Rekebisha haya ili CV yako in'gae na upate kuitwa kwenye interviews/usaili.
Daftari/kitabu
Usiandike kitabu na experience ya kuandika huna, acha iwe page 1 au 2 tuu inatosha, kwa nini? Mfano wewe ndio afisa rasilimali watu ina CV 300 mezani utasoma CV ndefu?
Usiandike majukumu yako uliyokuwa unafanya awali.
Yeah naona kuna mtu alikuwa anakula baada ya kusoma hiyo anatafuna taratibu sasa, NDIO andika mafanikio na sio majukumu, mfano wewe ni mwalimu usiandike nilikuwa nafundisha, natunga mitihani, na kusahihisha instead andika nimefanikiwa kufundisha wanafunzi 500 geography na katika hao walifaulu 400, rafiki unaitwa haraaakaaa kuanza kazi.
kuweka vipengelea ambavyo havihusiani na kazi unayoitiwa.
CV sio ukishatengeneza basi ndio imetoka hapana, ukiitwa kwenye kazi ya jamii CV yako ioneshe sehemu ulijitolea hata kwenye vikundi vya dini, kuonyesha uongozi, ila ukiitwa kazi ya ofisini, toa vipengele vya vikundi vya kijamii unavyojitolea maana utaonekana uko busy na kazi yao unaweza lipua au ukawa na visingizio vingi vya kutoka kazini.
Hobbies
Kama bado unaweka hizi acha huu uhuni.
Referees.
Usiweke mtu ambaye hajawahi kuwa supervisor wako au boss wako, kama unatoka chuo si ulienda field? kawatafute huko, na utafute lecturer hata mmoja, chondechonde usimuweke ndugu yako.
BONUS
Hebu nenda katafute muundo mzuri wa CV mambo ya CV Kuonekana kama CV ya Chifu Mashuposhupo acha...tembelea cvmkr.com itakusaidia.
Kwa ushauri na mawasiliano tembelea rainstech.com wasiliana nasi kupitia live chats
Thanks
ReplyDelete