Fahamu kitovu cha teknolojia( Technology Hub) hapa Tanzania ambacho wanafunzi wa chuo na wataalamu katika nyanja mbali mbali za teknolojia yaani Software developers, Web developers, Electricians, Electronics Engineers and Computer Engineers n.k hukutanika na kuvumbua au kuboresha vitu.

Kitovu cha teknolojia au kwa lugha ya kiingereza technology hub ni sehemu ambazo huanzishwa kwa malengo ya uvumbuzi na utatuzi wa matatizo kwa nji ya teknolojia. 


Kwa Afrika, sehemu hizi zimefikia 314 katika miji 93 katika inchi 42 nchi kama South Afrika ikiwa inaongeza kuwa na vitovu vingi.

Kwa hapa Tanzania, tuna kitovu cha teknolojia kimoja ambacho kinaitwa Buni Hub.

BUNI Hub.
Buni huhusika zaidi na kuwasaidia wanafunzi hata watu wabunifu katika teknolojia kwa kuwapa ushauri(mentoring) na kuwaongoza kupata uwezo wa kufanya ujasiriamali kwa kupitia teknolojia n.k.


BUNI huwa inaendesha semina, mafunzo mafupi mara kwa mara ili kuweza kuwajenga wanachama wake katika uanzishwaji wa project na hata usimamizi wa project hizo za kitaalamu na kuwaongoza waweze kufikia malengo yao.
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya BUNI hapa na wasiliana nao kuweza kujiunga. 

MANUFAA YA KUJIUNGA.
Utajenga uwezo wako binafsi katika kubuni mambo mbali mbali ya kiteknolojia.


Utakutanishwa na watu ambao wana mawazo kama yako ambao watakusaidia kusimama vizuri zaidi.

Ni sehemu ambayo inaweza ikawa uwanda wa wewe kuelewa njia ya kupata hata ufadhili wa kazi yako. 

Muhimu zaidi chochote ambacho hutumii kitapotea na kama wewe ni mwanafunzi wa IT,au kozi zozote za science ni muhimu kuwa pamoja na watu ambao wana elimu kama yako ili elimu yako isije ikalala na ukaanza kufakamia fani za watu wengine.

Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   

Application Programmer huhusika na kudesign, kutest programu katika upande wa logic, pia huandaa documentation na kutengeneza programu kwa ajili ya matumizi ya kampuni husika.


Kazi Afanyazo

  • Anafanya coding, testing, debugging, documenting na installation ya programu.

  • Anatumia lugha maalumu za computer ili kuongeza ufanisi wa programu zinazoendelea kufanya kazi.

  • Anafuatilia ufanyaji kazi wa ufanisi wa programu zote zinazofanya kazi, na kushughulikia mapungufu yote yanayojitokeza.

  • Anatumia mahitaji maalumu ambayo amepewa na kampuni, na kutengeneza programu mbazo zitasaidia kutimiza malengo hayo...mfano: Vodacom wanapotaka kuongeza offer kwenye menu ya MPESA watahitaji kumuona huyu mtu.

  • Muda wote huutumia kujiupdate ili kuhakikisha ya kwamba mifumo yote ya kampuni inafanya kazi katika viwango vya kisasa.

  • Hujifunza na kuchambua kazi mbali mbali za kampuni na kutoa mchango wake katika kuboresha mifumo husika ili kuleta ufanisi wa hali ya juu katika MIS(Management Information Systems).


Vigezo Vya Kazi.
  • Awe na uelewa mzuri wa software na hardware( Technical Capacity)

  • Awe na uwezo mzuri wa kutatua changamoto zote zinazojitokeza kwa kutengeneza majawabu ya kiteknolojia.(Problem Solving/ Analysis)

  • Awe na uwezo wa kujisamamia mwenyewe na kuchukua hatua mbali mbali za kiutendaji(Initiative).

  • Uwe na uwezo mzuri wa kuwasiliana na wengine na kuweza kuwasilisha kile ambacho unataka kufanya kwa lugha nyepesi na ya kueleweka zaidi.

  • Uwe vizuri katika kutumia muda vizuri.


Elimu na Mafunzo
Uwe amepitia kozi zifuatazo , lakini pia awe na ujuzi binafsi wa lugha za computer kama zifuatazo Java, Android, PHP, SQL, HTML,CSS, ASP.Net, Javascript, Python, VB.Net etc.

Bachelor in Computer Science

Bachelor in Information Systems

Bachelor in Software Engineering

Bachelor in Computer Engineering

Bachelor in Information Technology

Na kozi nyingine zinazofanana na hizo hapo juu. 
Kwa maelezo, msaada au ushauri zaidi usisite kuzungumza nami. 

Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa    

elisanteshibanda@yahoo.com

Fahamu Business Analyst ni nani? 
na nini kinahitajika ili kuwa Business Analyst,
ili uweze kufahamu 
kama je una muhitaji mtu kama huyu katika biashara yako au 
ujiandaaje kufanya interview ya nafasi ya Business Analyst na zaidi 
unafanyaje kujiboresha zaidi kama wewe ni Business Analyst.

Business Analyst Ni Nani?

Business Analyst ni mtaalamu ambaye anahusika katika kuisaidia biashara 
kutumia teknolojia kwa gharama nafuu, 
ili kuboresha mfumo wa biashara uweze kuipatia kampuni faida kubwa zaidi.

Chimbuko lao

Hii kazi ilianza kuchukua nafasi kubwa katika karne ya 21, wakiwa na kazi moja kubwa 
ya kuunganisha teknolojia 
iliyopo na utimizaji wa malengo ya kampuni husika.

Kazi yao

Kuleta ufanisi katika uendeshaji wa biashara.

Huhusika katika kupanga mipango mbali na kufuatilia mipango hiyo kwa umakini.


Kufuatilia mahitaji yanayojitokeza siku hadi siku katika uendeshaji wa biashara.


Kuboresha mfumo wa uendeshaji uliokowapo ili ufanye kazi kwa ufanisi zaidi.


Kutafuta majibu ya kiteknolojia juu ya changamoto zote katika mfumo wa uendeshaji wa biashara.


Sifa za kuwa Business Analyst

Uwezo wa kuwasiliana vizuri kwa njia ya kuandika na kuongea, kawaida na kitaalamu zaidi.

Uelewa wa mambo kadha yanayohusu software engineering.

Uwezo wa kufanya cost/benefit analysis.

Uwezo wa kufanya Business Case development

Uwezo wa kutumia modeling techniques 

Uongozi.

Elimu na Mafunzo ya Business Analyst

Kazi hii huwa inahitaji zaidi digrii ya Information technology, Computer Science au Software Engineering na kozi zinazolingana na zilizotajwa hapo juu.

Halafu unatakiwa ila sio lazima upate mafunzo zaidi(Certifications) kama IIBA and CBAP ila ukiwa na hizo   digrii hapo juu unafaa kuanza kazi. 


Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   
Kwa maswali zaidi wasiliana nasi.

Fanya Maandalizi ya Kutosha, ili uweze kufanikiwa na hatimaye kupata kazi kama System Administrator.

Mambo ya Kuzingatia.

👉Uwe umesoma IT au Computer Science au 
  una Elimu ya mambo hayo,  

kwa maana vitu kadhaa ambavyo vinahitajika humo vilishafundishwa katika kozi hizo.




👉Uwe umejiongeza mwenyewe binafsi na unafahamu fika,
nini kinaendelea katika nafasi hiyo, 
kwa maana wewe unahusika na usalama wa taarifa 



nyeti za kampuni na muundo mbinu yote ya Tehama.


👉Itafaa zaidi kama utakuwa una vyeti vya CISCO au Microsoft,



Ili uwaaminishe watu yakuwa wewe unaweza ukaihudumia vizuri mitambo ya IT. Ukitaka kujua ni zipi soma article yangu ya certifications hapa...


👉Cha mwisho lakini cha muhimu sana, jifunze Linux, 



ni muhimu hata Microsoft katika server zake nyeti anatumia Linux.


Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   


Hayo yalikuwa, kutoka kwangu kama IT Consultant.

Yafuatayo yatakusaidia kukuandaa zaidi katika Interview yako....Mungu akusaidie.

Kwa mambo ya kujisomea binafsi, maswali na majibu kwa interview ya kuandika(written)

Link hii hapa...

Kwa mambo ya kujisomea binafsi, maswali na majibu kwa interview ya Kuongea(oral)

Link hii hapa...


Angalia hii video kukubrush na kazi ya System Administration



Hii Video ya pili itakupa kujiamini katika maswali utakayoulizwa...




Kwa ushauri zaidi, wasiliana nami katika elisanteshibanda@yahoo.com.
Interview Njema.

Ulimwengu wa teknolojia ya mtandao yaani Information technology ni mkubwa sana, na  wengi huwa wanajikuta wanashindwa kufikia malengpo yao, kwa  kushindwa kujua tofauti ya kozi zilizopo, hebu fuatilia uelewe kipi ni kipi?

Information Technology

Hii ni kozi ambayo inadili zaidi na mawasiliano ya njia ya kompyuta na uendeshaji wa mifumo/systems ya kompyuta na hata designing. 

kozi hii hutoa watu/professionals ambao ni system administrators,ICT officers, Graphics Designers etc 


watu ambao wapo kwa ajili ya kuwasaidia watu wengine kuweza kutumia vizuri, mifumo ya kompyuta.

Kazi.

Hawa watu wengi huwa wanaajiriwa, 

zaidi ila pia wanaweza kuajiajili kwa katika kufanya maintenance ya vifaa vya ICT, ICT Equipment supply, 

na hata kufunga mifumo ya network sehemu mbali mbali na akijiendeleza huweza kuwa Webmaster wa tovuti mbali mbali.

Kipato.

Mishahara yao hulipwa kulingana na elimu ya Degree au ya diploma aliyonayo kama fani nyingine na Zaidi ikizingatia kazi anayofanya na unyeti wa kazi hiyo.



Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   

Computer science.

Uwanda huu upo ndani zaidi kuliko IT, maana hawa watu mbali na kujua vitu vyote vya kozi ya IT,


pia huweza kujua kutengeneza program za aina mbali mbali za computer, na pia hufundishwa lugha nyingi za computer na huwa wako vizuri kiasi hata kwenye hardware ya computer.

Kazi.

Hawa watu utawakuta kama pia ma system administrators, business analysts, system analysts, ICT Officers, Application programmers, software developers. 

Pia wengi hujiajiari na kuanzisha makampuni/biashara za kutengeneza kompyuta hardware na software, 
websites na kazi nyinginezo nyingi katika uwanda wa technology.

Kipato

Wanapoajiriwa kipato chao hakitofautiani na IT.

Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   

Computer Engineering

Fani hii, hujikita Zaidi na hardware ya computer, huku tunapata watu ambao wanaunda vifaa ambavyo vinaweza fanya kazi na mifumo ya computer. 

Hawa kwa nchi zenye viwanda vya kutengeneza vifaa hivyo,  huwa ni soko kubwa sana, 

ila kwa nchi ambazo zinaendelea huwa bado wana soko dogo sana, na hata huogopwa kuajiriwa kulingana na Title yao ya Kuwa engineer.

Kazi.

Hawa hufanya kazi ya kutengeneza vifaa ila pia huweza kufanya kazi nyingi ambazo mtu wa computer science anafanya, 
pia ni mafundi waliobobea katika kurekebisha computer mbovu.

Kipato

Hawa huwa na mshahara wa juu kuliko IT na Computer Science, maana hulipwa katika kiwango cha ma engineers,

 lakini pia hufungua biashara kubwa za computer maintenance na hardware Suppliers na zaidi...
  

Software engineering

Katika Fani hii tunakutana na watu ambao wanataka kubobea katika kutengeneza programu za computer, 

hawa watadeal na program tuu na kidgo sana mambo mengine katika fani ya teknolojia.


Kazi.

Hawa hufanya kazi kutengeneza program za kila aina, pia huingia kwenye network na kubobea humo,

na huwa pia kuweza kufanya kazi za Computer Science kwa kiasi na hukinzana kabisa na computer engineers maana wao hufanya kazi na hardware.

Kipato

Hawa wana mshahara mkubwa wa kiwango cha Engineer kama computer engineer anavyolipwa na pia huwa wanajiajiri sana na kuanzisha makampuni ya kutengeneza programu.

 

Jinsi ya Kujiendeleza…

Ulimwengu wa Computer umejaa vyeti vya mafunzo mbali, 

ili mtu abobee katika sehemu maalumu hizo huitwa certifications mfano mafunzo ya Network hutoa vyeti,

kama CCNA, CCNP na kuendelea na mafunzo ya database kama Oracle , na hata auditing(Ukaguzi) kwa maelezo Zaidi fuatilia article yangu ya kuhusu certications za IT.


Lakini pia anaweza jiendeleza katika masters degree za vitu mbali na hata kuwa Tutorial au lecturer au professor maana bado kuna upungufu mkubwa mno katika ngazi hizo.

Kwa muongozo zaidi, Wasiliana nami katika email elisanteshibanda@yahoo.com au

Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa    



 

Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   



Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   


Fahamu jinsi ya kuuingiza biashara yako katika ulimwengu wa kisasa wa computer, wenye ufanisi na faida kwako maradufu.

Programu ni kitu gani?

Programu ni maelekezo ambayo huandikwa na mwanadamu katika lugha za ki computer ili computer iweze kuyafuata na kurahisisha ufanyikaji wa kazi fulani.

Ni biashara gani unaweza tumia 

programu hizi?

Biashara ya aina yeyote ile inaweza kurahishishwa uendeshaji wake, kwa asilimia 80% na zaidi, katika uendeshaji wake.

Faida ya kutumia programu ni zipi?

Faida ni nyingi sana ila kuzitaja kwa uharaka ni kurahisisha uendeshaji wa biashara mfano duka linalotumia programu katika kuhifadhi mauzo yake, huwa lina uwezo kujua nini kipo na nini kimekwisha kwa uharaka zaidi na hata ni bidhaa gani imekwisha muda wake wa matumizi kwa uharaka zaidi na pia hata kujua faida iliyopatikana kwa siku mara moja, kwa kubonyeza button moja tuu na hata kujua biashara inaendeleaje na hata kupewa ushauri na programu hiyo hiyo kipi cha kuongeza na kipi kimekaa muda mrefu.

Aina za programu ambazo hutumika.

Programu hizi zipo na zinatofautiana kutokana na vipengele vifuatavyo.
·         MICROSOFT OFFICE
Hapa kuna programu ambazo zenyewe zimetengenezwa kwa ajili ya shughuli zote za kibiashara na za kiofisi, hizi mfano ni Microsoft office package, hizi hutumiwa kwenye biashara yeyote ile, kwa mafunzo mafupi sana.
Pia Kuna programu ambazo zinatengenezwa mahususi kwa ajili ya biashara yako na wataalamu wa computer ambao wewe utawalipa kwa ajili ya kazi hiyo, programu hizi huwa na ufanisi mkubwa mno kulinganisha na hizo za awali hapo juu.

·       BUSINESS MANAGEMENT SOFTWARE
Kuna programu ambazo zimeshatengenezwa teyari kwa ajili ya kazi hiyo, nikiamaanisha mfano microsoft office zenyewe ni gharama nafuu zaidi kuanza kutumia, chini sana ukilinganisha na  kundi la programu za hapo juu.
Jinsi ya kupata programu mahususi 

ajili ya biashara yako.
 Ondoa shaka kabisa hapa kuna wataalamu mbali mbali ambao wamebobea katika utengenezaji wa programu hizi kwa sasa ni....
·         Duka Pro
·         Nyumbani Creative
Endapo utahitaji maelezo mengine yeyote zaidi, kuhusu maswala haya, usisite kuwasiliana nami, nitakusadia zaidi katika elisanteshibanda@yahoo.com na +255753592886 
 Jinsi ya kupata programu ya kiofisi 
  ajili ya biashara yako.

Jinsi ya kupata programu hizi na mafunzo ya jinsi ya kuitumia, tafadhali wasiliana nami pia kwa namba nilizozitoa hapo juu au unaweza kutafuta madukani na wakakuwekea kwa gharama nafuu zaidi ila kwa mafunzo inabidi utafute vyuo vinavyotoa mafunzo ya "computer course" ambayo pia hata mimi ni trainer/mwalimu wa hayo mafunzo ndani ya wiki chache tuu utakuwa teyari kabisa.
  Hitimisho

Computer huwa zinaathiriwa na virusi na hata watu wenye nia mbaya wanaweza ingia na kufuta taarifa zako, kwa hiyo kuwa makini computer yako kujua nani anaitumia na jee ni muhusika, na pia kutumia programu za kujikinga na virus zinazoitwa Anti-Virus mfano Karspesky na zaidi hifadhi data zako sehemu mbali mbali mfano kwenye external drives, flash drives na internet.









Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   


Jinsi ya Kujifunza Web Design and Graphics Design Kwa urahisi. 

Web Design/Development 

Katika mambo ya tovuti au website huwa zinatengenezwa na Lugha mbali mbali za  computer ambazo ni

  1. HTML 
  2. CSS  
  3. JAVASCRIPT 

Hizo ni lugha kuu lakini website za kisasa zinahitaji Lugha zifuatazi ili ziwe nzuri zaidi JQUEERY, PHP na lugha nyingine za database  mfano SQL na uelewa wa kawaida wajinsi  database zinazyofanya kazi na jinsi ya kuziunganisha na tovuti, pindi tu kama tovuti itahitaji kuwa na uwezo wa kusajili watu na kufanya kazi nyingine.

Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   

JINSI YA KUSOMA

 Siku hzi kila kitu kipo kwenye mtandao wa internet, nakushauri tumia zaidi videos uweze kusoma kwa haraka zaidi,jinsi ya kupata elimu hii ingia kwenye mtandao wa youtube na search kwa njia hii… andika web design for beginners, html for beginners ,css for beginners  and  javascript for beginners 
Au
Ili upate vitabu andika google free HTML,CSS and Javascript for beginners .PDF na kila lugha I search kwa kuishia mwisho .PDF na kuanzia na free.

Blogs. 

Blogs ni rahisi kutengeneza unaweza ukatengeneza hata kama huna knowledge ya Code hata moja au hizo programming language.  Kama kawaida nenda youtube andika how to design a blog or blogging for beginners ili uweze kupata knowledge zaidi juu ya hayo mambo.
 Kuna makampuni kadhaa yanayokupa wewe uwezo wewe wakutengeneza blogu nayo ni Blogger na Wordpress na kumbuka blogu unaweza kuifanya ndio ikawa website kabisa ukiisajili kwenye mtandao kwa malipo maalumu. 
Angalizo. 
Ujuzi wa hizo lugha ni muhimu sana maana utakusadia kuweza pia kuikarabati blogu yako kitaalamu zaidi.

Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa   

 Graphics Design

Fani hii inaundwa kwa kujifunza program zinafanya kazi ya kutengeneza vitu ambavyo nimevitaja hapo juu.
Graphics Design inahitaji ujifunze program zifuatazo;

  • Adobe Photoshop**)Kwa ajili ya photo digital editing 
  • Adobe Illustrator**) Kwa ajili ya Drawing/digital art creation. 
  • Adobe InDesign**)Kwa ajili ya kutengeneza vitabu, magazeti au hata vipeperushi.  

Jinsi ya kujifunza ni rahisi sana, Tumia Zaidi mtandao wa Youtube.com search ifuatavyo; 

  1. Kujifunza Photoshop**) Adobe photoshop cc for beginners.
  2.  Kujifunza Illustrator**)Adobe Illustrator CC for beginners.
  3. Kujifunza InDesign**)Adobe indesign CC for beginners. 

Program za kuweka, tafuta program zifuatazo; 

  • Adobe photoshop CC au Adobe Photoshop 2017 
  • Adobe Illustrator CC au Adobe Illustrator 2017 
  • Adobe InDesign CC au Adobe InDesign 2017 

Watu wazuri kwenye Youtube wanaitwa tastetusty wako vizuri sana. 

Kwa Taarifa, Maswali, fursa mbali mbali za IT hapa Tanzania na Africa Mashariki, pamoja na kozi fupi za ujuzi mbali mbali katika IT(information Technology),jiunge na group la whatsapp la MAXPO Tanzania Maximize your potential Bonyeza hapa