Ulimwengu wa teknolojia ya mtandao yaani Information
technology ni mkubwa sana, na wengi huwa
wanajikuta wanashindwa kufikia malengpo yao, kwa kushindwa kujua
tofauti ya kozi zilizopo, hebu fuatilia uelewe kipi ni kipi?
Information Technology
Hii ni kozi ambayo inadili zaidi na mawasiliano ya njia ya
kompyuta na uendeshaji wa mifumo/systems ya kompyuta na hata designing.
kozi
hii hutoa watu/professionals ambao ni system administrators,ICT officers,
Graphics Designers etc
watu ambao wapo kwa ajili ya kuwasaidia watu wengine kuweza
kutumia vizuri, mifumo ya kompyuta.
Kazi.
Hawa watu wengi huwa wanaajiriwa,
zaidi ila pia wanaweza
kuajiajili kwa katika kufanya maintenance ya vifaa vya ICT, ICT Equipment
supply,
na hata kufunga mifumo ya network sehemu mbali mbali na akijiendeleza
huweza kuwa Webmaster wa tovuti mbali mbali.
Kipato.
Mishahara yao hulipwa kulingana na elimu ya Degree au ya
diploma aliyonayo kama fani nyingine na Zaidi ikizingatia kazi anayofanya na
unyeti wa kazi hiyo.
Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa
Computer science.
Uwanda huu upo ndani zaidi kuliko IT, maana hawa watu mbali
na kujua vitu vyote vya kozi ya IT,
pia huweza kujua kutengeneza program za aina
mbali mbali za computer, na pia hufundishwa lugha nyingi za computer na huwa
wako vizuri kiasi hata kwenye hardware ya computer.
Kazi.
Hawa watu utawakuta kama pia ma system administrators,
business analysts, system analysts, ICT Officers, Application programmers,
software developers.
Pia wengi hujiajiari na kuanzisha makampuni/biashara za
kutengeneza kompyuta hardware na software,
websites na kazi nyinginezo nyingi
katika uwanda wa technology.
Kipato
Wanapoajiriwa kipato chao hakitofautiani na IT.
Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa
Computer Engineering
Fani hii, hujikita Zaidi na hardware ya computer, huku
tunapata watu ambao wanaunda vifaa ambavyo vinaweza fanya kazi na mifumo ya
computer.
Hawa kwa nchi zenye viwanda vya kutengeneza vifaa hivyo, huwa ni soko
kubwa sana,
ila kwa nchi ambazo zinaendelea huwa bado wana soko dogo sana, na
hata huogopwa kuajiriwa kulingana na Title yao ya Kuwa engineer.
Kazi.
Hawa hufanya kazi ya kutengeneza vifaa ila pia huweza
kufanya kazi nyingi ambazo mtu wa computer science anafanya,
pia ni mafundi
waliobobea katika kurekebisha computer mbovu.
Kipato
Hawa huwa na mshahara wa juu kuliko IT na Computer Science,
maana hulipwa katika kiwango cha ma engineers,
lakini pia hufungua biashara
kubwa za computer maintenance na hardware Suppliers na zaidi...
Software engineering
Katika Fani hii tunakutana na watu ambao wanataka kubobea
katika kutengeneza programu za computer,
hawa watadeal na program tuu na kidgo sana mambo mengine katika fani ya teknolojia.
Kazi.
Hawa hufanya kazi kutengeneza program za kila aina, pia
huingia kwenye network na kubobea humo,
na huwa pia kuweza kufanya kazi za
Computer Science kwa kiasi na hukinzana kabisa na computer engineers maana wao
hufanya kazi na hardware.
Kipato
Hawa wana mshahara mkubwa wa kiwango cha Engineer kama
computer engineer anavyolipwa na pia huwa wanajiajiri sana na kuanzisha
makampuni ya kutengeneza programu.
Jinsi ya Kujiendeleza…
Ulimwengu wa Computer umejaa vyeti vya mafunzo mbali,
ili mtu
abobee katika sehemu maalumu hizo huitwa certifications mfano mafunzo ya
Network hutoa vyeti,
kama CCNA, CCNP na kuendelea na mafunzo ya database kama
Oracle , na hata auditing(Ukaguzi) kwa maelezo Zaidi fuatilia article yangu ya
kuhusu certications za IT.
Lakini pia anaweza jiendeleza katika masters degree za vitu
mbali na hata kuwa Tutorial au lecturer au professor maana bado kuna upungufu
mkubwa mno katika ngazi hizo.
Kwa muongozo zaidi, Wasiliana nami katika email elisanteshibanda@yahoo.com au
Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa