Tehama(ICT) na Teknolojia kwa ujumla imeweza kuajiri zaidi ya milioni 6.7 na inawalipa mara 2 zaidi ya sekta nyingine katika Nchi ya Marekani(compIT), lakini kwa hapa Tanzania bado fani hii ina watu wachache sana na ukizingatia vijana wengi wanalalamika ukosefu wa ajira.
Kwa nini ni jawabu mojawapo la Ajira?
- Mtaji wake ni mdogo sana na ukilinganisha na maeneo mengine ya kuwekeza kama kilimo na sekta nyingine na pia unalenga vijana zaidi ambao ndio wanakumbwa na tatizo hilo la ukosefu wa ajira.
- Tehama haihitaji mtu aajiriwe ili aweze kujipatia kipato kwenye sekta hii kwa maana hutegemea zaidi ubunifu wa mtu na juhudi zake binafsi na mahali mtu alipo ndio panaweza geuka ofisi.
- Unaweza ukajifunza tehama bila hata kuingia darasani au kwenda chuoni na ndani ya mwezi ukawa vizuri kabisa.
Ukitaka kujifunza tehema wasiliana nasi tutakupa mwanga katika tasnia hii.
0 comments:
Post a Comment