Sanaa ya Matangazo ni mojawapo ya vitu vinachangia mvuto mkubwa wa bidhaa inayotangazwa, Nini cha kufanya unapohitaji tangazo bora.

Kwanza kabisa onyesha uhalisia kwa kiasi juu ya biashara yako, unapotengeneza tangazo ambalo ni perfect sana, yaani halina uhalisia wa uwezo wako kiasi au uhalisia wa Nchi husika, husababisha watu wakuone wewe ni feki. lakini zaidi la muhimu zingatia ushauri wa mafundi wa sanaa hii.
Mfano mzuri angalia matangazo ya mitandao ya simu, huvutia wengi.

Kwa ushauri na utengenezaji wa matangazo haya karibu uongee nasi.
Vitendo 100%, utajifunza kutoka kwa walimu na Washauri katika sekta hii ya IT, Field Trip kwa makampuni yaliyobobea katika fani hii na zaidi ya yote tuna ratiba zinazojali muda wako.

Karibu katika madarasa yetu hapa  AMD Academy ghorofa ya 19, RITA Towers, karibu na POSTA MPYA(madarasa yenye viyoyozi safi, mwanga safi and muonekano mzuri wa bahari)...Tupigie AMD Academy 0656480666.
Tovuti ama kwa jina la kiingereza(website) imekuwa ni kama mavazi ya biashara katika mtandao wa Internet.

Nimeona Clients wengi wakibadili mawazo kwa kutembelea tovuti ya biashara ya wahusika mara moja, pale wanapokuta tovuti haina ufanisi wa hali ya juu au inachelewa kufunguka au ina muonekano mbaya.
 Siku zote hakikisha tovuti yako ina uwezo mkubwa, inapendeza na kuvutia watu haswa pale inapofunguka kwenye simu za mkononi na imekuwa hosted katika server bora na zenye ufanisi wa hali ya juu kabisa.

ECL Computer Clinic huwa tunachukua hatua za ziada kutafuta server bora duniani na kuhost tovuti za wateja wetu huku tukihakikisha zinapata usajili wa Tanzania na zinakubalika na watu wote na rika lote mfano Apollo Heavy Equipment Limited , Bright Future Academy  and so on.... karibu ufanye kazi nasi.

Ni vyema kupata ushauri wa kitaalamu kabla ya kufanya mabadiliko yeyote yale yanahusiana na teknolojia...

Ni kwa sababu zifuatazo
Usalama
Katika ulimwengu wa leo, kuna wizi mwingi sana katika mitandao haswa katika teknolojia inayohusiana na kompyuta, na hata tuna taarifa ya kwamza hapa Tanzania tupo katika nchi chache duniani ambapo wizi mwingi hutokea.

Mabadiliko ya Teknolojia
Teknolojia hubadilika mara kwa mara, unayotaka kutumia au kununua leo inaweza ikawa ishatoka katika usasa na ni ya zamani na inatakiwa kubadilishwa kutokana na sababu za kiusalama. Kwa hiyo ukajikuta umepoteza pesa zako nyingi.

Sheria na Matakwa ya Nchi Husika
Sio kila teknolojia unaweza kuitumia Tanzania au nchi nyingine na hata kuna njia ya kutengeneza system yeyote ili ikidhi viwango vya nchi husika mfano katika maswala ya usajili wa tovuti kwa Tanzania kuna sheria mahususi ambazo ni za kipekee kabisa hazipo duniani kote.

Kupata Wataalamu Husika
Sio kila aliye kwenye fani hii ni bora na anafaa kutumiwa, wengine wana uwezo tofauti na utawapata kulingana na mfuko wako.