Tofauti kati ya IT na ICT
Kwa hiyo hili wimbi la ma Vyuo kubadili majina ya course kutoka IT kwenda ICT lisikutishe, ujue tuu hiyo term ya ICT inatumika zaidi katika Elimu, ila ukimaliza wewe ni IT kama kawaida.
Maarifa Thabiti ya Ulimwengu wa Teknolojia ya Kompyuta.
Kwa hiyo hili wimbi la ma Vyuo kubadili majina ya course kutoka IT kwenda ICT lisikutishe, ujue tuu hiyo term ya ICT inatumika zaidi katika Elimu, ila ukimaliza wewe ni IT kama kawaida.
Self employing - unaweza kujiajiri
Marketable - Ajira nyingi
Less marketable - Ajira chache
Poorly marketable - Ajira hakuna
Business Information system - Marketable
Computer and information systems security - Less marketable(better in masters
computer engineering - Poorly marketable
computer science - Self employing and marketable
Geoinformatics - Less marketable but needed.
ICT mediated content development - New and poorly marketable
information systems - Marketable
Multimedia Technology and animation - Self employing course, marketable in Medias
software engineering - Marketable and self employing
Telecommunication Engineering - Marketable
Computer and business management - Marketable and self employing.
computer networks - Less marketable( uwanda mdogo)
Computer system administration - Marketable like IT
Graphics Design and web technology - Self employing
information and telecommunication technology - Marketable
information technology - Marketable
Rekebisha haya ili CV yako in'gae na upate kuitwa kwenye interviews/usaili.
Daftari/kitabu
Usiandike kitabu na experience ya kuandika huna, acha iwe page 1 au 2 tuu inatosha, kwa nini? Mfano wewe ndio afisa rasilimali watu ina CV 300 mezani utasoma CV ndefu?
Usiandike majukumu yako uliyokuwa unafanya awali.
Yeah naona kuna mtu alikuwa anakula baada ya kusoma hiyo anatafuna taratibu sasa, NDIO andika mafanikio na sio majukumu, mfano wewe ni mwalimu usiandike nilikuwa nafundisha, natunga mitihani, na kusahihisha instead andika nimefanikiwa kufundisha wanafunzi 500 geography na katika hao walifaulu 400, rafiki unaitwa haraaakaaa kuanza kazi.
kuweka vipengelea ambavyo havihusiani na kazi unayoitiwa.
CV sio ukishatengeneza basi ndio imetoka hapana, ukiitwa kwenye kazi ya jamii CV yako ioneshe sehemu ulijitolea hata kwenye vikundi vya dini, kuonyesha uongozi, ila ukiitwa kazi ya ofisini, toa vipengele vya vikundi vya kijamii unavyojitolea maana utaonekana uko busy na kazi yao unaweza lipua au ukawa na visingizio vingi vya kutoka kazini.
Hobbies
Kama bado unaweka hizi acha huu uhuni.
Referees.
Usiweke mtu ambaye hajawahi kuwa supervisor wako au boss wako, kama unatoka chuo si ulienda field? kawatafute huko, na utafute lecturer hata mmoja, chondechonde usimuweke ndugu yako.
BONUS
Hebu nenda katafute muundo mzuri wa CV mambo ya CV Kuonekana kama CV ya Chifu Mashuposhupo acha...tembelea cvmkr.com itakusaidia.
Kwa ushauri na mawasiliano tembelea rainstech.com wasiliana nasi kupitia live chats
Ili uweze kufanya kazi mtandaoni unahitaji kuwa na ujuzi ambao mtu anaweza kuutumia ujuzi wako bila kuonana na wewe, na pia uwe na ujuzi wa lugha ya kiingereza vizuri ikiwezekana na lugha nyingine kubwa kama kifaransa.
Na hapo ndio unaona ujuzi wa IT huongoza katika hili lakini pia hata secretarial ila hizi kuna program nyingi ambazo zinafanya kazi zaidi ya secretary.
ujuzi au skills ambazo huhitajika mara kwa mara na watu haujiriwa na kulipwa mtandaoni ni kama ziifuatazo:
Advanced microsoft office Skills( Excel, Word, Powerpoint, access)
Application development(Android, IOS, web applications)
Web design
Graphics Design( artworks, branding, video editing, adverts etc)
Mitandao inayotoa ajira hizi, inahitaji vitambulisho na sometimes ukitaka kuwa member basi utagharamia membership kama 10 dollars inategemea ila huwa ni bure, na katika kila malipo yako utakwatwa hela hapo.
na mingineyo ila hiyo ndio naona vijana wa Tanzania hapa hapa wanalipwa hela.
.
IT(Information Technology) ni kozi nzuri sana kwa vijana na pia ni mojawapo ya sekta ambayo makampuni yaliyowekeza humo yanatengeneza pesa nyingi sana.
Na tunapokwenda IT Imekuwa ikifuta nafasi za kazi nyingi sana kwa kompyuta kuzifanya hizo kazi, mfano;
Assembly line & factory workers
Phone Operators and receptionists
Cashiers
Bank tellers and clerks
Pilots
Journalists and reporters
Stock traders
Postal workers
Travel agents
Accountants
Na kadhalika ni kazi nyingi zinapotea,hatuwezi maliza ila pia IT inatengeneza ajira zake nyingi sana, nyingine hazihitaji hata uajiriwe na mtu.
NJIA YA SHULE KUPITIA ADVANCE HIGH SCHOOL
Kuanza kama ni mwanafunzi wa sekondari hakikisha unasoma masomo ya science na biashara na uendelee advance na masomo hayo hlafu ukifika chuo chagua kozi za IT.
NJIA YA SHULE KUPITIA CHUO
Soma mpaka form four masomo ya science na biashara, halafu chukua certificate ya IT, halafu diploma halafu degree. Vyuo bora ni University of Dodoma, St.Joseph University in Tanzania, Dar es salaam Institute of Technology,College of Information and Communication Technologies (CoICT) - University of Dar es salaam na University of Dar es salaam Computing centre.
NJIA YA KUTOKEA CHUO NA KUENDELEA.
Soma kozi yeyote halafu ukimaliza unaweza nenda kwenye vyuo vya IT, kama unaweza soma degree nyingine ya IT au nenda kwenye vyuo vinavyotoa ujuzi wa IT na ujifunze unaotaka.
Mfano Degree ya Uchumi ila unapenda IT. basi nenda kwenye chuo kinachotoa IT, tafuta Ujuzi unaoutaka mfano:
Application Development
Networking(Inategemea vigezo)
Cyber security(Inategemea vigezo)
Computer TIA
Web development
Graphics Design.
Accounting package Training.
Halafu tafuta college inayotoa ujuzi husika katika vyuo nilivyoviorodhosha hapo juu.
Mara nyingi kozi nyingine hapo huwa hazifundiswi mavyuoni mfano cyber security au App development kwa hizi kozi inabidi ufanye paid online training katika mitandao kama Udemy, Tutsplus etc.
NJIA YA BURE
Kama unapenda IT na hauna hela zaidi ya hela ya bundle, basi chagua kozi unayotaka kusoma, halafu nenda kwa wanao download movies mtandaoni waambia wakusaidie kukutafutia hizo online courses then wakuwekee kwenye hard drive ili ukajifunze wemyewe privately, na watu wengi wamejifunza kwa njia hii, ila hautapata cheti chochote zaidi ya ujuzi.
Enter your email address below to subscribe to our newsletter.