Unaanzaje kutumia program ya computer kwenye biashara yako...2024



Fahamu jinsi ya kuuingiza biashara yako katika ulimwengu wa kisasa wa computer, wenye ufanisi na faida kwako maradufu.

Programu ni kitu gani?

Programu ni maelekezo ambayo huandikwa na mwanadamu katika lugha za ki computer ili computer iweze kuyafuata na kurahisisha ufanyikaji wa kazi fulani.

Ni biashara gani unaweza tumia 

programu hizi?

Biashara ya aina yeyote ile inaweza kurahishishwa uendeshaji wake, kwa asilimia 80% na zaidi, katika uendeshaji wake.

Faida ya kutumia programu ni zipi?

Faida ni nyingi sana ila kuzitaja kwa uharaka ni kurahisisha uendeshaji wa biashara mfano duka linalotumia programu katika kuhifadhi mauzo yake, huwa lina uwezo kujua nini kipo na nini kimekwisha kwa uharaka zaidi na hata ni bidhaa gani imekwisha muda wake wa matumizi kwa uharaka zaidi na pia hata kujua faida iliyopatikana kwa siku mara moja, kwa kubonyeza button moja tuu na hata kujua biashara inaendeleaje na hata kupewa ushauri na programu hiyo hiyo kipi cha kuongeza na kipi kimekaa muda mrefu.

Aina za programu ambazo hutumika.

Programu hizi zipo na zinatofautiana kutokana na vipengele vifuatavyo.
·         UTENDAJI KAZI
Hapa kuna programu ambazo zenyewe zimetengenezwa kwa ajili ya shughuli zote za kibiashara na za kiofisi, hizi mfano ni Microsoft office package, hizi hutumiwa kwenye biashara yeyote ile, kwa mafunzo mafupi sana.
Pia Kuna programu ambazo zinatengenezwa mahususi kwa ajili ya biashara yako na wataalamu wa computer ambao wewe utawalipa kwa ajili ya kazi hiyo, programu hizi huwa na ufanisi mkubwa mno kulinganisha na hizo za awali hapo juu.

·        Gharama
Programu zote zile ambazo utahitaji utengenezewe na wataalamu wa computer hizi zitakugharimu zaidi, ila kwa bei ya soko la sasa, huwa zinaanzia kiasi cha Tsh.400,000/= na kuendelea hii ni kutokana na mfumo wa biashara yako, kama ni mkubwa sana basi gharama huwa juu, kama ni mdogo sana basi gharama huwa chini.

Ila kwa programu ambazo zimeshatengenezwa teyari kwa ajili ya kazi hiyo, nikiamaanisha mfano microsoft office zenyewe ni gharama nafuu zaidi kuanza kutumia, chini sana ukilinganisha na  kundi la programu za hapo juu.
Jinsi ya kupata programu mahususi 

ajili ya biashara yako.
 Ondoa shaka kabisa hapa kuna wataalamu mbali mbali ambao wamebobea katika utengenezaji wa programu hizi kwa sasa ni....
·         Duka Pro
·         Nyumbani Creative
Endapo utahitaji maelezo mengine yeyote zaidi, kuhusu maswala haya, usisite kuwasiliana nami, nitakusadia zaidi katika elisanteshibanda@yahoo.com na +255753592886 
 Jinsi ya kupata programu ya kiofisi 
  ajili ya biashara yako.

Jinsi ya kupata programu hizi na mafunzo ya jinsi ya kuitumia, tafadhali wasiliana nami pia kwa namba nilizozitoa hapo juu au unaweza kutafuta madukani na wakakuwekea kwa gharama nafuu zaidi ila kwa mafunzo inabidi utafute vyuo vinavyotoa mafunzo ya "computer course" ambayo pia hata mimi ni trainer/mwalimu wa hayo mafunzo ndani ya wiki chache tuu utakuwa teyari kabisa.
  Hitimisho

Computer huwa zinaathiriwa na virusi na hata watu wenye nia mbaya wanaweza ingia na kufuta taarifa zako, kwa hiyo kuwa makini computer yako kujua nani anaitumia na jee ni muhusika, na pia kutumia programu za kujikinga na virus zinazoitwa Anti-Virus mfano Karspesky na zaidi hifadhi data zako sehemu mbali mbali mfano kwenye external drives, flash drives na internet.

Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   
Elisante Shibanda.
IT Consultant/Trainer 
elisanteshibanda@yahoo.com
+255753592886





0 comments:

Post a Comment