Kompyuta ni kama yalivyo magari, yanatembea na ya na kimbi lakini yanatofautiana na yana hadhi na uwezo tofauti kulingana na mtengenezaji.
Kwanza nakupa aina ya kompyuta pamoja na matumizi yanayofaa zaidi.
LAPTOP VS DESKTOP
- Unashauriwa kutumia desktop maofisini kwa sababu zifuatazo za kiulinzi na za kiusalama, kwani ni rahisi kwa laptop kuibwa na nyaraka nyingi kupotea au kuibiwa kuliko desktop, na pia kompyuta ya desktop ina uwezo mkubwa sana ukilinganisha na kompyuta ya laptop.
- Unashauriwa kutumia laptop kama ni mfanyabiashara au mwanafunzi,kwa sababu ya wewe kuhitajika kutembea mara kwa mara na kompyuta yako ila inakupasa kuwa na desktop au external hard drive, mahali ili kuweza kuwa na back up ya data zako.
HP
Kompyuta hizi zina uimara mkubwa sana na hudumu kwa muda mrefu sana,pia zina hali ya juu ya utendaji na mara nyingi hutumiwa kwakazi zinazohitaji ukokotoaji mkubwa. Pia hutumika katika kwenye tasnia ya uhandisi na hata designing.
DELL
Kompyuta hizi zina sifa ya ubora sana zaidi husifika kwa kioo(monitor) chake kizuri sana cha HD(High definition) ambacho ni kizuri kuliko vya computer nyingine.
Kompyuta hizi hutumika sana maofisini na hata kwa kujiliwaza kwa kuangalia videos kutokana na ubora wa kioo chake.
LENOVO
Kompyuta hizi zinasifika kwa kuishi kwa muda mrefu kama ikitumika kwa matumizi ya kawaida, yaani yasiyo hitaji ukokotoaji wa hali ya juu.,kama kuangalia movies sana na kucheza michezo kama fifa, magari.
APPLE
Kompyuta hizi zina ubora wa hali ya juu pamoja na uwezo mkubwa sana na pia hudumu kwa muda mrefu. Katika USALAMA haziingiwi na virus kama kompyuta nyingine na ikitokea vimeingia ni mara chache sana. UTENDAJI wake ni mkubwa maana zina nguvu kubwa za ukokotoaji. Pia ni rahisi kubeba kwa maana ni nyembamba na nyepesi kubeba, na zaidi hutumika zaidi kufanya Graphics Design.
MUHIMU
Nimejaribu kukupa mwanga kuhusu makampuni haya, haimaanishi mapungufu haya utayakuta katika kompyuta zao zote, kwa maana hushughulika kila siku kuweza kurekebisha mapungufu hayo. Ni bora kununua kompyuta za toleo jipya kuweza kuepukana na shida zozote..
0 comments:
Post a Comment