Kanuni nzuri za biashara kutoka kwa Mangi.


Kama kijana mdogo nisiyekuwa na uzoefu  hata kidogo  wala msaada katika biashara, nilijikuta nikiona jinsi gani duka la Mangi lilikuwa likikua kwa kasi, na la kwangu taratibu mno, nilijiuliza maswali mengi lakini kwa sababu Mangi alikuwa mfanyabiashara mwenzangu na rafiki yangu sikusita kumuomba ushauri, na ndipo aliponiambia mambo haya amabyo yalibadilisha biashara yangu na mtazamo wangu katika uwanda huu wa biashara.

MTAJI.
Unapoanzisha biashara na unapokuwa na mtaji wako wa kiasi fulani , unapokuwa ukipata faida . inakupasa ufanye kila liwezekanalo kutogusa FAIDA, sijakosea sio MTAJI pekee bali FAIDA na MTAJI kwa mwaka mzima, hapo ndipo utaona ukuaji wa duka unaostahili..utapata wapi hela ya kula na matumizi mengine we mtu mzima umiza kichwa.

UENDESHAJI
Imezoeleka kuwaweka ndugu na jamaa au hata watu tuu tunaowaajiri kama wauzaji halafu sio tukaendelea na kufanya kazi nyingine.HAYO NI MAKOSA TENA NI MWIKO KUFANYA HIVYO.
Wafanyakazi waajiriwa wengi wameanzisha maduka yamekufa kwa sababu hiyo.
Wanaopaswa kuendesha duka lako ni "WEWE", "MKEO" na "WEWE+MKEO" kama watu hao hawatakuwepo, tafuta shughuli nyingine ya kufanya na hela yako.

MUNGU
Unaweza ukafanya vizuri kote katika hayo niliyoyasema hapo juu, lakini ukweli ni kwamba biashara zimetawaliwa na nguvu za giza sana, ni lazima uchague utakaa upande gani na ukae huko moto  moto na sio robo au nusu, kama ni uchawi ujue ipo siku utakufa na biashara yako itakufa vibaya na utaangamiza watoto na familia yako so nakushauri mtafute Mungu wako.

NIDHAMU
Watu wengi huchukia mabosi, wakiwaona kama wanawanyanyasa wanavyowashurutisha kufanya kazi, yaani wakitunza nidhamu kazini, lakini ukweli ni kwamba biashara inahitaji nidhamu ya hali ya juu mno, isiyosuburi kukumbushwa...mazoea, uchelewaji, kauli chafu,uvivu huua biashara mara moja.

UTU
lazima uwe na utu, ujali wafanyakazi wako, kimahitaji na hata kimahusiano yaani waheshimu, hata kama umewazidi kipato kiasi gani.
"Kumbuka wamiliki wengi wa biashara wameuawa na majambazi kwa mpango uliosukwa na wafanyakazi wao au hata kuporwa mali kutokana na kisasi walichonacho wafanyakazi"

FULLITIME/PARTTIME
Biashara sio part time nik full time job kama hauko teyari kuwekeza muda wako wote nenda kanunue hisa wekeza huko maana huko hauhitajiki sana kama una hisa ndogo na hisa zikizidi bado ushauri wangu utaendelea utakabidhiwa ofisi tuu.

Kwa hayo nimeona nikushirikishe wewe ili kama umejipanga kufanya biashara basi uwe makini usije ukapoteza hela zako bure.
Mangi yeye ni mfanyabishara mkubwa wa maduka ya jumla ya vyakula kwa aina nyingine ya biashara tanua fikra zako.

2 comments: