Anti-Virus ni programu ambayo hutumika kuilinda kompyuta, kutoka kwa mashambulizi ya virusi ambavyo huathiri mifumo yake na uwezo wake wa kiutendaji kazi.


Jinsi Anti-virus inavyofanya kazi.
kama bodyguard anavyomlinda mtu, basi na anti-virus hulinda kompyuta kwa staili hiyo. Yenyewe huhakiki na kupitia kila kinachofanywa na kompyuta ili kuweza kujua kama kitakuwa na madhara au la!
Mfano:
Unapoingiza tuu flash yako kwenye kompyuta kabla hata hujaifungua anti virus ni ya kwanza kuleta warning kama kuna kirusi au la kwa sababu imeshaipitia kabla.


Tatizo lilipo:
Kutokana na kitendo hicho processor ya kompyuta hufanya kazi mara mbili zaidi kwa kila kitendo kinachofanyika, ya kwanza ikiwa ni kazi ya Anti virus(ukaguzi) na ya pili ikiwa ni kazi ya Operating system(windows) ya kumhudumia mtumiaji matakwa yake.
kwa hali hiyo anti virus kubwa zenye nguvu kama karspesky, avg, avast huhitaji uwezo mkubwa zaidi wa ukokotoaji ili ziweze kufanya kazi na kompyuta na endapo uwezo wa kompyuta ni mdogo, hapo husababisha kompyuta kufanya kazi kwa utaratibu na hata husababisha ukwamaji(stucking) wa kompyuta ikiwa inafanya kazi mara kwa mara.


Ushauri.
kwa matumizi ya sasa unashauriwa kuongeza uwezo wako wa kompyuta mpaka kufikia RAM=4GB na zaidi muone mtaalamu wa tehama ili aweze kukusaidia kusimamia matumizi mazuri ya diski yako inayobeba Operating system iwe na nafasi ya kutosha.

Je ni nani mwenye kiwanda hichi? na ni kwa nini Rwanda, je kompyuta hizi zina uwezo gani?

Soma zaidi.. Rwanda ni kati ya nchi zinazokua kiuchumi kwa kasi hapa katika Afrika Mashariki na miaka ya hivi karibuni imeanzisha utengenezwaji wa kompyuta, kwa kusaini mkataba na kuiruhusu kampuni ya POSITIVO BGH kuweza kuanza utengenezaji wa kompyuta nchini mwake.

POSITIVO BGH  ni muunganiko wa kampuni 2 kubwa, kutoka Amerika ya kusini, ambazo ni POSITIVO yenye makao yako nchini Brazil na BGH yenye makao yake Argentina, kampuni zilianza tangia muda kufanya biashara kwa kuungana na katika moja ya mipango yake ziliamua kuanzisha kiwanda Afrika ili kupanua soko lake.

Kwa nini Rwanda?
Kutokana na maelezo ya Juan Ponelli, Rais wa POSITIVO Afrika, Rwanda imeonesha juhudi kubwa za kusaka maendeleo na pia ina GDP nzuri ya 8.8% ukilinganisha na nchi nyingine hapa Afrika na pia ina utulivu wa kutosha...soma zaidi

Hii ni mojawapo ya kompyuta zinazotengenezwa..

Positivo BGH 11CLE2-R

Specifications
OS: Windows 8.1 Pro
Processor: Intel® Celeron® N2840
Platform: Bay Trail
RAM Memory: 2 GB
Storage: 320 GB
Screen: 11,6"
Camera: 1 Mpx HD
Video: Intel® HD Graphics; DirectX 11
Audio: High Definition
Ports: VGA y HDMI
Memory Reader: 9-in-1 memory multi reader
Security: Kensington port


Kompyuta ni kama yalivyo magari, yanatembea na ya na kimbi lakini yanatofautiana na yana hadhi na uwezo tofauti kulingana na mtengenezaji.
Kwanza nakupa aina ya kompyuta pamoja na matumizi yanayofaa zaidi.
LAPTOP VS DESKTOP
  • Unashauriwa kutumia desktop maofisini kwa sababu zifuatazo za kiulinzi na za kiusalama, kwani ni rahisi kwa laptop kuibwa na nyaraka nyingi kupotea au kuibiwa kuliko desktop, na pia kompyuta ya desktop  ina uwezo mkubwa sana ukilinganisha na kompyuta ya laptop.
  • Unashauriwa kutumia laptop kama ni mfanyabiashara au mwanafunzi,kwa sababu ya wewe kuhitajika kutembea mara kwa mara na kompyuta yako ila inakupasa kuwa na desktop au external hard drive,  mahali ili kuweza kuwa na back up ya data zako.
MAKAMPUNI YA KOMPYUTA NA SIFA ZAKE
HP
Kompyuta hizi zina uimara mkubwa sana na hudumu kwa muda mrefu sana,pia zina hali ya juu ya utendaji na mara nyingi hutumiwa kwakazi zinazohitaji ukokotoaji mkubwa. Pia hutumika katika kwenye tasnia ya uhandisi na hata designing.

DELL
 Kompyuta hizi zina sifa ya ubora sana zaidi husifika kwa kioo(monitor) chake kizuri sana cha HD(High definition) ambacho ni kizuri kuliko vya computer nyingine.

Kompyuta hizi hutumika sana maofisini na hata kwa kujiliwaza kwa kuangalia videos kutokana na ubora wa kioo chake.

LENOVO
Kompyuta hizi zinasifika kwa kuishi kwa muda mrefu kama ikitumika kwa matumizi ya kawaida, yaani yasiyo hitaji ukokotoaji wa hali ya juu.,kama kuangalia movies sana na kucheza michezo kama fifa, magari.

APPLE
Kompyuta hizi zina ubora wa hali ya juu pamoja na uwezo mkubwa sana na pia hudumu kwa muda mrefu. Katika USALAMA haziingiwi na virus kama kompyuta nyingine na ikitokea vimeingia ni mara chache sana. UTENDAJI wake ni mkubwa maana zina nguvu kubwa za ukokotoaji. Pia ni rahisi kubeba kwa maana ni nyembamba na nyepesi kubeba, na zaidi hutumika zaidi kufanya Graphics Design.

MUHIMU 
Nimejaribu kukupa mwanga kuhusu makampuni haya, haimaanishi mapungufu haya utayakuta katika kompyuta zao zote, kwa maana hushughulika kila siku kuweza kurekebisha mapungufu hayo. Ni bora kununua kompyuta za toleo jipya kuweza kuepukana na shida zozote..


 

Fuatilia kwa umakini mambo haya ili usije ukapoteza hela yako bure au kupata kompyuta isiyolingana na mahitaji yako.

MATUMIZI

Kwa matumizi ya kiofisi ,kama kuandika (microsoft word)  na kutumia spreadsheet(excel),intaneti na kusoma barua pepe unapaswa kununua kompyuta yenye uwezo mdogo hadi yenye uwezo wa kati:
vipimo:
RAM=2GB-4GB
Processor= 1.8-2.0 Ghz 
Architecture= 32Bit.


Kwa matumizi ya kujiliwaza(Entertainment) mfano kucheza michezo kama mpira(FIFA) magari,au kwa matumizi ya kudesign hii unahitaji kompyuta yenye uwezo mkubwa:
Vipimo:
RAM=4GB-8GB
Processor=2.5Ghz--> Nakuendelea, Dual-->na Kuendelea
Architecture= 64Bit.


VIFAA VINAVYOAMBATANA NA KOMPYUTA.

Ni muhimu sana kuhakikisha vifaa kama adapter vinavyokuja na kompyuta kama vimetengenezwa na mtengenezaji halisi wa kompyuta hiyo na ni original! Unapokuwa unapewa Vifaa hivyo hakiki kama vimeandikwa jina la mtengenezaji wa kompyuta hiyo mfano HP na adapter yake iandikwe HP na hata muonekano wake uwe unaridhisha machoni ya kwamba ni original ukijimuisha uzito wake pia. 


HAKIKI UKUBWA WA HARD DRIVE, RAM NA PROCESSOR .

hakikisha kompyuta inapowashwa inaonesha ukubwa halisi kama ulivyoandikwa kwenye vitabu vyake au kama mlivyokubaliana na muuzaji. Ili usidanganywe, inapowashwa kompyuta pale kwenye desktop right-click computer halafu chagua properties hapo utaweza kuona ukubwa wa vitu hivyo.


NENDA MAHALI PANAPO AMINIKA KWA UUZAJI WA VITU ORIGINAL.

Usijaribu kununua kompyuta maeneo ambayo yamezoeleka kwa wizi kwa maana , kuna mambo mengi ambayo mtu mwingine hawezi kukagua zaidi ya mtaalamu wa Tehama. Na kama utahitajika kununua huko tafadhali nenda na mtaalamu wa tehama.

HAKIKI THIBITISHO(WARRANTY) YA KOMPYUTA HIYO.

Kama kompyuta ni mpya ni lazima na muhimu iwe na thibitisho hata la kuanzia mwaka mmoja(1) na ikipungua sana napo haishauriwi mwisho miezi sita(6).


USIJARIBU KUNUNUA KOMPYUTA MPYA KUTOKA KWA MTU AU KOMPYUTA YENYE UWEZO MKUBWA KWA GHARAMA NDOGO.

Kuwa makini kizuri chajiuza kibaya chajitembeza. Unapoona kompyuta yenye uwezo mkubwa kwa gharama ndogo usinunue mpaka umeipeleka kwa mtaalamu aihakiki kama ni nzima.

Imeandaliwa na 
Elisante Shibanda.