Hebu jaribu kuchukua nafasi ya Human resource manager(Meneja wa rasilimali za binadamu) akiwa amepokea maombi ya watu 5000 kwa ajili ya nafasi moja ya kazi aliyoitangaza, unadhani atapitia na CV yako kwa jinsi ilivyo? 😓

Basi kama unataka kufanya CV yako, ipendeze kimuonekano na hata iweze kumzuia meneja aliyechoka kupitia CV za watu hebu ingia hapa tengeneza akaunti yako bure na fuata maelekezo maana ni rahisi mno kutumia.
 
  • Kwanza Relax acha uoga na punguza presha, kutype ni kitu chepesi sana.
  • Fahamu herifu za kompyuta zilipo na ukumbuke taratibu taratibu mahali zilipo kila moja hata ikiwa moja kwa siku.
  • Acha kutype kwa kidole kimoja, tafadhali weka mikono yako yote kwenye keyboard na yote ifanye kazi ya kutype.
  • Acha kutumia kidole kimoja kwa kutype kwa kila mkono, tumia vidole vyote kwa kila mkono.
  •  Hakikisha kila kidole kina herufi ambazo kina husika na kutype zinaweza zikawa mbili au tatu ...mfano kidole changu kidogo kinahusika na herufi A,Q huku kidole gumba kikitumika kwa space.
  • Usiogope kukosea kutype herufi pindi unapotype kwa haraka maana hamna shortcut lazima ukubali makosa ili uweze kupata spidi nzuri ya kutype.
  • Tumia programu za bure kabisa za kukufundisha kutype ndani ya wiki moja utakuwa vizuri kabisa. mfano: tembelea hapoa ujipatie programu yako ya bure www.typingmaster.com
  1. Usiishi katika mitandao ya kijamii HAMNA MAISHA HUKO UNAJIDANGANYA TUU!!
Siku ina masaa 24, usitumie masaa mengi huko maana sio maisha halisi kama unavyodhani. kaa na watu unaowajali zaidi, watu halisi wa karibu yako ie majirani,utakapoumwa au kuwa na tatizo la ghafla huyo rafiki yako mbelgiji au mnamibia au muafrika ya kusini hataweza kukusaidia.

    2.Usipende kuandika ujinga.
Katika ulimwengu wa sasa, watu wengi hutafuta kuwafahamu wengine katika uelewana hekima kwa vile wanavyoandika kwenye mitandao ya kijamii, kwa hali hiyo waajiri kama serikali na makampuni huhakiki sana watu kabla hawajawaajiri kuwa ni wema.

   3.Usipige picha za ajabu na zisizona maadili.
Hili wote tulishuhudia pale muheshimiwa alipoteua wanawake kadhaa na pindi tuu walipoingia ofisini ghafla picha zao za ajabu zikaibuka mitandaoni zikiwachafua wao na muheshimiwa kwa ujumla akishushiwa hadhi yake.

   4.Usipende kuandika taarifa zinazoonyesha mahali ulipo.
Ni vyema kushare mahali ulipo kama ni pazuri lakini kumbuka kuna waovu wengi wanaweza kuchukulia hiyo kama nafasi ya kukufanyia uhalifu wewe au familia yako ulipoiacha...hizi ni nyakati ngumu.

   5.Usitaje majina ya watu mashuhuri au yeyote yule pale unapoandika kitu.
Sheria ya Tanzania ya mtandao ni kali sana, hata kama mamia wamemtaja wewe unashauriwa usimtaje maana huo ndio utakuwa ushahidi tosha wa kukufunga...Hili limekuwa tatizo hata tunaona muheshimiwa raisi amekuwa akikamata wengi ambao wanamtukana, hafanyi ubabe au hayuko njee ya sheria, yuko katika sheria kabisa na ana haki ya kumshtaki yeyote atakayemnenea vibaya bila kibali chake.

   6.Unapotumiwa picha chafu na mtu yeyote yule futa na umkanye huyo mtu na kama una uwezo nenda hata polisi kama utakuwa hujafuta hizo picha kama unataka huyo mtu akamatwe.

   7.Usikubali kuwa tagged katika post zozote zile za uchochezi au uchafu wowote ule.

  8.Kama una addiction au tatizo la kutumia mitandao hii bila kipimo, vunja kwa kutafuta kitu cha kuchukua nafasi yake hiyo taratibu taratibu..mfano anza kujiuliza taratibu maswali kama "Una hela za kutosha? unaenda wapi? uko wapi?" pia FANYA KAZI,  Omba Mungu akusaidie na incase ACHA UMBEA.


Kutokana na  maendeleo ya kiteknolojia, sio jambo la kuepuka tena kufanya manunuzi kwa njia mtandao wa internet, maana umejaa vitu vya thamani ndogo na vizuri lakini pia umejaa wezi.  Fuatilia haya ili uweze kufanya manunuzi bila kujutia...

  1. Fungua akaunti pekee benki ambayo itatumika kwa ajili ya matumizi hayo ya manunuzi tuu, na uweke hela tuu pale pindi unapotaka kununua vitu, tunafanya hivyo ili endapo akaunti ikafikiwa na wezi wasiweze kuiba chochote.
  2. Pata elimu ya kutosha benki juu ya kitu gani cha kulinda kuhusu taarifa zako.
  3. Nunua sehemu maarufu au kwenye tovuti zinazofahamika dunia nzima kwa manunuzi mfano...GooglePlay, Amazon,eBay na alibaba.
  4. Usimtumie mtu usiyemfahamu taarifa zako za kibenki kwa njia ya email au yeyote ile.
  5. Hakikisha katika browser yako wakati unataka kufanya manunuzi pale kwenye sehemu ya address  imeandikwa au inaanza address kwa njia hii "HTTPS://....." na sio "HTTP://...." ina maana ya kitaalamu "Hyper text transfer protocol secure"
  6. Jiridhishe ya kwamba hiyo ndio tovuti yenyewe au kuna mtu ametengeneza tovuti feki ili kukuibia taarifa zako.
  7. Ukimaliza kufanya manunuzi yako ni vyema zaidi ukafuta browsing history yako yote ili kufuta cookies zenye mabaki ya taarifa zako.
  8. Muone mtaalamu wa Ecommerce ili akusaidie unapotaka kufanya manunuzi makubwa.

Battery hutumika kuendesha umeme ndani ya laptop yako endapo pale unapokuwa hujaichomeka kwenye charge laptop yako.



Uharibifu unaofanyika.
  1. Unapotumia laptop ikiwa imechomekwa kwenye umeme siku nzima bila kuichomoa pale battery inapojaa.
  2. Unaposafiri kwa muda mrefu au kiacha laptop bila kuitumia kwa muda mrefu, na kuiacha battery ya laptop ndani ya laptop bila kuitoa.
  3. Unaponunua adapter feki ili kuchaji battery ya laptop yako.
Ufumbuzi.
  • Laptop ikijaa charge chomoa kwenye umeme na ikiisha chomeka.
  • Ukiona unasumbuka na chomeka chomoa ya hapo juu, tafuta energy management software hiyo itakusadia.
  • Unaposafiri kwa muda mrefu zaidi ya siku moja au kupanga kuto kuitumia laptop yako kwa muda mrefu, chomoa battery ya laptop na uihifadhi mahali salama.
  • Tumia vifaa au adapter original vya laptop husika vyenye meno matatu(Earth,Live and Neutral).
  • Ukiona hali inakuwa mbaya omba msaada.





Anti-Virus ni programu ambayo hutumika kuilinda kompyuta, kutoka kwa mashambulizi ya virusi ambavyo huathiri mifumo yake na uwezo wake wa kiutendaji kazi.


Jinsi Anti-virus inavyofanya kazi.
kama bodyguard anavyomlinda mtu, basi na anti-virus hulinda kompyuta kwa staili hiyo. Yenyewe huhakiki na kupitia kila kinachofanywa na kompyuta ili kuweza kujua kama kitakuwa na madhara au la!
Mfano:
Unapoingiza tuu flash yako kwenye kompyuta kabla hata hujaifungua anti virus ni ya kwanza kuleta warning kama kuna kirusi au la kwa sababu imeshaipitia kabla.


Tatizo lilipo:
Kutokana na kitendo hicho processor ya kompyuta hufanya kazi mara mbili zaidi kwa kila kitendo kinachofanyika, ya kwanza ikiwa ni kazi ya Anti virus(ukaguzi) na ya pili ikiwa ni kazi ya Operating system(windows) ya kumhudumia mtumiaji matakwa yake.
kwa hali hiyo anti virus kubwa zenye nguvu kama karspesky, avg, avast huhitaji uwezo mkubwa zaidi wa ukokotoaji ili ziweze kufanya kazi na kompyuta na endapo uwezo wa kompyuta ni mdogo, hapo husababisha kompyuta kufanya kazi kwa utaratibu na hata husababisha ukwamaji(stucking) wa kompyuta ikiwa inafanya kazi mara kwa mara.


Ushauri.
kwa matumizi ya sasa unashauriwa kuongeza uwezo wako wa kompyuta mpaka kufikia RAM=4GB na zaidi muone mtaalamu wa tehama ili aweze kukusaidia kusimamia matumizi mazuri ya diski yako inayobeba Operating system iwe na nafasi ya kutosha.

Je ni nani mwenye kiwanda hichi? na ni kwa nini Rwanda, je kompyuta hizi zina uwezo gani?

Soma zaidi.. Rwanda ni kati ya nchi zinazokua kiuchumi kwa kasi hapa katika Afrika Mashariki na miaka ya hivi karibuni imeanzisha utengenezwaji wa kompyuta, kwa kusaini mkataba na kuiruhusu kampuni ya POSITIVO BGH kuweza kuanza utengenezaji wa kompyuta nchini mwake.

POSITIVO BGH  ni muunganiko wa kampuni 2 kubwa, kutoka Amerika ya kusini, ambazo ni POSITIVO yenye makao yako nchini Brazil na BGH yenye makao yake Argentina, kampuni zilianza tangia muda kufanya biashara kwa kuungana na katika moja ya mipango yake ziliamua kuanzisha kiwanda Afrika ili kupanua soko lake.

Kwa nini Rwanda?
Kutokana na maelezo ya Juan Ponelli, Rais wa POSITIVO Afrika, Rwanda imeonesha juhudi kubwa za kusaka maendeleo na pia ina GDP nzuri ya 8.8% ukilinganisha na nchi nyingine hapa Afrika na pia ina utulivu wa kutosha...soma zaidi

Hii ni mojawapo ya kompyuta zinazotengenezwa..

Positivo BGH 11CLE2-R

Specifications
OS: Windows 8.1 Pro
Processor: Intel® Celeron® N2840
Platform: Bay Trail
RAM Memory: 2 GB
Storage: 320 GB
Screen: 11,6"
Camera: 1 Mpx HD
Video: Intel® HD Graphics; DirectX 11
Audio: High Definition
Ports: VGA y HDMI
Memory Reader: 9-in-1 memory multi reader
Security: Kensington port


Kompyuta ni kama yalivyo magari, yanatembea na ya na kimbi lakini yanatofautiana na yana hadhi na uwezo tofauti kulingana na mtengenezaji.
Kwanza nakupa aina ya kompyuta pamoja na matumizi yanayofaa zaidi.
LAPTOP VS DESKTOP
  • Unashauriwa kutumia desktop maofisini kwa sababu zifuatazo za kiulinzi na za kiusalama, kwani ni rahisi kwa laptop kuibwa na nyaraka nyingi kupotea au kuibiwa kuliko desktop, na pia kompyuta ya desktop  ina uwezo mkubwa sana ukilinganisha na kompyuta ya laptop.
  • Unashauriwa kutumia laptop kama ni mfanyabiashara au mwanafunzi,kwa sababu ya wewe kuhitajika kutembea mara kwa mara na kompyuta yako ila inakupasa kuwa na desktop au external hard drive,  mahali ili kuweza kuwa na back up ya data zako.
MAKAMPUNI YA KOMPYUTA NA SIFA ZAKE
HP
Kompyuta hizi zina uimara mkubwa sana na hudumu kwa muda mrefu sana,pia zina hali ya juu ya utendaji na mara nyingi hutumiwa kwakazi zinazohitaji ukokotoaji mkubwa. Pia hutumika katika kwenye tasnia ya uhandisi na hata designing.

DELL
 Kompyuta hizi zina sifa ya ubora sana zaidi husifika kwa kioo(monitor) chake kizuri sana cha HD(High definition) ambacho ni kizuri kuliko vya computer nyingine.

Kompyuta hizi hutumika sana maofisini na hata kwa kujiliwaza kwa kuangalia videos kutokana na ubora wa kioo chake.

LENOVO
Kompyuta hizi zinasifika kwa kuishi kwa muda mrefu kama ikitumika kwa matumizi ya kawaida, yaani yasiyo hitaji ukokotoaji wa hali ya juu.,kama kuangalia movies sana na kucheza michezo kama fifa, magari.

APPLE
Kompyuta hizi zina ubora wa hali ya juu pamoja na uwezo mkubwa sana na pia hudumu kwa muda mrefu. Katika USALAMA haziingiwi na virus kama kompyuta nyingine na ikitokea vimeingia ni mara chache sana. UTENDAJI wake ni mkubwa maana zina nguvu kubwa za ukokotoaji. Pia ni rahisi kubeba kwa maana ni nyembamba na nyepesi kubeba, na zaidi hutumika zaidi kufanya Graphics Design.

MUHIMU 
Nimejaribu kukupa mwanga kuhusu makampuni haya, haimaanishi mapungufu haya utayakuta katika kompyuta zao zote, kwa maana hushughulika kila siku kuweza kurekebisha mapungufu hayo. Ni bora kununua kompyuta za toleo jipya kuweza kuepukana na shida zozote..


 



Unatafuta kununua laptop Dar es Salaam lakini hujui uanze wapi? Soko la Dar lina laptop mpya, refurbished na mitumba — lakini bila mwongozo sahihi unaweza kupoteza hela au kununua laptop isiyofaa mahitaji yako.

Huu ni mwongozo kamili wa kukusaidia kununua laptop bora kulingana na matumizi yako.


Laptop Bora kwa Wanafunzi na Matumizi ya Ofisini

Kwa matumizi ya kawaida kama Microsoft Office, internet, online classes na software za ofisini, chagua laptop yenye:

  • 8GB RAM minimum

  • Intel Core i3 11th Gen au Ryzen 3 (au zaidi)

  • SSD 512GB(ili upate nafasi ya kuhifadhi vitu vyako, MUHIMU SANA)

  • 64-bit system

Hii ni laptop nzuri kwa wanafunzi wa vyuo, wafanyakazi na biashara ndogo.


Laptop Bora kwa Graphic Design na Gaming Dar es Salaam

Kwa kazi nzito kama video editing, graphic design au gaming, tafuta laptop yenye:

  • 16GB – 32GB RAM

  • Intel Core i5/i7 12th Gen au Ryzen 5/7

  • Graphics card ya NVIDIA GTX/RTX

  • SSD 512GB au 1TB

Hizi ndizo laptop zinazofaa kwa wabunifu na content creators.


Tofauti ya SSD na HDD Drives.

Laptop yenye SSD ina speed sana kuliko HDD, ila SSD ina gharama kubwa hivyo ni rahsi wauzaji kukuuzia space ndgo kama 256GB ambayo baadaye itakuja kuleta shida kwenye performance utakapoanza kuhifadhi vitu vyako na software nyingine.


Ukiona laptop bei ndogo sana lakini ina HDD, fahamu performance itakuwa polepole.


Jinsi ya Kuthibitisha Specs za Laptop

Washa laptop → Right-click This PC → Properties
Angalia RAM, Processor na System type.

Usikubali kununua laptop bila kuthibitisha specs mwenyewe.


Je, Ununue Laptop Mpya au Refurbished Dar es Salaam?

Laptop refurbished inaweza kuwa nzuri kama:

  • Ina warranty

  • Battery iko sawa

  • Haina cracks

Lakini bei lazima iwe chini ya mpya.


Hitimisho

Kununua laptop Dar es Salaam siyo suala la bahati — ni suala la maarifa.

Chagua laptop kulingana na matumizi yako, hakikisha ina SSD, thibitisha specs na nunua sehemu yenye warranty.

Ukifanya hivi, utaepuka hasara na kupata thamani ya pesa yako.


Imeandaliwa na 
Elisante Shibanda.
 
Usipate tabu tena, jifunze computer kwa lugha ya asili yako,lugha unayoielewa, Lugha ya Kiswahili.
Hii ni zawadi kutoka ECL Computer Clinic bure kabisa na wewe ufahamu kutumia computer. Furahia zawadi hii.Soma Kitabu hapa