CERTIFICATIONS  CERTIFICATIONS CERTIFICATIONS

Sijui niseme ni ubaya au uzuri Ukimaliza kusoma IT au computer science au computer engineering ndgu safari ya kupata ajira itakuwa ngumu sana kwako unahitaji kwenda kusoma tena vyeti vya ujuzi maalumu ili uonekane umebobea wapi.

NI gharama ila ukitaka kazi haraka basi nenda kasome hivyo vyeti yaani utapata kazi haraka sana.


Cisco Certified Network Professional (CCNP)

The Cisco Certified Network Associate (CCNA) certification hii inatoa  specializations katika  security, wireless, routing and switching, industrial, IoT, data center, cyber operations, collaboration and cloud.

kama unataka kazi yeyote ya system administration kama huna hichi cheti sahau kupata kazi...nenda University of Dar es salaam computing centre wanatoa.

Oracle Certified MySQL Database Administrator (CMDBA)

kama unahitaji kuhudumia systems za database bado haswa katika kazi ya system administration unahitaji sana hichi cheti, na  ni kama dhahabu maana hakuna program inayo run bila database. 

Certified Information Systems Security Professional (CISSP)

Security sasa hivi ni issue moja kubwa sana kwa makampuni mengi maana wizi ni mwingi sana, unahitaji hichi cheti ili uwe vizuri katika kulinda systems za organization, na katika certifications za muhimu kabisa hichi ni bora uanze nacho.

Microsoft Certified Solutions Associate (MCSA)

Certifications hizi zinakusaidia kuweza kuoperate na ku maintain server infrastructure za office, Servers kama kompyuta nyingine huwa zinapata changamoto nyingi unaposomea haya mambo unakuwa fundi kabisa tena certified kabisa.

Certified Data Professional (CDP)

Ulimwengu unapoelekea sasa hivi unaendeshwa na data. Certfications kama hizi zintakuweka katika ramani ya makampuni ya mawasiliano, kamali yaani yote yanayodeal na big data.

Kwa maswali zaidi wasiliana nami kupitia elisanteshibanda@yahoo.com

 


Ninavyozungumzia Information technology course najumuisha computer science, computer engineering, Software engineering etc.
Sasa zingatia vigezo vifuatavyo kwa ngazi tofauti.

CHETI


Utahitaji cheti cha form four (CSEE) chenye kuanzia pass 4 (Ukiondoa masomo ya dini)


au 
     

Utahitaji  cheti cha National vocational training award level 3.


au


Kwa kwenda kusoma business Informational technology unaweza ukapeleka hata National Business certificate stage 1 kikiwa na pass 2.




DIPLOMA

Utahitaji cheti cha advanced Certificate of Secondary Education(ACSE) ukiwa na principal pass 1 na subsidiary pass 1


au

Basic Technician Certificate (NTA Level 4) katika kozi za certificate in computer science, IT, Business IT, Computer Engineering na Electrical Engineering.


DEGREE

Utahitaji cheti cha advanced Certificate of Secondary Education(ACSE) ukiwa na principal pass 2 ambayo mojawapo lazima iwe Advanced Mathematics 

au 

ufaulu wa pass katika masomo yeyote mawili ya sayansi na Advanced Mathematics uwe na ufaulu wa subsidiary pass.

au 

Uwe na ufaulu wa GPA zaidi ya 3.0 katika ngazi ya Diploma.


Kwa maelezo zaidi wasiliana na uongozi wa vyuo vinavyotoa IT kwa kutembelea tovuti zao. Kila la kheri.

Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na magroup ya Whatsapp ya MAXPO Tanzania  Maximize your potential