Jinsi ya kuandika barua ya kuomba kazi yenye msisimko…2023



Kuomba kazi ni jambo la kawaida na ni njia mojawapo ya kufikia malengo yako. Kuna vigezo vingi ambavyo hutumika kumuita mtu aliyeomba kazi kwenye usaili(Interview).

1. Uwezo wa kuifanya kazi kwa ubora zaidi kuliko wengine wanayoiomba.

2.Elimu.

3.Ujuzi.

Ukiangalia pointi namba moja itatumika Zaidi au itaonekana tuu ndani ya barua ya maombi ya kazi(cover letter/application letter).

       


 
Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   

Yafuatayo ni ya kuzingatia unapoandika hiyo barua.


1.Mtangulize Mungu mbele.

2. Kama ni ya kiingereza basi hakiki msamiati wako uwe sahihi na unaotumia lugha nyepesi na isiyo na maneno ya kitaalamu mengi.

3. Aya ya rejea(reference) eleza umetoa wapi taarifa ya kazi husika.

4. Unapohitaji kutaja hiyo kampuni, itaje jina lake na sio kuishia kutaja kampuni. Mfano “Ningependa kufanya kazi Vodacom” hii ni safi wakati “ningependa kufanya kazi kwenye hii kampuni” hii ni mbaya.

5. Onyesha ya kwamba unapendezwa na kazi yao, Zaidi pale kama shirika husika ni NGO ya kijamii au hata serikalini.

6. Onyesha ya kwamba unafahamu malengo yao na ungependa kua mmoja wao katika kuyafanikisha.

7. Eleza kwa nini wewe unafaa zaidi kuliko wengine walioomba nafasi husika. Tumia vigezo vifuatavyo.

· Ujuzi wako

· Ari yako ya kufanya kazi

· Mapenzi binafsi kwa kampuni.

· Ikiwezekana jinsi malengo yako yanashabihiana na ya kampuni husika.

8. Tumia maneno machache na barua iwe fupi, ikiwezekana, upande mmoja tuu wa karatasi.

9. Tambua unayemwandikia ni afisa rasirimali watu, kwa hiyo chunga lugha yako isiwe ya kitaalamu sana la sivyo hatakuelewa na ataweka barua pembeni.

10. Kama unatuma barua kwa njia ya posta inapendeza na inafaa uiandike kwa mkono barua yako ya kazi na sio kutype barua hiyo labda ikiwa pale wametaka wenyewe.
           


Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   
Kwa mfano wa barua nzuri ya kuomba kazi, nitafute katika email yangu elisanteshibanda@yahoo.com

4 comments:

  1. Asant mtaalam kwa maelezo sahihi

    ReplyDelete
  2. Bro nahitaji niombee kaziya udereva wa magari madogo katika kampuni ya CCECC na Nina uzoefu wa kutoshatangu mwaka 2009 na nishafanya kazi ktk kampunitatu tofaut mpaka Sasa ikiwemo SINOHYDRO,CCECC hii ilikuwa ya RELI na YAPI MERKEZI na hv Sasa nahitaji nitumie hapo CCECC Hawa wanajenga Barbara ya mzunguko......nipangie fupi na ya kueleweka kiwepes ndugu

    ReplyDelete