Kwa miaka tumekua tukiona watu wanaanzisha mablogu kama michuzi, milardayo na wengineo wengi, na tunafurahi maana wanatuletea taarifa nyingi kwa kweli, lakini unajua hawa wanapata hela nyingi ambazo hata wewe unaweza pata!!!

Blogu ni tovuti ambazo zinaruhusu mtumiaji aweze kuhusishwa na kile ambacho kimewekwa kwenye tovuti, kama habari kwa mfano, mtu anaweza iona na kuandika yeye ameiopokeaje na hata kuwasiliana papo na hapo kwa watu wengine kuhusu habari hiyo.

Je kuanzisha biashara hii inagharimu kiasi gani?
Kuanzisha biashara hii inahitaji uwelewa wa utumiaji wa mtandao, inahitaji uwe na internet zaidi ya hapo hakuna gharama nyingine zaidi...Kumbuka: uelewa huu wa mtandao sio wa kwenda chuo ni uelewa mdogo tuu  ambao unaweza kujua ndani ya wiki 2 au moja tuu.

Nini kinahitajika ili kuanzisha biashara hii?
unahitaji kitu cha kuandika, mfano michuzi yeye kaamua kujikita kwenye habari na kwa hilo amewapata wengi ambao wanatembelea kwenye blogu yake...kama hauna fikiri kwanza ni kitu gani  watu gani wanataka.

Unapataje pesa sasa?
Jinsi blogu yako itakavyo vuta watu wengi na kuingia, basi utapata hela kwa njia zifuatazo;

  • Matangazo
Ukitembelea blogu hizi utakuta matangazo kama ya vodacom na makampuni mengine ambayo hulipa mtu anapoclick tuu na hata mtu anapoliona hilo tangazo. Mfano mkikubaliana mtu anapoclick upate Tsh 100 na kuendelea na kwa mwezi labda ulipwe laki 4 ni wewe utachagua na kukubaliana na mwenye tangazo.

  • Pia unaweza uza vitu kama vitabu vya mtandao vyenye mafunzo mbali mbali kwa njia ya sauti au video kwa watu.

  • Unaweza pia ukauza post zako kwa njia ya kuwaweka kampuni kama ndio wamechangia kuileta...mfano: unawe za kwenye TV kipindi cha Tamthilia unasikia tamthilia hii imeletwa kwenu na Wizara ya afya.
Ukweli ni kwamba huku ubunifu wako utakuletea pesa, na kujitoa kwako na ukitaka kujifunza hivi endelea kutembelea hapa na karibuni tutaleta mafunzo haya bure.

Tehama(ICT) na Teknolojia kwa ujumla imeweza kuajiri zaidi ya milioni 6.7 na inawalipa mara 2 zaidi ya sekta nyingine katika Nchi ya Marekani(compIT), lakini kwa hapa Tanzania bado fani hii ina watu wachache sana na ukizingatia vijana wengi wanalalamika ukosefu wa ajira.

Kwa nini ni jawabu mojawapo la Ajira?

  • Mtaji wake ni mdogo sana na ukilinganisha na maeneo mengine ya kuwekeza kama kilimo na sekta nyingine na pia unalenga vijana zaidi ambao ndio wanakumbwa na tatizo hilo la ukosefu wa ajira.
  • Tehama haihitaji mtu aajiriwe ili aweze kujipatia kipato kwenye sekta hii kwa maana hutegemea zaidi ubunifu wa mtu na juhudi zake binafsi na mahali mtu alipo ndio panaweza geuka ofisi.
  • Unaweza ukajifunza tehama bila hata kuingia darasani au kwenda chuoni na ndani ya mwezi ukawa vizuri kabisa.

Ukitaka kujifunza tehema wasiliana nasi tutakupa mwanga katika tasnia hii.



 Programu bora Afrika
   Afrika hatuna haja ya kushindana kugundua teknolojia kama Mataifa mengine kwa maana huko huhitaji pesa nyingi sana, ila tunaloweza kufanya ni kuitumia teknolojia iliyekuwepo na kuiweka katika mazingira ambayo itatusaidia katika maisha, Pongezi ziwaendee hawa wataalamu hawa wa tehama walivyo weza kufanya haya. Angalizo zipo nyingine sokoni pia ila muda unavyozidi kwenda tutazigundua na kuzitangaza ili zifahamike. Tazama hapa

Hebu jaribu kuchukua nafasi ya Human resource manager(Meneja wa rasilimali za binadamu) akiwa amepokea maombi ya watu 5000 kwa ajili ya nafasi moja ya kazi aliyoitangaza, unadhani atapitia na CV yako kwa jinsi ilivyo? 😓

Basi kama unataka kufanya CV yako, ipendeze kimuonekano na hata iweze kumzuia meneja aliyechoka kupitia CV za watu hebu ingia hapa tengeneza akaunti yako bure na fuata maelekezo maana ni rahisi mno kutumia.
 
  • Kwanza Relax acha uoga na punguza presha, kutype ni kitu chepesi sana.
  • Fahamu herifu za kompyuta zilipo na ukumbuke taratibu taratibu mahali zilipo kila moja hata ikiwa moja kwa siku.
  • Acha kutype kwa kidole kimoja, tafadhali weka mikono yako yote kwenye keyboard na yote ifanye kazi ya kutype.
  • Acha kutumia kidole kimoja kwa kutype kwa kila mkono, tumia vidole vyote kwa kila mkono.
  •  Hakikisha kila kidole kina herufi ambazo kina husika na kutype zinaweza zikawa mbili au tatu ...mfano kidole changu kidogo kinahusika na herufi A,Q huku kidole gumba kikitumika kwa space.
  • Usiogope kukosea kutype herufi pindi unapotype kwa haraka maana hamna shortcut lazima ukubali makosa ili uweze kupata spidi nzuri ya kutype.
  • Tumia programu za bure kabisa za kukufundisha kutype ndani ya wiki moja utakuwa vizuri kabisa. mfano: tembelea hapoa ujipatie programu yako ya bure www.typingmaster.com
  1. Usiishi katika mitandao ya kijamii HAMNA MAISHA HUKO UNAJIDANGANYA TUU!!
Siku ina masaa 24, usitumie masaa mengi huko maana sio maisha halisi kama unavyodhani. kaa na watu unaowajali zaidi, watu halisi wa karibu yako ie majirani,utakapoumwa au kuwa na tatizo la ghafla huyo rafiki yako mbelgiji au mnamibia au muafrika ya kusini hataweza kukusaidia.

    2.Usipende kuandika ujinga.
Katika ulimwengu wa sasa, watu wengi hutafuta kuwafahamu wengine katika uelewana hekima kwa vile wanavyoandika kwenye mitandao ya kijamii, kwa hali hiyo waajiri kama serikali na makampuni huhakiki sana watu kabla hawajawaajiri kuwa ni wema.

   3.Usipige picha za ajabu na zisizona maadili.
Hili wote tulishuhudia pale muheshimiwa alipoteua wanawake kadhaa na pindi tuu walipoingia ofisini ghafla picha zao za ajabu zikaibuka mitandaoni zikiwachafua wao na muheshimiwa kwa ujumla akishushiwa hadhi yake.

   4.Usipende kuandika taarifa zinazoonyesha mahali ulipo.
Ni vyema kushare mahali ulipo kama ni pazuri lakini kumbuka kuna waovu wengi wanaweza kuchukulia hiyo kama nafasi ya kukufanyia uhalifu wewe au familia yako ulipoiacha...hizi ni nyakati ngumu.

   5.Usitaje majina ya watu mashuhuri au yeyote yule pale unapoandika kitu.
Sheria ya Tanzania ya mtandao ni kali sana, hata kama mamia wamemtaja wewe unashauriwa usimtaje maana huo ndio utakuwa ushahidi tosha wa kukufunga...Hili limekuwa tatizo hata tunaona muheshimiwa raisi amekuwa akikamata wengi ambao wanamtukana, hafanyi ubabe au hayuko njee ya sheria, yuko katika sheria kabisa na ana haki ya kumshtaki yeyote atakayemnenea vibaya bila kibali chake.

   6.Unapotumiwa picha chafu na mtu yeyote yule futa na umkanye huyo mtu na kama una uwezo nenda hata polisi kama utakuwa hujafuta hizo picha kama unataka huyo mtu akamatwe.

   7.Usikubali kuwa tagged katika post zozote zile za uchochezi au uchafu wowote ule.

  8.Kama una addiction au tatizo la kutumia mitandao hii bila kipimo, vunja kwa kutafuta kitu cha kuchukua nafasi yake hiyo taratibu taratibu..mfano anza kujiuliza taratibu maswali kama "Una hela za kutosha? unaenda wapi? uko wapi?" pia FANYA KAZI,  Omba Mungu akusaidie na incase ACHA UMBEA.


Kutokana na  maendeleo ya kiteknolojia, sio jambo la kuepuka tena kufanya manunuzi kwa njia mtandao wa internet, maana umejaa vitu vya thamani ndogo na vizuri lakini pia umejaa wezi.  Fuatilia haya ili uweze kufanya manunuzi bila kujutia...

  1. Fungua akaunti pekee benki ambayo itatumika kwa ajili ya matumizi hayo ya manunuzi tuu, na uweke hela tuu pale pindi unapotaka kununua vitu, tunafanya hivyo ili endapo akaunti ikafikiwa na wezi wasiweze kuiba chochote.
  2. Pata elimu ya kutosha benki juu ya kitu gani cha kulinda kuhusu taarifa zako.
  3. Nunua sehemu maarufu au kwenye tovuti zinazofahamika dunia nzima kwa manunuzi mfano...GooglePlay, Amazon,eBay na alibaba.
  4. Usimtumie mtu usiyemfahamu taarifa zako za kibenki kwa njia ya email au yeyote ile.
  5. Hakikisha katika browser yako wakati unataka kufanya manunuzi pale kwenye sehemu ya address  imeandikwa au inaanza address kwa njia hii "HTTPS://....." na sio "HTTP://...." ina maana ya kitaalamu "Hyper text transfer protocol secure"
  6. Jiridhishe ya kwamba hiyo ndio tovuti yenyewe au kuna mtu ametengeneza tovuti feki ili kukuibia taarifa zako.
  7. Ukimaliza kufanya manunuzi yako ni vyema zaidi ukafuta browsing history yako yote ili kufuta cookies zenye mabaki ya taarifa zako.
  8. Muone mtaalamu wa Ecommerce ili akusaidie unapotaka kufanya manunuzi makubwa.

Battery hutumika kuendesha umeme ndani ya laptop yako endapo pale unapokuwa hujaichomeka kwenye charge laptop yako.



Uharibifu unaofanyika.
  1. Unapotumia laptop ikiwa imechomekwa kwenye umeme siku nzima bila kuichomoa pale battery inapojaa.
  2. Unaposafiri kwa muda mrefu au kiacha laptop bila kuitumia kwa muda mrefu, na kuiacha battery ya laptop ndani ya laptop bila kuitoa.
  3. Unaponunua adapter feki ili kuchaji battery ya laptop yako.
Ufumbuzi.
  • Laptop ikijaa charge chomoa kwenye umeme na ikiisha chomeka.
  • Ukiona unasumbuka na chomeka chomoa ya hapo juu, tafuta energy management software hiyo itakusadia.
  • Unaposafiri kwa muda mrefu zaidi ya siku moja au kupanga kuto kuitumia laptop yako kwa muda mrefu, chomoa battery ya laptop na uihifadhi mahali salama.
  • Tumia vifaa au adapter original vya laptop husika vyenye meno matatu(Earth,Live and Neutral).
  • Ukiona hali inakuwa mbaya omba msaada.





Anti-Virus ni programu ambayo hutumika kuilinda kompyuta, kutoka kwa mashambulizi ya virusi ambavyo huathiri mifumo yake na uwezo wake wa kiutendaji kazi.


Jinsi Anti-virus inavyofanya kazi.
kama bodyguard anavyomlinda mtu, basi na anti-virus hulinda kompyuta kwa staili hiyo. Yenyewe huhakiki na kupitia kila kinachofanywa na kompyuta ili kuweza kujua kama kitakuwa na madhara au la!
Mfano:
Unapoingiza tuu flash yako kwenye kompyuta kabla hata hujaifungua anti virus ni ya kwanza kuleta warning kama kuna kirusi au la kwa sababu imeshaipitia kabla.


Tatizo lilipo:
Kutokana na kitendo hicho processor ya kompyuta hufanya kazi mara mbili zaidi kwa kila kitendo kinachofanyika, ya kwanza ikiwa ni kazi ya Anti virus(ukaguzi) na ya pili ikiwa ni kazi ya Operating system(windows) ya kumhudumia mtumiaji matakwa yake.
kwa hali hiyo anti virus kubwa zenye nguvu kama karspesky, avg, avast huhitaji uwezo mkubwa zaidi wa ukokotoaji ili ziweze kufanya kazi na kompyuta na endapo uwezo wa kompyuta ni mdogo, hapo husababisha kompyuta kufanya kazi kwa utaratibu na hata husababisha ukwamaji(stucking) wa kompyuta ikiwa inafanya kazi mara kwa mara.


Ushauri.
kwa matumizi ya sasa unashauriwa kuongeza uwezo wako wa kompyuta mpaka kufikia RAM=4GB na zaidi muone mtaalamu wa tehama ili aweze kukusaidia kusimamia matumizi mazuri ya diski yako inayobeba Operating system iwe na nafasi ya kutosha.

Je ni nani mwenye kiwanda hichi? na ni kwa nini Rwanda, je kompyuta hizi zina uwezo gani?

Soma zaidi.. Rwanda ni kati ya nchi zinazokua kiuchumi kwa kasi hapa katika Afrika Mashariki na miaka ya hivi karibuni imeanzisha utengenezwaji wa kompyuta, kwa kusaini mkataba na kuiruhusu kampuni ya POSITIVO BGH kuweza kuanza utengenezaji wa kompyuta nchini mwake.

POSITIVO BGH  ni muunganiko wa kampuni 2 kubwa, kutoka Amerika ya kusini, ambazo ni POSITIVO yenye makao yako nchini Brazil na BGH yenye makao yake Argentina, kampuni zilianza tangia muda kufanya biashara kwa kuungana na katika moja ya mipango yake ziliamua kuanzisha kiwanda Afrika ili kupanua soko lake.

Kwa nini Rwanda?
Kutokana na maelezo ya Juan Ponelli, Rais wa POSITIVO Afrika, Rwanda imeonesha juhudi kubwa za kusaka maendeleo na pia ina GDP nzuri ya 8.8% ukilinganisha na nchi nyingine hapa Afrika na pia ina utulivu wa kutosha...soma zaidi

Hii ni mojawapo ya kompyuta zinazotengenezwa..

Positivo BGH 11CLE2-R

Specifications
OS: Windows 8.1 Pro
Processor: Intel® Celeron® N2840
Platform: Bay Trail
RAM Memory: 2 GB
Storage: 320 GB
Screen: 11,6"
Camera: 1 Mpx HD
Video: Intel® HD Graphics; DirectX 11
Audio: High Definition
Ports: VGA y HDMI
Memory Reader: 9-in-1 memory multi reader
Security: Kensington port