoma IT
Kufeli Form Four haimaanishi mwisho wa ndoto zako. Watu wengi waliofanikiwa, ikiwa ni pamoja na maprofesa na wafanyabiashara wakubwa, walipitia changamoto sawa na zako. Katika makala hii, tutaelezea njia ambazo unaweza kutumia kuanza kusoma IT, hata kama ulifeli mitihani ya Form Four.
Njia ya Kwanza: Kurudia Form Four
Moja ya njia za moja kwa moja ni kurudia Form Four na kupata ufaulu unaohitajika. Baada ya kupita, unaweza kujiunga na chuo chochote cha IT na kusoma IT Certificate.
Njia ya Pili: Commercial Secretarial Course Kupitia Chuo cha utumishi wa Umma.
Kozi ya Commercial Secretarial inaweza kukupa msingi imara katika ujuzi wa ofisi. Baada ya kumaliza kozi, unaweza kushiriki mtihani wa VETA na kupata cheti cha NATIONAL BUSINESS CERTIFICATE STAGE 1. Cheti hiki kinaweza kukusaidia kujiunga na programu za IT katika vyuo mbalimbali.
Njia Nyingine:
- VETA: VETA hutoa kozi za IT za viwango tofauti. Wasiliana nao kwa maelezo zaidi.
- UDSM: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) pia hutoa programu za IT.
- Kozi za Mtandaoni: Platforms kama Coursera, edX, na Udemy hutoa kozi za IT za mtandaoni.
- Ujuzi wa Vitendo: Pamoja na masomo ya kitheori, jifunze ujuzi wa vitendo kama coding na design.
Vidokezo vya Ziada:
- Utafiti: Fanya utafiti wa kina kuhusu vyuo vya IT, mahitaji ya uandikishaji, na gharama za masomo.
- Mikopo na Masomo: Tazama fursa za mikopo ya wanafunzi na masomo ya udhamini.
- Networking: Jenga mtandao wa watu katika sekta ya IT ili kupata ushauri na fursa.
- Motisha: Imani na kujitolea ni muhimu katika kufikia malengo yako.
Kumbuka: Kufeli sio mwisho wa dunia. Kwa bidii, ubunifu, na kujitolea, unaweza kufikia malengo yako katika ulimwengu wa IT.
Article inayofuata: Jinsi ya kusoma IT kwa gharama nafuu kabisa.
Cha kushangaza Takwimu zinasema ya kwamba, wanaongoza kukosa ajira ni waliosoma Computer Science.
Hizi ni mojawapo ya sababu zinazowafanya wahitimu wa computer science wengi kuhangaika kukosa ajira...na kuifanya hii kozi kuwa imepitwa na wakati kwa sasa.
Kozi haiandai wahitimu wake kwa soko la ajira.
Mifumo ya kizamani ya ufundishaji.
Kutokusoma vitu kwa undani.
Gharama kubwa
Imepoteza umuhimu wake.
Tunasonga mbele vipi...
SKILLS:
User Experience (UX) Design, Digital Marketing, Artificial Intelligence (AI) & Machine Learning (ML), App Development , Cybersecurity...E.T.C
CODING SKILLS:
JavaScript, Kotlin, Python, Rust and C/C++
Tunavyosoma Chuoni, mavyuo hujitahidi kukupa uwezo kutambua maeneo mengi iwezekanavyo ya Information Technology, na wanafanya hivyo kwa dhumuni zuri la kukuhakikishia unaelewa kwa asilimia kubwa kitu gani kinaendelea katika maeneo mbali mbali ya IT.
Tatizo linakuja pale unapochukua hiyo elimu ambayo huwa ni fupi(shallow), kutoka nayo huku njee ukiamini ya kwamba umepata elimu, na hapo ndio soko la ajira linakuona hufai na hauna chochote cha maana cha kuwasaidia.
Mfano:
Unaposoma Network ukamaliza ukirudi kwenye soko la ajira, wewe bado sio mtaalamu wa Network, unahitaji vyeti vya CISCO, SERVERS, ETHICAL HACKING etc hapo ndio utapata kipaumbele na utakuwa na practical knowledge ya Networking katika IT.
Suluhisho:
- Wakati ukiwa Chuoni, soma hivyo vyeti vingine mtandaoni kama nivyoviainisha hapo juu, na zaidi katika kila maeneo vingine ni bure, vingine vitakugharimu.
Note:
Chagua wapi kwa kubobea na sio usome coding, network umo, hapana...chagua sehemu then bobea kuelekea huko...na gharama zitapoa pia.
- Hudhuria semina na michuano ya IT Tech world mfano hackathon ambapo watu wa IT zaidi wanafunzi hukutanika nakutengeneza Apps kwa muda mfupi huko utajifunza mengi...mara ya mwisho CRDB na makampuni mengi yalijitokeza kudhamini tukio mojawapo hapa Dar es salaam.
- Jiunge na TECH Hubs zenye Uhai maana huko utapata ma IT wengi mnaweza hata kukutana na mkapata wazo la kufanya jambo fulani la IT kuliko kukaa mtaani na wabeba zege wanaojiona wao ni bora kuliko wewe.
- Kama utafanikiwa tafuta field kwenye kampuni za IT, ila ukishindwa achana nayo maana na wenyewe huwa ni wagumu sana kutoa field kwa wanafunzi.
- Kikubwa zaidi kumbuka chuo kinakupa 25% tuu ya maarifa, shughulika kupata mengine kabla hujatoka uanze kukataliwa kila mahali.
- Jiunge na online communities za Tech, mfano mzuri ni GitHub huko unaweza changia hata open source software na zaidi...na mengine mengi.
Katika kozi ambazo zinaongoza kwa watu wake kutokuwa na ajira ni Computer science, Information Technology and nyinginezo za Technology. Ni ajabu lkni ukilinganisha na nature ya ulimwengu wa sasa, ila ndio uhalisia.
Jambo kubwa linalofanya watu hawa kukosa ajira ni kosa ambalo linafanya mavyuoni bila kutambua, vyuo vinajikita katika kuwa expose(funulia) katika ulimwengu mzima wa IT nakusahau kwa fanya wachague mapema sehemu gani wanatakiwa wajikite kwa isiyopungua miaka 2 ya mwisho ya masomo yao.
Kwa kutambua hilo nimejaribu kuchambua maeneo kadhaa unaposoma chuo unahitaji kujikita kulingana na soko halisi huku njee.
Cyber Technology
Hili eneo linahusika na ulimwengu wa Mtandao wa Internet na Network, jinsi gani connection zinafanyika kati ya watu na vifaa na programu mbali mbali, kwa ufupi ukijikita katika cyber technology utajikita zaidi katika ku maintain security ya mifumo isidukuliwe na kulinda data za watu katika mifumo hiyo, hawa watu ni muhimu sana katika kila organization inayotumia mifumo na yenye data nyeti sana mfano serikali, benki na maeneo yanayofanya tafiti na sasa hata chaguzi...
Njia.
Kwanza uwe katika kozi kama computer science au IT, halafu unatakiwa usomee vyeti vya ujuzi maalumu mfano CompTIA Security+ na Certified Ethical Hacker (CEH) na pia ujichanganye katika mashindano mbali mbali ya mambo hayo yanayotokea ili kujinoa.
Ila vyovyote ufanyavyo unatakiwa uji-update katika Artificial Intelligence maana inachukua nafasi kubwa sana, marobot ndio yanahack siku hizi, na Ai ndio ina ulinzi mkali kuliko watu, so unaweza soma ukashangaa anaajiriwa robot anaitwa Junior kutoka uswisi π
KAZI
Peleka CV yako maeneo kama Benki, Nafasi zikitoka serikalini zaidi TCRA, na makampuni ya mitandao ya simu
Application Development
Bila ubishi tunahitaji Apps siku hzi kwa hali na mali na bei ya App moja sasa, unaweza ukajisikia kizungu zungu...kwa sababu wataalamu ni wachache sana na bado tuna mahitaji mengi sana ya App kwa ajili ya mazingira yetu ya Africa, Tanzania.
Njia
Ngoma iko wazi, tutorial lundo mtandaoni chuoni usimuone Prof wa watu yeye ni mkufunzi wewe ndio mhusika haswa na Tech inabadilika kwa speed kubwa sana, ingia website za matorrent badala ya kudownlaod movies download udemy tutorials katika Lugha za Apps kama Javascript na mifumo mbali mbali...YOutube kuna professional watakueleza 1 mpka 10, pa kuanza hadi pa kumaliza.
Server/Computer troubleshooting, maintenance and installation.
Hapa kuna wataalamu wengi ila wamejikita zaidi katika maeneo ya kawaida sana, yaani kutengeneza computer za kawaida tuu, ila katika upande wa servers ni wachache sana, kila kampuni kubwa inahitaji server kuweza kutumia programu za ERP, na nyinginezo nyingi tuu...Lkni pia kutokana na kuboreka kwa mtandao wa Internet, makampuni mengi yamekuwa yakitumia server za njee ya nchi maana kutunza server computer imekuwa gharama sana kuliko kulipa kwa wenye nazo.
Njia
somea Microsoft Certified Solutions Expert (MCSE), CompTIA Server+, Red Hat Certified Engineer (RHCE) na VMware Certified Professional-Data Center Virtualization (VCP-DCV), masomo haya yanapatikana mtandaoni na utabidi ulipie, ili uwe mzuri katika IT ni lazima uingie gharama no shortcut, vyeti hivyo vitakuitisha kwenye interview haraka sana.
Software Sales, maintenance and installations.
Huku unajikita zaidi katika kuuza Programu za kitaalamu, za mifumo mbali mbali ya kuendesha makampuni au taasisi mfano hospital management, school management, church management N.K
Njia
Unahitaji unavyosoma uzitatute hizi programu uelewe zinavyofanya kazi na uanze kuziuza, au wewe utengengeneze za kwako. soko lipo kubwa , sehemu nyinginr unahitaji kutoa elimu kabla ya kuuza ila zinahitajika sana hadi sasa.
Network Installations and Maintenance and security.
Eneo hili linahusika na kufunga mtandao kwa njia ya nyaya na bila wire, pamoja na maendeleo makubwa ya teknolojia, badi tunahitaji waya kwa sababu zina ulinzi mzuri wa kuto kutoa nafasi ya kudukuliwa, na pia nimejumuisha kufunga mifumo ya camera za ulinzi kwenye majengo.
Njia
Nenda kasome vyeti vya cisco na pia kaa na wataalamu wa mifumo ya security camera, kama hakuna vyeti hata ujuzi wenyewe unaweza andika katika CV yako ikawa safi sana, na ukapata ajira au kipato haraka.
Computer Rent and sales
Kama una uwezo wa kupata mtaji, fungua duka la kuuza computers au laptops. siku hizi taasisi nyingi zinapenda kukodi computer kwa muda maalumu na kukulipa, kama ukiwa nazo basi utafaidika, anza na kuuza kwanza baadaye ukipata channel nzuri utakodisha, nunua kutoka China maana laptops zimekuwa bei ndgo sana siku hizi.
Professional Software Training.
Sizingumzi kufundisha computer hapa, nazungumzia kufundisha hizi programu za kuendesha taasisi na makampuni mfano za wahasibu, mahospitali, mashule na kadhalika, kuna zile maarufu ukizifahamu zitakufanya uitwe na makampuni kwenda kuziweka, kuziuza na hata kufundisha wafanyakazi wao.
Njia
Jifunze mtandaoni au kama upo kweye sekta mabayo imekuvutia tengeneza mfumo mzuri na uuze kama kuna uhitaji eneo hilo.
Graphics Design
Sanaa ya matangazo ni muhimu siku hzi kwa ukuaji wa biashara, ila imekuwa nyepesi sana maana programu zimekuwa nyepesi kutumia ya kwamba watu wengi wanafanya wao wenyewe. Ila kuna matangazo yanahitaji skills zaidi kama ya Video so jikite huko, nenda mbali zaidi kwenye 3D na motion graphics.
Njia
Youtube ina mafunzo ya kila aina ya programu, tafute mafunzo muhimu ya programu mama kama Adobe Illustrator, Photoshop na Indesign, then hamia katika After effects, Maya, cinema4D na kuendelea kazi zipo nyingi mitandao ya UPwork.
KUJITENGA
KUWEZA KUFIKIRI HARAKA
KUVUNJA MAHUSIANO
PESA NYINGI
MUDA
MATATIZO YA KIAFYA
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA:
- Kupata wazo jipya kabisa ambalo halijawahi kufanyika, haiwezekani kwa 78%.
- Programu au App inayofanya kazi na kupendwa na watu Ulaya, inaweza isifanye kazi vizuri Africa..sababu ni Tamaduni, miundo mbinu..etc.
- Sio kila wazo la Tech, haijalishi ni zuri kiasi gani, ni muda wake, mengine watu wanaweza wasilipokee au wasilipende kwa sababu tuu ya muda bado.
- Mawazo mazuri sio lazima yawe "complicated"magumu yaani hata tech yake, coding lundo...Hell No π€ Issue ya muhimu ni moja tuu, kurahisisha utendaji wa kazi, na tumia technolojia ya bure kwa nafasi kubwa sana...
- Kuchukua wazo la mtu na kuliboresha ni ubunifu pia, ila vizuri uombe kibali na pia uliboreshe kwa viwango vya hali ya juu isije ikaonekana umecopy tuu.
- Ukitaka baadaye uwe unafanya software development, hakikisha kwenye project unajifunza ku code, yaani wewe ndio uwe mwandika code, usifanye uhuni wa kurukia rukia na kuwaachia wengine.
- Usipende shortcuts katika coding, itakufanya ushidwe kudevelop uwezo mzuri wa kuandika programu baadaye.
- Usiogope kupresent wazo, kwa sababu litatumia lugha nyingi au hujui utatumia lugha ghani ya computer kulitimiza, niamini utapata tuu lugha za kutumia, na utajifunza vizuri na utaweza bila shida yeyote...nimepita hapo naelewa pressure yake unaweza unahisi unataka kuaga dunia..π
- Sio lazima uwe programmer kama ni kiongozi mzuri unaweza tengeneza Team na ukasonga mbeleπ ila Programmer akisusa utajuta.π₯
- Mawazo mazuri ya Project ni matatizo ya kila siku, katika maeneo ya kazi, katika jamii..mfano tunaona Uber ni mtu aliona matax yanazingua..etc.