Interview za mchujo ni interview za awali, ambazo hutumika kupunguza watu wengi walioomba kazi husika,

ili wabaki wachache kwa ajili ya hatua ya pili ya interview(usaili).
Interview hizi zina sifa kubwa sana ya kuvunja mioyo ya watu walioomba kazi, kwa watu wengi hujikuta wamejiandaa visivyo na kufanya vibaya.



Hebu kwanza tufahamu mambo ya kuzingatia unavyojiandaa na interview.


Muombe Mungu akusaidie kujibu kwa ufasaha, maana ni rahisi sana kujibu visivyo, pamoja ya kuwa unajua kila kitu.



Fahamu kwa undani kazi iliyotangazwa. Ni rahisi kusema, mimi nimesoma chuo kama IT, Computer science N.K na ndio maana kozi yangu imeorodhoshwa na nikaitwa, 
ila kufikiri huko sio sahihi na wengi hufeli maswali yanayohusiana na kazi hiyo. 
Fanya utafiti wa hali ya juu kwenye mtandao au kwa waliokwisha fanya teyari na uelewe.

kozi za IT Tanzania na Soko lake

Fahamu majukumu yaliyotangazwa na kazi husika na uhakikishe unayafahamu jinsi ya kuyatekeleza yote
au kama ukishidwa yote angalau ujue nini kinaendelea,     kwa maana maswali mengine hulenga humo.


Fahamu ni masomo/kozi gani yanayoendana na kazi husika,uliyoyasoma chuoni, halafu uyapitie kwa umakini.



MIUNDO YA MASWALI YA INTERVIEW(USAILI)

Muundo wa 1

Muundo huu utakutana na maswali 40 hadi 50, yanayokuwa ya kuchagua, na huwa yanagusa sehemu mbali mbali, ila zaidi sehemu zinazohusiana na kazi husika na sub course husika mojawapo huonekana kwa wingi.

Mfano:
Kazi ya Business analyst, maswali mengi asilimia 60-70 yatakuwa ya software engineering.

Jinsi ya kujiandaa:
Tafuta subcourse husika na uisome sana gusia maeneo mengine pia.

Muundo wa 2

Muundo huwa na maswali 4 hadi 5, ila maswali huwa yanalenga maeneo husika na yale ya kuzunguka.

Mfano:
System Administrator, maswali 2 yatahusiana na Networking lakini 2 mengine yawaweza kugusa database na hardware.

Jinsi ya kujiandaa:
Soma yote yanayoendana na kozi husika na course zinazoendana na hiyo course.

Muundo wa 3

Muundo huu una maswali 4 hadi 5, na maswali hugusa course husika tuu na huulizwa kwa mfumo wa maswali ya scenario.
Mfano:
System Administrator, maswali yote ni ya networking, na yanaulizwa yakitakiwa kujibiwa kitaalamu na sio kitaaluma
Namaanisha kitaalumu ujibu kama mtu mwenye ujuzi na scenario hiyo  na sio kama mtu aliyakariri kutoka kwenye kitabu. 

Jinsi ya kujiandaa:
kama una uzoefu kumbuka uzoefu wako, kama una mafunzo ya certifications yatumie ipasavyo, lakni kama huna hivyo vyote usijali jiandae vyema na sub course husika nawe utafanikiwa.

Muundo wa 4

Muundo huu huwa na maswali 4 hadi 5, ambayo hujikita zaidi kitaalamu na katika majukumu yaliyorodheshwa na tangazo la kazi.

Jinsi ya Kujiandaa:
Soma kwa umakini yale majukumu ujue jinsi ya kuyatimiliza kivitendo kila moja na kama kuna vigezo vipitie hata ujue tuu kwa mbali nini kinaendelea.

Angalizo:
Ni kawaida kabisa kumaliza mtihani huu usijue kama umefaulu au umefeli, na hali hii huifanya ionekane ngumu sana, ila kabla ya kujibu swali tafakari linahitaji nini na ujibu vizuri ukujibu juu juu uamini kuna watu watajibu kwa umakini kuliko wewe.


Hiyo ni muundo ambayo imekuwapo ila inaweza badilika muda wowote hata kesho ikaja mengine zaidi, na sijakugusia interview za awamu ya pili na za mahojiano,ila kwa hayo chukua hatua, na nikutakie interview njema.
Kwa ushauri zaidi wasiliana nami 


Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   






Imekuwa ni jambo la kawaida huku mavyuoni kutenganisha ajira na masomo, 
haswa katika vyuo vyetu hapa Tanzania, 
kiasi ambacho tumekuwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira,
 ambalo ukilatazama kwa umakini kuna uwezo fulani wahitimu wanakosa ndio maana, tatizo linakuwa kubwa mno. 
Lakini pia kuna sababu za msingi tuu ambazo ni za kiuchumi ambazo hata wahitimu hawahusiki ambazo zinakuza tatizo hili.

Kwa upande wa Information Technology na kozi zote zinazoendana na hiyo kozi, 

kuna vitu vifuatavyo ambavyo mwanafunzi akivifanya vinaweza fungua njia au 
kupanua wigo wako wa ajira kwa kiasi kikubwa sana. 


GPA/ UFAULU CHUONI

Huu ni ufaulu wako chuoni, najua ninavyozungumza hivi kwa wingine ni kama kuwaambia wanywe maji ya sumu, ila ndugu zangu hakuna jinsi, 
 GPA ina faida kwanza GPA kubwa inachangia kwa kiasi kukuitisha katika interview ya kazi,

kwa maana inaonesha una uelewa mkubwa na inaonesha kwa kiasi unaweza chapa kazi,
kama ulisoma kwa bidii kwa kiasi hicho basi unaweza ukawa na bidii hata kazini.

Lakini pia mavyuoni tunahitaji wahadhiri na kigezo kikubwa ni GPA ndio utaitwa kwenye interview za huko na hata watu wanaoomba ni wachache sana.
GPA nzuri huanzia 3.5 na kuendelea ila vyuoni ajira zake inategemea huwa inaweza anzia 3.5 wakati mwingine 3.8.


PROFESSIONAL CERTIFICATIONS/ VYETI VYA UTAALAMU.

Hivi ni vyeti vya kitaalamu yaani kubobea katika sehemu fulani, 
hivi havikupi degree au diploma, ila inapewa hadhi ya kuwa mtaalamu katika eneo moja tuu la IT mablo linaweza likawa sio kubwa. 


Mfano 
ukitaka kubobea kwenye networking lazima upitie CCNA Certifications, MCSA na kadhalika. 
Katika kazi kama za System Administrator bila vyeti kama hivi kuapply ni kazi bure na hata kama ukiitwa mitihani inaweza kukushinda kwa ugumu wake. 



SKILLS/UJUZI BINAFSI

 Katika maswala ya IT, swali halipo sana unamefundishwa nini
 ila lipo katika unaweza kufanya nini 
na unajua nini?


Hakuna muda mzuri wa kujifunza lugha mbali mbali za computer 
na kujua jinsi ya kuzitumia kama muda huo, 
maana kuna kujiajiri kwingi sana huko na hata serikali na mashirika,
yanatafuta watu wa kutengeneza software  mbali mbali.
Mfano wa lugha za kujifunza ni Android, Java, HTML, PHP,Javascript, CSS, Ruby, Python N.K.
Na pia uwezo binafsi wa kutengeneza programs peke yako, websites, blogs N.K

PUBLIC WORKING PROJECTS/Project ambazo umefanya na bado zinafanya kazi.

Tofauti ya elimu ya vyuo vyetu na vyuo vya njee,
ni kwamba mkazo uliokuwepo upo kwenye projects au practical,
ni mkubwa sana ukilinganisha na hapa ambao upo kwenye nadharia zaidi. 

Kwa hiyo hakikisha projects unayofanya inatatua matatizo ya jamii.
Hiyo hata kwenye interview sehemu ya projects inaweza mvutia HR kukuita.


IMPORTANT INTERNSHIP EXPERIENCE/MAFUNZO YA VITENDO YENYE TIJA.

Unapofika muda wa kutafuta field usifanye mzaha, tafuta makampuni ya kiteknolojia, ili ijifunze jinsi yanavyofanya kazi na hata kupata kazi kwenye makampuni mengine itakuwa rahisi kwa maana mzigo wa kuku train utakuwa umepungua.


Hayo ni maeneo muhimu ambayo ukiyashughulikia vizuri hautapoteza muda mwingi kutafuta ajira, kama hali itakuwa shwari ya uchumi.
Kwa ushauri zaidi wasiliana nami,


Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   

elisanteshibanda@yahoo.com





Elimu ya IT hapa Tanzania ni changa sana na imejaa ujuzi mwingi na unahitajika sana katika Taifa hili, 
ujuzi wa IT wa ngazi ya chini kabisa, unaweza ukampa mtu uwezo mkubwa tuu wa kujiajiri na  
kuendeleza maisha yake.

Zifuatazo ni kozi ambazo zinaweza kumsaidia yeyote kuwa na uwezo wa kujiajiri.


Jinsi ya kufanya kazi na kulipwa mtandaoni ukiwa Tanzania

Course in Graphics Design.

 Kozi hii itamuwezesha mwanafunzi kufanya yafuatayo;
  • Kuchora chochote kwa njia ya kompyuta.
  • Kubuni/design magazeti, vitabu,vipeperushi,kalenda n.k
  • Kutengeneza matangazo makubwa na madogo kwa ajili ya kuprint au kuweka mtandaoni.
  • Kubuni/design business cards, cover letter, cards za mialiko N.K
  • Kurekebisha picha zilizopigwa na camera kiustadi zaidi na kuboresha muonekano wake.

Course in Web Design

 

Kozi hii inajikita katika kuunda tovuti za aina mbali mbali yaani za kibiashara na binafsi, na hii itampa mwanafunzi uwezo kufanya yafuatayo.
  • Kuweza kuunda tovuti(website) na kuelewa inayoendana na tovuti.
  • Kuipandisha tovuti kwenye mtandao.
  • Kuunda tovuti za kisasa kwa njia tofauti.
  • kutengeneza mablogu(tovuti ambazo watu wanaweza kuongea humo yaani kuchat mfano hii ni blogu) ya aina zote.
  • kusajili tovuti ndani na njee ya nchi.
  

Course in Computer Administration

 


  1. Ujuzi huu utamsaidia mwanafunzi kupata uwezo wa kufanya yafuatayo;
  2. Kufahamu kompyuta na mifumo inayoendana nayo.
  3. Kufahamu Computer Hardware, yaani vifaa vyake  na jinsi inavyofanya kazi, na hata kujua jinsi ya kuitengeneza pale inapoharibika. 
  4. Kufahamu Computer software, yaani programu za kompyuta na aina zake, jinsi ya kuziweka, kuzitoa na hata kuzishughulikia na kuzitibu pale ambapo zinakuwa hazifanyi kazi vizuri.
  5. Kufahamu mfumo wa usalama wa kompyuta, jinsi ya kuilinda kompyuta  yako na mshambulizi ya kimtandao ya virusi na watu wa njee wanaokuzunguka.
  6. Kufahamu mifumo ya mawasiliano(Networks) ya kompyuta, jinsi inavyofanya kazi na jinsi ya kuifunga njia ya kuilinda pia.
  7. Kufahamu jinsi ya kutumia windows 10 na programu nyingine za kuendesha kompyuta mfano windows 8 na Linux.
             



Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na magroup ya Whatsapp ya MAXPO Tanzania  Maximize your potential   

Course in Advanced Microsoft Office

Kozi hii inamsaidia mtu kuweza kufanya shughuli zote za kiofisi kwa njia ya kompyuta, kuanzia zile nyepesi mpaka zile ngumu kufanya kwenye kompyuta.
Kozi hutoa uwezo wa kufanya yafuatayo;

Kutumia programu za microsoft office zifuatazo

        Microsoft Word
        Microsoft Powerpoint
        Microsoft Excel

Kwa kiwango cha juu kabisa katika

        Kukusanya data
        Kuchambua data
        Kupresent/wasilisha data mbele za watu
Na pia kutengeneza njia za kuingiza data na kutumia microsoft office katika biashara yako yoyote ile 

kwa  ajili ya kumbu kumbu na hata kuonyesha muelekeo wa biashara, katika mapato na matumizi. 



Kumalizia kozi zote hizi hupatikana kwenye vyuo vya kitaalamu yaani Professional colleges ambazo zimejikita tuu katika kozi hizi, 
 kuchagua chuo chenye uwezo mdgo utakupelekea kupoteza muda wako na kutoka katika kiwango kibaya.

Nakushauri chukua mafunzo ya MAXPO Tanzania, yanatolewa na Kampuni ya Rains Technologies Co LTD iliyopo Ilala, Bungoni Str/Chunya Str Dar es salaam.

 na wanakupangia ratiba kulingana na ratiba yako na wana Professional Lecturers wenye uzoefu na pia ni wafanyabishara katika Tehama, kwa hiyo utapata, elimu na ushauri na kusaidiwa jinsi ya kuanza, ila pia kuna vyuo vingine vipo ila sina uhakika na hivyo ila pia ukumbuke jitihada zako binafsi zitakusaidia kupata ujuzi zaidi  

Kwa ushauri zaidi wasiliana nami katika 


Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na magroup ya Whatsapp ya MAXPO Tanzania  Maximize your potential   







Katika Upande wa Elimu ya juu, ni vizuri kupata ushauri bora kabla hujaenda kujiunga na chuo chochote.
Kwa maana uamuzi wako huo utaamua mambo yafuatayo katika maisha yako...




JINSI YA KUSOMA IT: Mwongozo kwa Wanafunzi Waliofeli Form Four, 2024

KIPATO CHAKO BINAFSI
Kozi hii ya IT, Kichwa chako ni ofisi yako, kwa hiyo kama utapata elimu mbovu,utapoteza uwezo wako wa kujiajiri na unaweza ishia pabaya.


AJIRA
Interviews za kazi hizi za IT, sio nyepesi, na kwa hali hii itakushinda kushindana na watu waliofundishwa vyema na kuwa wazuri katika maeneo muhimu ya Information Technology.

MCHANGO WAKO KWA TAIFA
Kozi hii au profession hiii au kazi hii ya IT ina mzigo mkubwa katika taifa hili changa kiteknolojia.
Kuna matatizo katika jamii ambayo yanahitaji kutatuliwa kidigitali,kwa sababu hii kama utakuwa na elimu mbovu,

utakuwa mmoja wa walalamikaji badala ya wabunifu na watatuaji matatizo.



VIGEZO VYA CHUO BORA KATIKA IT
Vifuatavyo ni mojawapo ya vigezo muhimu,ila vinaweza vikawepo vingine zaidi.




UBUNIFU UNAOFANYA KAZI
katika mavyuo mengi sikatai kama kuna ubunifu ila mwingi unaishia kwenye makaratasi ya chuo na kutupwa stoo(store). 
Ubunifu hujulikana kwa project ambazo zinavuka mipaka ya chuo na kuifikia jamii.

UFUATILIAJI WA CHUO KWA PROJECT ZA WANAFUNZI.
Kuna mavyuo yanaongoza kwa kutupa store project za wanafunzi lakini pia kutokuchukulia kwa umakini project zinazofanywa na wanafunzi, kiasi kwamba wanafunzi wako huru kuforge project zao na chuo kuzipokea tuu kwa kutokujali ya kwamba hii project imefanyika au laa. 

ASILIMIA YA VITENDO KATIKA ELIMU INAYOTOLEWA.
Ni muhimu kwa chuo kuwa na asilimia kubwa sana ya vitendo kuliko nadharia

VIFAA VYA KUJIFUNZIA IT
Ni muhimu kusoma  kwenye chuo chenye vifaa vya kutosha ili ujue haswa nini kinaendelea makazini ila ni kwa  asilimia ndogo hii pointi ina umuhimu maana IT inakuwa kwa kasi na Vyuo vya haviwezi kuwa na vifaa vya kisasa kila wakati.


"Chuo kinaweza kumtengeneza mhitimu wa IT,ila ni jukumu la mwanafunzi binafsi akiwa chuoni, kutoka chuoni kama mtaalamu,na sio mhitimu pekee kwa maana wahitimu hupata shida sana kutafuta ajira wakati wataalamu hutafutwa na ajira na pia hujiajiri."




Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na magroup ya Whatsapp ya MAXPO Tanzania  Maximize your potential   


VIFUATAVYO NI VYUO BORA KUJIFUNZA IT  TANZANIA.
 1. Dar es salaam Institute of Technology (DIT)

2. St. Joseph University in Tanzania.

3.University of Dar es Salaam.

4. University of Dodoma



Kwa kumalizia, vyuo vipo vingi na wanafunzi wanazidiana uwezo 
kwa hiyo inawezekana ubunifu wa hali ya juu ukatokea kwenye chuo ambacho hakipo hata kwenye list hii, 
na pia vyuo vingine vinaweza vikaboresha ufundishaji wake na kuvipiku vyuo vilivyopo sasa.

Na la muhimu college za IT zipo nyingi na kwenye mikoa mingi, kwa hiyo kukosa nafasi kwenye vyuo hapo juu haimaanishi IT yako umeitupa, ila ina maana wewe ndio wa kukin'garisha chuo ulichokuwepo.




Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na magroup ya Whatsapp ya MAXPO Tanzania Maximize your potential  


 





Fahamu kitovu cha teknolojia( Technology Hub) hapa Tanzania ambacho wanafunzi wa chuo na wataalamu katika nyanja mbali mbali za teknolojia yaani Software developers, Web developers, Electricians, Electronics Engineers and Computer Engineers n.k hukutanika na kuvumbua au kuboresha vitu.

Kitovu cha teknolojia au kwa lugha ya kiingereza technology hub ni sehemu ambazo huanzishwa kwa malengo ya uvumbuzi na utatuzi wa matatizo kwa nji ya teknolojia. 


Kwa Afrika, sehemu hizi zimefikia 314 katika miji 93 katika inchi 42 nchi kama South Afrika ikiwa inaongeza kuwa na vitovu vingi.

Kwa hapa Tanzania, tuna kitovu cha teknolojia kimoja ambacho kinaitwa Buni Hub.

BUNI Hub.
Buni huhusika zaidi na kuwasaidia wanafunzi hata watu wabunifu katika teknolojia kwa kuwapa ushauri(mentoring) na kuwaongoza kupata uwezo wa kufanya ujasiriamali kwa kupitia teknolojia n.k.


BUNI huwa inaendesha semina, mafunzo mafupi mara kwa mara ili kuweza kuwajenga wanachama wake katika uanzishwaji wa project na hata usimamizi wa project hizo za kitaalamu na kuwaongoza waweze kufikia malengo yao.
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya BUNI hapa na wasiliana nao kuweza kujiunga. 

MANUFAA YA KUJIUNGA.
Utajenga uwezo wako binafsi katika kubuni mambo mbali mbali ya kiteknolojia.


Utakutanishwa na watu ambao wana mawazo kama yako ambao watakusaidia kusimama vizuri zaidi.

Ni sehemu ambayo inaweza ikawa uwanda wa wewe kuelewa njia ya kupata hata ufadhili wa kazi yako. 

Muhimu zaidi chochote ambacho hutumii kitapotea na kama wewe ni mwanafunzi wa IT,au kozi zozote za science ni muhimu kuwa pamoja na watu ambao wana elimu kama yako ili elimu yako isije ikalala na ukaanza kufakamia fani za watu wengine.

Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   

Application Programmer huhusika na kudesign, kutest programu katika upande wa logic, pia huandaa documentation na kutengeneza programu kwa ajili ya matumizi ya kampuni husika.


Kazi Afanyazo

  • Anafanya coding, testing, debugging, documenting na installation ya programu.

  • Anatumia lugha maalumu za computer ili kuongeza ufanisi wa programu zinazoendelea kufanya kazi.

  • Anafuatilia ufanyaji kazi wa ufanisi wa programu zote zinazofanya kazi, na kushughulikia mapungufu yote yanayojitokeza.

  • Anatumia mahitaji maalumu ambayo amepewa na kampuni, na kutengeneza programu mbazo zitasaidia kutimiza malengo hayo...mfano: Vodacom wanapotaka kuongeza offer kwenye menu ya MPESA watahitaji kumuona huyu mtu.

  • Muda wote huutumia kujiupdate ili kuhakikisha ya kwamba mifumo yote ya kampuni inafanya kazi katika viwango vya kisasa.

  • Hujifunza na kuchambua kazi mbali mbali za kampuni na kutoa mchango wake katika kuboresha mifumo husika ili kuleta ufanisi wa hali ya juu katika MIS(Management Information Systems).


Vigezo Vya Kazi.
  • Awe na uelewa mzuri wa software na hardware( Technical Capacity)

  • Awe na uwezo mzuri wa kutatua changamoto zote zinazojitokeza kwa kutengeneza majawabu ya kiteknolojia.(Problem Solving/ Analysis)

  • Awe na uwezo wa kujisamamia mwenyewe na kuchukua hatua mbali mbali za kiutendaji(Initiative).

  • Uwe na uwezo mzuri wa kuwasiliana na wengine na kuweza kuwasilisha kile ambacho unataka kufanya kwa lugha nyepesi na ya kueleweka zaidi.

  • Uwe vizuri katika kutumia muda vizuri.


Elimu na Mafunzo
Uwe amepitia kozi zifuatazo , lakini pia awe na ujuzi binafsi wa lugha za computer kama zifuatazo Java, Android, PHP, SQL, HTML,CSS, ASP.Net, Javascript, Python, VB.Net etc.

Bachelor in Computer Science

Bachelor in Information Systems

Bachelor in Software Engineering

Bachelor in Computer Engineering

Bachelor in Information Technology

Na kozi nyingine zinazofanana na hizo hapo juu. 
Kwa maelezo, msaada au ushauri zaidi usisite kuzungumza nami. 

Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa    

elisanteshibanda@yahoo.com

Fahamu Business Analyst ni nani? 
na nini kinahitajika ili kuwa Business Analyst,
ili uweze kufahamu 
kama je una muhitaji mtu kama huyu katika biashara yako au 
ujiandaaje kufanya interview ya nafasi ya Business Analyst na zaidi 
unafanyaje kujiboresha zaidi kama wewe ni Business Analyst.

Business Analyst Ni Nani?

Business Analyst ni mtaalamu ambaye anahusika katika kuisaidia biashara 
kutumia teknolojia kwa gharama nafuu, 
ili kuboresha mfumo wa biashara uweze kuipatia kampuni faida kubwa zaidi.

Chimbuko lao

Hii kazi ilianza kuchukua nafasi kubwa katika karne ya 21, wakiwa na kazi moja kubwa 
ya kuunganisha teknolojia 
iliyopo na utimizaji wa malengo ya kampuni husika.

Kazi yao

Kuleta ufanisi katika uendeshaji wa biashara.

Huhusika katika kupanga mipango mbali na kufuatilia mipango hiyo kwa umakini.


Kufuatilia mahitaji yanayojitokeza siku hadi siku katika uendeshaji wa biashara.


Kuboresha mfumo wa uendeshaji uliokowapo ili ufanye kazi kwa ufanisi zaidi.


Kutafuta majibu ya kiteknolojia juu ya changamoto zote katika mfumo wa uendeshaji wa biashara.


Sifa za kuwa Business Analyst

Uwezo wa kuwasiliana vizuri kwa njia ya kuandika na kuongea, kawaida na kitaalamu zaidi.

Uelewa wa mambo kadha yanayohusu software engineering.

Uwezo wa kufanya cost/benefit analysis.

Uwezo wa kufanya Business Case development

Uwezo wa kutumia modeling techniques 

Uongozi.

Elimu na Mafunzo ya Business Analyst

Kazi hii huwa inahitaji zaidi digrii ya Information technology, Computer Science au Software Engineering na kozi zinazolingana na zilizotajwa hapo juu.

Halafu unatakiwa ila sio lazima upate mafunzo zaidi(Certifications) kama IIBA and CBAP ila ukiwa na hizo   digrii hapo juu unafaa kuanza kazi. 


Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   
Kwa maswali zaidi wasiliana nasi.