Kwa miaka tumekua tukiona watu wanaanzisha mablogu kama michuzi, milardayo na wengineo wengi, na tunafurahi maana wanatuletea taarifa nyingi kwa kweli, lakini unajua hawa wanapata hela nyingi ambazo hata wewe unaweza pata!!!
Blogu ni tovuti ambazo zinaruhusu mtumiaji aweze kuhusishwa na kile ambacho kimewekwa kwenye tovuti, kama habari kwa mfano, mtu anaweza iona na kuandika yeye ameiopokeaje na hata kuwasiliana papo na hapo kwa watu wengine kuhusu habari hiyo.
Je kuanzisha biashara hii inagharimu kiasi gani?
Kuanzisha biashara hii inahitaji uwelewa wa utumiaji wa mtandao, inahitaji uwe na internet zaidi ya hapo hakuna gharama nyingine zaidi...Kumbuka: uelewa huu wa mtandao sio wa kwenda chuo ni uelewa mdogo tuu ambao unaweza kujua ndani ya wiki 2 au moja tuu.
Nini kinahitajika ili kuanzisha biashara hii?
unahitaji kitu cha kuandika, mfano michuzi yeye kaamua kujikita kwenye habari na kwa hilo amewapata wengi ambao wanatembelea kwenye blogu yake...kama hauna fikiri kwanza ni kitu gani watu gani wanataka.
Unapataje pesa sasa?
Jinsi blogu yako itakavyo vuta watu wengi na kuingia, basi utapata hela kwa njia zifuatazo;
- Matangazo
Ukitembelea blogu hizi utakuta matangazo kama ya vodacom na makampuni mengine ambayo hulipa mtu anapoclick tuu na hata mtu anapoliona hilo tangazo. Mfano mkikubaliana mtu anapoclick upate Tsh 100 na kuendelea na kwa mwezi labda ulipwe laki 4 ni wewe utachagua na kukubaliana na mwenye tangazo.
- Pia unaweza uza vitu kama vitabu vya mtandao vyenye mafunzo mbali mbali kwa njia ya sauti au video kwa watu.
- Unaweza pia ukauza post zako kwa njia ya kuwaweka kampuni kama ndio wamechangia kuileta...mfano: unawe za kwenye TV kipindi cha Tamthilia unasikia tamthilia hii imeletwa kwenu na Wizara ya afya.
Ukweli ni kwamba huku ubunifu wako utakuletea pesa, na kujitoa kwako na ukitaka kujifunza hivi endelea kutembelea hapa na karibuni tutaleta mafunzo haya bure.